Uchaguzi 2020 Jaji Kaijage ana nafasi nzuri ya kutengeneza historia na hata kupendekezwa kugombea Tuzo ya Amani ya Nobel

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,796
Macho yote yako tume ya uchaguzi chini ya jaji Kaijage mziki huu school mate wangu kihamia asingeuweza kamwe. So far tume inafanya vema. Si vibaya kwa hatua hii kutoa pongezi za awali.

Kuna mambo yanatokea kwa kasi ya ajabu na kwa haraka mno mpaka kuna vitu vinatupita. Ni ukweli usiopingika CCM HAKUKO SHWARI Kuna kila dalili mgombea kasusiwa ama kaachwa yatima wale manguli wa kuisimamia ccm hasa nyakati hizi hawaonekani popote wakikipigania na kukipamba chama.

Kasi ya mgombea wa CHADEMA inaleta taharuki mpya kila hatua anayopiga..na ni taharuki ya hoja zilizojaa sheria...ni wazi kabisa CCM haikujiandaa kabisa na hili waligeuza mazoea yakawa sheria

CCM kumepooza! Huo ndio ukweli mchungu na hata makada wake mitandaoni ni kama wamegeuka majuha na kichekesho kwa hoja zao zilizokosa weledi na mashiko

Jaji Kaijage karahisishiwa kazi nyingi na mgombea wa Chadema ambaye kitaaluma ni mwanasheria nguli...Hivyo basi jaji Kaijage akizisimamia sheria za tume ya uchaguzi kwa weledi (hitaji kubwa la CHADEMA) Bila kujali matokeo yatakuwaje atajitengenezea jina na historia tukuka

Akifanikiwa hilo namuona wazi akitutoa kimasomaso kwenye tuzo za amani za dunia
 
Tuzo ya Amani ya Nobel?
Mzee unaijua hii tuzo vizuri?
Inatolewa kwa mtu aliyesuluhisha Vita au machafuko yaliyokuwepo muda mrefu

Mfano yule Waziri Mkuu wa Ethiopia kwa kumaliza yale machafuko ya wa Oromo kipindi kile
 
Maneno haya tuliyasikia tangu 2015 JPM alipochaguliwa mara ya kwanza. Mmekuwa wazuri sana wa kuhamisha magoli ya kwamba JPM , CCM na Serikali wamefeli. Hizi ni ndoto za alinacha. Ndio kauli kama, washamba wamepewa nchi, nk zikatamalaki. 2020 bado hamjalipata somo tu?
 
Mshana, una maanisha ' Nobel peace prize' ? Kweli? Kwa kipi hasa. Sema unatania ili heshima ulojijegea humu iendelee kutamalaki
 
Hujui unachoongea.....unamjua Mandela na de clak?na Dalai lama je? Kwa uchache hawa
Sio lazima . Wengi sana wameshinda bila hayo uliyoyasema
Yule mama Mkenya aliyehamasisha upandaji miti

Wangarĩ Muta Maathai was a renowned Kenyan social, environmental and political activist and the first African woman to win the Nobel Prize
 
Tuzo ya Amani ya Nobel?
Mzee unaijua hii tuzo vizuri?
Inatolewa kwa mtu aliyesuluhisha Vita au machafuko yaliyokuwepo muda mrefu
Mfano yule Waziri Mkuu wa Ethiopia kwa kumaliza yale machafuko ya waOromo kipindi kile

Kwani wewe kuiondo ccm Madarakani huoni ni kuleta amani?
Au amani gani unasemea zaidi ya hii ya kutolewa utumwani?!!!!
 
Back
Top Bottom