Wewe unasema wapiga kura walizidi huko Pemba.Na hili la Maalim Sefu kujipa nafasi ya ZEC na kujitangaza mshindi nalo mnalisemeaje. na ile idadi ya wapiga kura iliyozidi kule Pemba watu wakae kimya, hizo siyo dosari zisisemwe? unafki huo. uchaguzi urudiwe tu. CUF wajiamini. kama ushindi ni wao wataupata tu.
Huyo Bomani ambaye aliwahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali, kwa kuyatamka hayo ameishusha taaluma yake ya uanasheria kwa kiwango cha hali ya juu sana.Kama kweli jaji ameongea haya basi akapimwe akili!!!
Na hili la Maalim Sefu kujipa nafasi ya ZEC na kujitangaza mshindi nalo mnalisemeaje. na ile idadi ya wapiga kura iliyozidi kule Pemba watu wakae kimya, hizo siyo dosari zisisemwe? unafki huo. uchaguzi urudiwe tu. CUF wajiamini. kama ushindi ni wao wataupata tu.
Wewe unasema wapiga kura walizidi huko Pemba.
Sasa nikuulize swali moja tu jepesi, hivi si kila kituo kulikuwa na mawakala wa vyama vyote?
Sasa kama mawakala hao, pamoja na wa vyama vya CCM na CUF waliweka saini ya fomu za matokeo, ikiwa na maana walikuwa wamejiridhisha kuwa uchaguzi haukuwa na kasoro zozote.
Sasa huyo Jecha kukurupuka na kutangaza kuyafuta matokeo hayo tena bila kushirikisha makamishna wenzake wa ZEC, hivi huo bado
haujawa ushahidi wa kutosha wa mazingira kuwa Jecha 'aliamriwa' na CCM kutoa tamko hilo baada ya kugundua ya kuwa mgombea wao Dr Shein amebwagwa na Maalim Seif?
Kwa hali inayoendelea nchini mwetu ya CCM kutaka kung'ang'ania madarakani hata kwenye yale maeneo wanayojua dhahiri wameshindwa, kutakuja kuiletea maafa nchi hii.
Mfano halisi ni uchaguzi huo wa Zanzibar na hivi sasa umehamia kwenye uchaguzi wa mameya huku Bara.
Tumeshuhudia huko Tanga jana namna uchaguzi wa meya wa huko, namna msimamizi wa uchaguxi alivyoamua kumtangaza mgombea wa CCM ambaye alishindwa kuwa ndiye mshindi na mgombea wa CUF ambaye ndiye aliyeshinda akatangazwa kushindwa!
Hata hivyo kama lilivyotokea kwa Jecha baada ya kuyafuta matokeo ya Zanzibar 'akapelekwa' mafichoni, vivyo hivyo kwa msimamizi wa uchaguzi wa jijini Tanga, naye amepelekwa mafichoni mara tu baada ya kutangaza kuwa mgombea wa CCM kuwa ndiye aliyeshinda uchaguzi.
Hivi kama kweli msimamizi huyo angekuwa ametangaza kitu ambacho yeye aliamini ndicho sahihi, ni kitu gani kilichomtoa nduki baada ya kuyatangaza matokeo hayo??!!!!
Pokea like zangu 100 kwa mpigo.CCM mna unafiki wa hali ya juu.
Uchaguzi ulishafanyika na ulikwisha.
Matokeo yote yalishatangazwa majimboni. Matokeo ya wawakilishi yaliishia kwa walioshinda uwakilishi kupewa vyeti wa ushindi. Matokeo ya kura za uraisi pia yalibandikwa majimboni. Ni matokeo hayo yanayompa mgombea wa CUF ushindi na ni matokeo hayo yanayoonesha mgombea wa nafasi ya uraisi kupitia CCM ameangukia pua.
CCM imeamua kubaka demokrasia na kumwamuru Mwenyekiti wa Tume "huru", ZEC afute uchaguzi na matokeo yake bila ya kuwepo na malalamiko yaliyowasilishwa na mawakala wa vyama.
Kurudia uchaguzi ni uhuni wa CCM wa kutaka kufunga goli la Nape. Kama CCM ilishinda uchaguzi ule Jecha angekuwa na ubavu wa kufuta uchaguzi au matokeo?
CCM mnaiharibu nchi hii, CCM mnaichezea amani ya nchi. CCM iheshimu maamuzi ya wapiga kura.
Siri iko nje, tokea 1995 CCM haijawahi kushinda uchaguzi mkuu huko Zanzibar lakini Mwanyekiti wa ZEC amekuwa akilazimishwa kumtangaza mgombea wa CCM ameshinda.
Mimi nashangaa kwa nini Msajili wa vyama hajakifuta CCM kwa uhuni huu wanaoufanya kwa miongo miwili sasa. Hapo ndio utafahamu maana ya Chama dola.
Imeripotiwa Makamo Mwenyekiti alitekwa nyara na vyombo vya dola ili asiendelee kutangaza matokeo ya uchaguzi. Kwa nini alichukuliwa na vyombo vya dola? Nani aliamrisha uhuni huo? Huyo aliyeamrisha ndie alivuruga uchaguzi.
Ni wazi hilo lilifanyika ili kuminya na kuzuia haki isitendeke na ni ubakaji wa demokrasia.
Kwa vyovyote wote, waliohakikisha wanazuia matokeo yasiendelee kutangazwa wamefanya hivyo kwa malengo ya kukibeba CCM na hiyo ndio "siri" ya ukasuku wa "uchaguzi urudiwe".
CCM na wanachama wa CCM wamejigeuza makasuku na kauli mbiu ni "uchuguzi urudiwe".
Kwa nini CCM haitaki yale matokeo yaliyotangazwa na yaliyobandikwa vituoni, majimboni baada ya kuhesabiwa kura yasitangazwe na mwenyekiti wa ZEC?
CCM inabaka demokrasia na kutishia amani ya nchi yetu.
Huu ni mtihani kwa Magufuli . Magufuli atabakia kuwa msema kweli na kuukana unafiki wa CCM? Nimkumbushe tu , Raisi Pombe wa Magufuli alisema "mimi nauchukia unafiki, mimi ni msema kweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu"
Raisi Magufuli ajiulize;je aliye mnafiki na anayepindisha ukweli na anayebariki au kufumbia macho dhuluma kutendeka ni mpenzi wa nani?
Hawataki muungano kisa uislamu wao waachwe tu.
Duuuh huyu bomani hora angekaa kimya tu kuliko kujidhalilisha huku
Tatizo la watu wa kina Bomani ni kutanguliza UKEREKETWA NA UKADA na si TAALUMA NA UKWELI, huu ni ugonjwa kwa wataalamu wetu na hata washauri wa viongozi wetu wakubwa. Kwa hali hii watu wasimshangae jaji Bomani bali ekemewe .
Duuuh huyu bomani hora angekaa kimya tu kuliko kujidhalilisha huku