Jaji mstaafu Augustino Ramadhani chukua fomu

Jaji mstaafu Augustino Ramadhani chukua fomu

Naamini watanzania wengi wanamawazo kama yako,mh jaji Agustino Ramadhani anaweza kabisa kurejesha imani ya wengi kupitia CCM na hata kule visiwani watamkubali
 
Kweli watu wazuri bado wapo hata Mzee Iddi Simba anafaa kupewa urais
 
Naamini watanzania wengi wanamawazo kama yako,mh jaji Agustino Ramadhani anaweza kabisa kurejesha imani ya wengi kupitia CCM na hata kule visiwani watamkubali

Nikisoma kesi ya Mtikila ll sitaki kabisa kumsikia huyo jaji Ramadhani.
 
Ni vigumu kutokotoa gharama au faida halisi za helikopta kwa minajili ya fedha tu. Faida iliyoipata chadema baada ya matokeo haya ni zaidi ya hizo kura. Siamini kwamba matokeo ya mashindano katika siasa yanapimwa kwa kura peke yake. Siasa sio kama mchezo wa mpira wa miguu ambayo matokeo yake hujali takwimu za mwisho wa mchezo. Ninaamini kabisa kampeni za chadema katika uchaguzi uliopita zilikinufaisha chadema sana. Hata kitendo cha kuijadili chadema kwenye forum hii na sio vyama vingine vya upinzani ni mafanikio hayo ya kampeni za chadema. Kwa hiyo tunapojadili faida na hasara za helicopta kwa chadema inabidi tuende zaidi ya takwimu za mwisho za matokeo ya uchaguzi. Hata hivyo, itabidi tumuombe bwana JJ atuletee takwimu za gharama za kampeni kama chadema wangetumia magari na wakaenda katika maeneo yaleyale waliyokwenda kwa kutumia helkopta. Kuna haja pia kufanya utafiti halisi juu ya maoni ya watanzania kuhusu chadema kutumia helikopta katika kampeni kama ilikisaidia kisiasa au la. Tatizo letu wengi kwenye forum tunapenda zaidi kuongea kwa kutumwa na hisia na sio ushahidi wa kisayansi na bila takwimu zozote zilizo laini au ngumu.

Kuhusu hoja inayojirudia rudia kwamba chadema wasingegombea urais na wangejikita zaidi katika kusaka wabunge. Hii hoja hahuanika na hali halisi ya siasa za nchi hii. Ikumbukwe kwamba chadema iligombea urais kwa mara ya kwanza 2005 tangu kuanzaishwa kwa mfumo wa vyama vingi na waliwekeza nguvu zote katika ubunge. Matokeo yake walipata wabunge 2 (1995) na 3(2000). Zaidi ya yote katika kipindi chochote ambacho CHADEMA haikugombea urais umaarufu wake ulikuwa unalingana na chama cha NLD na ilikuwa nyuma kabisa ya nccr-mageuzi(utafiti wa REDET). Lakini kitendo cha kugombea urais kimeifanya chadema iwe masikioni, machoni na midomoni mwa watanzania waliopo ndani na nje ya nchi. Huu ni mtaji mkubwa. Jitihada zinazofanyika sasa ni kuihamisha chadema kutoka kwenye midomo, macho na masikio ya watanzania kuipeleka kwenye mikono na viganja vyao ili umaarufu wa chadema ubadilike kuwa kura katika chaguzi zijazo.

Hivi zile pesa za mauzo ya UDA Idd Simba alisema ni kwanini vile yalilipwa kwenye akaunti yake binafsi? Kana kuna mtu aliyekuwa na wadhifa katika serikali hii na hakuiba, basi huyo ni wakupimwa akili.
 
Amemaliza vizuri, kwa heshima zote, sijui amerudi kufanya nini, huyu jamaa anawadanganya sana wenzake, babu wa watu atajuta.
 
Back
Top Bottom