Mkeshahoi, nimekisikiliza kipindi, huna haja kuwa bored, mjadala ulikuwa mzuri na umeshiba hoja.
Kwa kuanzia, nampongeza sana Kibonde, kusema ukweli amebadilika sana katika kipindi kifupi. Sasa anaonekana a really mature person na sio zile enzi za yale maroroso yake akiweka jokes karibu kwenye kila issue.
Mjadala ulihusu makampuni makubwa na haswa ya kigeni, kuwaajiri zaidi wageni kisa wana jua zaidi kuzungumza kiingereza ili hali wengine hata kazi hawawezi na wanafanyiwa na watz waliochini yao.
Hoja ya Kibonde ni uwezo wa kazi na sio lugha, akasema Watanzania wana uwezo mkubwa, tatizo ni kutojiamini tuu kwenye lugha ya Kiingereza, na akashikilia kwani Kiingereza lazima?.
Hoja ya Kayanda, waajiri wanataka watu wenye uwezo kuwasiliana kwa lugha ya kimataifa, Kiingereza, kwa vile WaTZ hawajiamini, amewakubali waKenya wanauwezo.
Kipindi hiki ni Kibonde ameshuka nondo mpaka akakasirika, amesisitiza jiamini una uwezo wa kufanya mambo, fanya mambo, jithaminishe thamani yako, jiaminishe value yako, panga bei ya huduma yako watalipia kwa thamani yako, akasisitiza tusijishushe.