Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,181
Jinsi Msajili wa vyama anachochea migogoro ndani ya CUF inatia mashaka makubwa juu ya upeo wake na uwezo wake wa kuimudu nafasi hiyo.
Mifano michache inaasharia hata alipokuwa High Court alikuwa anajivunia dhuluma ndani ya moyo wake,:-
1) Upo uamuzi wa High Court ambao haujapingwa unaoelekeza ofisi ya Msajili haina ubavu wa kutatua migogoro ndani ya vyama vya siasa. Bila kujua ule uamuzi unambana kama mtendaji Mheshimiwa Mutungi akajisahau na kuchukulia bado yuko High Court ambako maamuzi yake hayambani bali ya Court of Appeals.
Sasa haya ni mapungufu makubwa ya kiupeo. Laiti angelikuwa na upeo mkubwa angeliweza kutambua ofisi ya Msajili siyo ya kimahakama bali ni ya kiutendaji hivyo inabanwa na maamuzi ya kimahakama.
Pili, kumtambua Magdalena Sakaya ambaye alisimamishwa uanachama na aliandika barua ya kupinga uamuzi tajwa kwa Baraza kuu la CUF ambalo hadi leo halijakutana kunazidi kukoleza marashi ya upeo hafifu wa huyu Msajili ambaye yaelekea anaubutu wa kutafakari. Ningelipenda sana kujua matokeo yake kidato cha nne, sita na ile LLB. Kuna uwezekano mkubwa alikuwa ni kilaza na hili tusishangae kwani vilaza tunao wengi kwenye utumishi wa umma na kupelekea uchumi kudorora.
Sijui Mheshimiwa Jaji Mutungi kala maharagwe ya wapi hata akafanyia kazi barua ya kaimu katibu mkuu wa CUF ambaye ni batili; Magdalena Sakaya, hadi kupitisha majina feki ya wagombea wa EALA!
Jingine ni kikao ambacho Prof. Lipumba alidai kilifanya maamuzi tajwa ni batili na hakitambuliwi na katiba ya CUF.
USHAURI.
Ninajua Jaji Mutungi ni kada wa CCM na kapachikwa nafasi hiyo kwa minaajili ya kuvidhoofisha vyama vya upinzani lakini ajue upeo wa kutekeleza hiyo dhuluma Mwenyezi Mungu kamnyima kwa kuelewa hilo ndiyo maana ana laana ya ukilaza.