Jaji Mgeta: They were convicted of those counts on the mere statements

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
"Nimesoma rufaa ya kesi ambayo Freeman Mbowe na wenzake walifungwa, Jaji wa mahakama kuu wanasema "nothing more is said in the judgement about evidence. They were convicted of those counts on the mere statements". Yaani wakihukumiwa bila ushahidi.. Kwanini mnawaonea watu hivi?

Ni dhuluma. Dhuluma dhidi ya haki na uhuru. Kwa utaratibu ni afadhali umuachie huru mtu kwa kukosa ushahidi kuliko kumtia hatiani mtu kwa kukosa ushahidi. Hakimu Thomas Simba aliwaonea akina Freeman. Wangapi wameonewa namna hii? Mahakama siyo chombo cha kutesa RAIA. hamuelewi?

Thomas Simba, wakati huo anafanya maamuzi hayo ya kidhalimu dhidi ya viongozi na wanachama hao wa Chadema, ndiye alikuwa Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama ya Kisutu. Tulitegemea awe jicho la mahakimu wengine wa chini yake, badala yske amewaonea watu wasiokuwa na hatia. Why?"

Martin M.M
 
Tupia nakala ya hukumu kamili ya Jaji Mgeta kama unayo au linki, tuone jinsi nchi ilivyokuwa imeharibiwa ndani ya utawala wa awamu ya tano.

Jukwaa letu ni sehemu nzuri ya kutunza hukumu kama hii ioneshayo jinsi mzizi wa udikteta unavyoweza kujikita ktk mihimili mingine na kupelekea kukosekana haki .
Chini ya awamu ya tano ya utawala wa Mwendazake (revered) hayati (late) Mh. John Pombe Joseph Magufuli , Criminal Justice System nchini Tanzania ilikuwa imepigwa kabali shingoni na kuwekewa mtutu wa bunduki itekeleza majukumu yake kwa mbinyo bila kuzingatia sheria au Katiba bali Hofu kali, kwa kifupi mhimili wa Mahakama ulikuwa sawia na mateka.
25 June 2021
Dar es Salaam, Tanzania

Wakili msomi Peter Kibatala afunguka kuhusu maamuzi ya Mahakama Kuu kutengua hukumu yote ya Mahakama ya Hakimu Mkazi



Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua hukumu ya kesi ya uchochezi dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake na kuamuru warejeshewe kiasi cha Sh.Mil 350 walicholipa kama faini.Anaripoti Mika Ndaba.
Source : Millard Ayo
 
Enzi hizo Mipolisi yetu ilikuwa kazi yao ni kuwavizia tu Viongozi na Wafuasi wa Chadema ili wawashtaki kwa kesi za kilichoitwa "UCHOCHEZI"

Lengo la hayo yote lilikuwa ni kumfurahisha tu mpenda sifa na utukufu wa wakati huo! Hakika tulipitia kipindi kigumu sana kama Taifa. Apumzike tu kwa amani huko aliko.
 
Enzi hizo Mipolisi yetu ilikuwa kazi yao ni kuwavizia tu Viongozi na Wafuasi wa Chadema ili wawashtaki kwa kesi za kilichoitwa "UCHOCHEZI"

Lengo la hayo yote lilikuwa ni kumfurahisha tu mpenda sifa na utukufu wa wakati huo! Hakika tulipitia kipindi kigumu sana kama Taifa. Apumzike tu kwa amani huko aliko.
Ateseke tu huko aliko.Kutesa kwa zamu!
 
Hao wanao rekebisha hukumu sasa hivi wametoka mbinguni?

Huu ni unafiki. Ni system ile ile.
 
"Mere" - ushahidi mdogo au usio na uzito, ni kama majaji waliwahukumu kina Mbowe kwa kulazimisha au kuwatafutia kosa ili wamfurahishe aliewateua/bosi wao.
 
Nchi ilifikishwa pabaya na utawala wa Bwana yuleeee.Mihimili ya Bunge na Mahakama ililegea na kuiacha Serekali kuifanya utakavyo.
 
... vyombo vya serikali; ofisi ya DPP, DCI, Polisi, mawakili wa serikali, hakimu aliyehusika, CCM, n.k. wakijua kabisa ni mashtaka ya uongo wali-colude ili kuumiza watu ili fulani afurahi na kukenua meno! Hii ni aibu! CCM si bado ni ile ile? DPP, DCI, Polisi, n.k. si ofisi zao bado ni zile zile itashangaza wasipokata rufaa dhidi ya hukumu hii.

Wakikaa kimya itakuwa walifanya vile kwa nia ovu! Ila kama ilikuwa ni kwa sababu za msingi, walitakiwa hadi muda huu wawe wamekata rufaa kupinga hukumu hii wakakutane Supreme Court majaji mahiri waweze kufafanua vizuri na kuweke presendence iliyo bora zaidi.
 

Mahakama kuu yatengua hukumu kesi ya Mbowe na Wenzake​

0
BY JANETH FRANCIS ON JUNE 25, 2021HABARI
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetengua hukumu ya kesi ya uchochezi dhidi ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Freeman Mbowe na wenzake na kuamuru warejeshewe kiasi cha sh. Milioni 350 walicholipa kama faini.

Akisoma uamuzi huo, Jaji Irvin Mgeta amesema ameangalia na kuzingatia kuwa hukumu iliyotolewa ilikuwa na mapungufu ya uchambuzi wa ushahidi na kwamba washtakiwa hawakuwa na kosa na hivyo anawaachia huru.

Akifafanua kosa la 2,3,4 ambayo ni ya kufanya mkusanyiko isivyo halali, kuandamana bila kibali na kukiuka amri ya polisi ya kuwataka kuacha kuandamana, Jaji Mgeta amesema, katika uchambuzi wake ameona eneo la Buibui Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Ambalo washtakiwa walidaiwa kutenda kosa, lilikuwa eneo halali kwa mkutano wa kampeni hakuna ushahidi unaonyesha nini kilitendeka pale isipokuwa wengi wa mashahidi walikuwa wakizugumzia barabara ya Kawawa jijini Dar es Salaam.

Ushahidi uliowasilishwa mahakamani ni pamoja na mkanda wa video, lakini katika video ile ilionyesha watu wa alikuwa wakiandamana kwa amani huku wakiwa wamenyoosha mikono juu lakini jeshi la polisi ndio lilianzisha vurugu baada ya kuanza kulipuwa mabomu ya machozi ili kutawanya watu.

Akifanua juu ya mashtaka ya uchochezi, Jaji Mgeta amesema, mashtaka hayo yalikuwa na mapungufu, hati ya mashtaka pia ilikuwa na mapungufu kwa sababu haikuanisha ni Makundi gani yaliyochochewa na kuathirika.

“Wakati wa uchaguzi wanasiasa hutumia maneno mbali mbali kwenye majukwaa ili kunadi sera zao…, kesi ambayo Hakimu wa Mahakama ya Kisutu (Thomas Simba) aliitumia ya Hussein Kasanga dhidi ya Jamuhuri ilitolewa mwaka 1974 wakati wa chama kimoja”, amesema Mgeta.

Amesema katika kesi hii ya Mbowe na wenzake huwezi kusema walifanya chuki dhidi ya nani lakini katika kesi hiyo inaonyesha Kasanga alisambaza chuki dhidi ya Nyerere ma Chama cha TANU lakini kesi ya Mbowe na wenzake pia imetenguliwa wakati wa mfumo wa vyama vingi hivyo lazima kuwe na lugha za kuhamasisha wananchi juu ya chama husika.

“Nimeona mashtaka yote dhidi ya washtakiwa yalikuwa hayajathibitishwa hivyo nawaachia huru. Aidha Jaji Mgeta amesema licha ya kwamba Vincent Mashinji alikuwa hajakata rufaa na wenzake lakini moja kwa moja nae anafaidika na rufaa hii hivyo nae arejeshewe fedha zake.

Kesi Hiyo ya 2018 Mbowe na wenzake walikuwa na mashtaka matatu likiwemo la uchochezi na kuandamana bila kibali.

Aprili 7, mwaka jana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilimuhukumu Mbowe na wenzake kulipa faini ya Sh.Milioni 350 ama kwenda jela miezi mitano kila mmoja baada ya kutiwa hatiani kwenye makosa 12 ikiwemo la kufanya mkusanyiko wenye ghasia.

Hukumu hiyo iliyochukua takribani saa nne, kuanzia saa 7:20 mchana hadi saa 11:20 jioni, ilitolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi nane wa upande wa mashitaka na mashahidi 15 wa utetezi.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mbunge wa Iringa mjini, Peter Msigwa, Naibu Katibu Mkuu Taifa, Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Kibamba, John Mnyika.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Dk. Vicent Mashinji ambaye alikuwa Katibu Mkuu taifà wa chama cha Chadema na Ester Matiko mbunge wa Bunda mjini.

Katika hukumu hiyo, Hakimu Simba alisema amewatia hatiani washitakiwa wote katika mashitaka 12 kati ya 13 yaliyokuwa yakiwakabili mahakamani hapo.

Kosa ambalo washitakiwa hao hawajatiwa nalo hatiani ni kosa la kwanza ambalo ni la kula njama kutenda makosa.
Katika adhabu hiyo, Mbowe alihukumiwa kulipa faini ya jumla ya Sh.Milioni 70 baada ya kutiwa hatiani katika mashitaka nane yaliyokuwa yakimkabili, Mdee Sh.Milioni 40, Dk.Mashinji Sh.Milioni 30, Heche Sh.Miliono 40, Msigwa Sh.Milioni 40, Bulaya Sh.Milioni 40, Mnyika Sh.Milioni 30, Mwalimu Sh.Milioni 30 na Matiko Sh.Milioni 30.

Hata hivyo viongozi hao walipelekwa gerezani kutokana na kushindwa kulipa faini hizo kwa siku ya jana.

Baada ya hukumu hiyo, Wakili wa Utetezi Peter Kibatala alisema kuwa watakata rufaa dhidi ya hukumu hiyo ila kwa sasa watalipa faini ili washitakiwa hao kuachiwa huru.

“Tutakata rufaa dhidi ya kesi hii ila kwa sasa hivi ngoja tulipe faini ili watu wetu watoke nje wawe huru,” alisema Kibatala

Mashtaka yaliyokuwa yakiwakabili
Mwaka 2018, viongozi hao walifikishwa mahakamani hapo wakikabiliwa na mashitaka 13 ikiwemo ya kufanya mkusanyiko usiohalali uliosababisha kifo cha mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji cha Taifa (NIT), Akwilina Akwiline.

Ilidaiwa kuwa washitakiwa kwa pamoja walitenda makosa hayo Februari 16, mwaka huu maeneo ya Viwanja vya Buibui pamoja na barabara ya Kawawa Mkwajuni wilayani Kinondoni, Dar es Salaam.

Katika shitaka la kwanza la kula njama, kwa pamoja inadaiwa Februari Mosi na 16, 2018, Dar es Salaam walikula njama pamoja na wenzao ambao hawapo mahakamani walikula njama ya kutenda kosa la kufanya mkusanyiko usio halali, mkusanyiko wenye ghasia na kukiuka tamko kutawanyika.

Ilidaiwa kuwa Februari 16,2018 katika ya viwanja vya buibui na Mwananyamala Kinondoni washtakiwa hao wakiwa wamekusanyika na adhma ya pamoja, waliitekeleza kwa kufanya mkusanyiko usio halali na kusababisha watu waogope kuwa watakwenda kupelekea vunjïfu wa amani.

Katika shitaka la tatu, washitakiwa hao wanadaiwa kuwa Februari 16, 2018 walifanya mkusanyiko wenye ghasia.

Ilidaiwa kuwa siku hiyo katika viwanja vya Buibui Mwananyamala na barabara ya Kawawa Kinondoni kwa pamoja na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walitekeleza mkusanyiko ama maandamano yasiyo halali wakiwa na lengo la kuvamia ofisi ya mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni na kuĺeta hofu ya uvunjifu wa amani.

Ilidaiwa kuwa Februari 16,2018 katika barabara ya Kawawa Kinondoni Mkwajuni washitakiwa hao wakiwa na wenzao 12 ambao hawapo mahakamani walikiuka tamko la kuwataka kutawanyika la Ofisa wa Polisi SSP, Gerald Ngiichi kwa kugoma kutawanyika na kupelekea uvunjifu wa amani ambao ulisababisha hofu na hatimaye kifo cha Akwilina na majeruhi kwa askari wawili ambao ni H.7856 PC Fikiri na E.6976 CPL Rahim Msangi.

Katika shitaka la tano, linamkabili Mbowe ambalo ni la kuhamasisha chuki, inadaiwa kuwa Februari 16, 2018 katika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni, Dar es Salaam, Mbowe wakati akihutubia wananchi wa jimbo hilo alihamasisha chuki isivyohalali kwa kutoa matamshi yafuatayo
“Ninapozungumza hapa kiongozi wetu wa kata ya kinondoni Hananasif jijini Dar es Salaam yupo mochwari..amekamatwa na makada wa ccm kwa msaada wa vyombo vya ulinzi na usalama…wamemnyonga wamemuua. Halafu sisi tunaona ni jambo la kwawaida…tunacheka na polisi…tunacheka na ccm”

Katika shitaka la sita, Mbowe anadaiwa kuwa Februari 16, 2018 katika mkutano wa umma uliofanyika viwanja vya Buibui wilayani Kinondoni Dar es Salaam, Mbowe alitamka maneno yafuatayo ” Tumejipa kibali cha kutangulia mbele ya haki…haiwezekani wanaume wazima na akili zetu na wake zetu na watoto wetu tukafanywa ndondocha….
….hiii ni nchi ya ajabu. Mimi leo nipo hapa kulinda taifa…kule Afrika kusini Jacob Zuma amelazimishwa kujiuzulu…Robart Mugabe wa Zimbabwe kangolewa, kangolewa Waziri mkuu wa Ethiopia…juzi ameondoka kwa people’s power. Magufuli ni mwepesi kama karatasi”Nchimbi alidai kuwa maneno hayo yalikuwa ya kuinua hali ya kutoridhika miongoni mwa watanzania dhidi ya serikali halali iliyopo

Mdee anadaiwa kuwa Februari 16,2018 akiwahutubia wakazi wa kindoni alitamka kuwa ” sîhitaji kuwasïmuĺia madhila yanayomkumba kila mmoja wetu kutokana na utawala wa awamu ya tano…tunamba kesho tukamchinje Magufuli na vibaraka wake wote…kama mbwai na iwe mbwai
 
Hao wanao rekebisha hukumu sasa hivi wametoka mbinguni?

Huu ni unafiki. Ni system ile ile.
Kama wameamua kubadilika basi tuwapongeze. Maana hata wangeamua kuwa vile vile au hata ubaya zaidi tulikuwa hatuna nguvu ya kuwazuia
 
Back
Top Bottom