Jaji Mkuu Prof Ibrahim jiuzulu umeshindwa usimamizi

Jaji Mkuu Prof Ibrahim jiuzulu umeshindwa usimamizi

MtuHabari

JF-Expert Member
Joined
Oct 16, 2020
Posts
321
Reaction score
1,020
Uendeshaji wa kesi ya kunajisi Bunge Tukufu la wananchi ya kuingia wabunge 19 ulipaswa kuwa katika rada zako na kuhakikisha hauwezi kuendeshwa kama kesi ya talaka.

Kama Jaji Mkuu unafahamu uzito wa mhimili wa Bunge, je ni halali kweli kesi kama ile ya wale 19 kuchukuwa muda wote na kuleta hasira kwenye jamii hadi inaleta Maandamano nchini kwa Bawacha ambao hasa wale Covid 19 walipaswa kusema wanaiwakilisha Bawacha?

Uliona kesi za maslahi ya wananchi zinavyo endeshwa kama ile kesi ya uchaguzi Kenya?

Sasa wewe kila leo uko kwenye sherehe za kuapishana Ikulu lini unakaa ofisini na kufuatilia Majaji wako wanasukuma haraka issue zenye public interest haraka?

JIUZULU maana umekuwa CEREMONIAL CHIEF JUSTICE.
 
Kesi inasikilizwa mara moja kwa miezi 8, Jaji mkuu wa hovyo kabisa kuwahi kutokea
Hajui kuwa mambo haya ndio yanaleta political unrest.

Haya maandamano ya Bawacha yanaweza kuchochea wengine kuingiza agenda zao na nchi ikaanza kuchafuka kisa mtu mmoja mwenye cheo kasinzia.
 
Jaji mwenye mitazamo ya kijamaa siku zote huamini kwenye kuitii serikali kwanza,kisha haki baadae. Kwa viongozi wa kisiasa kuujua udhaifu wake, ndio maana aliwekwa muda mrefu kama kaimu jaji mkuu, bila kuonyesha kuwa ni kutokufuata sheria. Sasa kama ameshindwa hata kutetea eneo lake, ataweza kusimamia haki za wengine?
 
Ila hakika awamu ya tano ilituletea mizigo isiyobebeka na ya hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom