Jafo: Viongozi acheni tabia ya kuinua mabega, jeuri na kiburi kwani sisi wote tutaonja mauti!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
85,191
144,238
Waziri wa Tamisemi mh Selemani Jaffo amewasihi viongozi wenzake kuacha tabia ya kuinua mabega kujitutumua, jeuri na kiburi kwani kila nafsi itaonja umauti.

Waziri Jaffo amesema hayo wakati wa mazishi ya mkuu wa mkoa mstaafu wa mkoa wa Kigoma hayati meja jenerali Maganga huko Mvomero mkoani Morogoro.

Jaffo alikuwa akielezea wasifu wa RC Maganga kwamba alikuwa ni mtu mnyenyekevu, asiye na majivuno na mwenye kuheshimu watu wengine bila kujali hadhi zao.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!
 
Jafo mwambie Jiwe kule Chato arudi Dom aache kujitutumua na kuiacha ikulu ya Dodoma wakati Watanzania tumeijenga kwa mamilioni ya shilingi
 
Waziri wa Tamisemi mh Selemani Jaffo amewasihi viongozi wenzake kuacha tabia ya kuinua mabega kujitutumua, jeuri na kiburi kwani kila nafsi itaonja umauti.
Ujumbe huu unqmfaa sana bosi wake a.k.a chato boy.

Ana kiburi jiwe huyu utadhani yeye ndiye kamuumba Mungu.
 
Huu ujumbe umfikie Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Dodoma , yaani kazidi na ni mnyanyasaji mkubwa si kwa watumishi pekee wanafuzi na hata wazazi wakienda kwa ajili ya jambo lolote la kikazi na kwa kweli huyu amulikwe na kushughulikiwa pia.
 
Naibu waziri David Silinde amekusikia!
 
Ni kweli Jaffo lakini kama Waziri mwenye dhamana ya uchaguzi wa serikali za mitaa uliuvuga.HII NI KIBRI!!
Jaffo,vijini watu wanchangishwa michango ya kujenga shule kwa serikali kuingiza wanfunzi wengi Sekondari lakini Ubungo shule inajengwa kwa gharama za serikali,au wazazi walichangishwa???
 
Wameinua muda mrefu sana sasa kama watu na familia zao wanacharazwa bakora hadharani unategemea nini?
 
Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…