logania
JF-Expert Member
- May 19, 2016
- 464
- 313
SIYO Jeep la Mmarekani wala Korando la Mkorea. Hili ni gariaina ya Kaparata ambalo limebuniwa na kutengenezwa na kijana Mtanzania, JacobLouis ‘Kaparata’ (38), mkazi wa Gongo la Mboto jijini Dar es Salaam ambayeametumia vifaa vingi vinavyopatikana hapa hapa nchini.
Waliobahatika kuliona gari hili katika Maonyesho ya Biasharaya Kimataifa – Saba Saba wamekiri kwamba huu ni ubunifu mkubwa ambao unastahilikuungwa mkono na serikali na mamlaka nyingine.
“Nimetumia vifaa vingi vinavyopatikana hapa nchini. Chassisnimeitengeneza kwa kutumia square pipe, bodi nimelisuka kwa kutumia brake pipeszinazotumika kutengenezea vitanda na nikatumia mabati ya gauge 18 ambayoyanatumika kutengenezea mageti,” anafafanua Kaparata.
Anaongeza: “Nilipomaliza kutengeneza chassis nikaenda kununuainjini, diff, gear box na matairi, ambavyo vyote ni vya gari aina ya SuzukiCarry. Unajua Suzuki Carry ni fupi ina futi 10, lakini nilichokifanya ni kuongezachassis hadi futi 12. Injini ina nguvu sana ila kigari kile kimenyimwa bodi.Sasa gari yangu hii imeonekana kuwa na nguvu, ina kasi.”
Kaparata anasema kwamba, gari yake ina muundo wa kipekeetofauti na gari lolote duniani na ameitengeneza kwa kipindi cha miezi mitatu tukabla ya maonyesho ya mwaka huu ya Saba Saba ambapo limemgharimu kiasi cha Shs.12,850,000.
“Nilipokuwa mdogo nilikuwa mtundu sana nikitengeneza magari navitu mbalimbali kwa kuiga nilivyoviona, ndipo watoto wenzangu wakanipachikajina la ‘Kaparata’, ambalo nimelizowea na kuamua kuiita kampuni yangu kwa jinahilo.
“Tangu mdogo nilipenda kuangalia filamu na nilivutiwa na garimoja nililoliona kwenye filamu ya Delta Force ya Chuck Norris (The Flyer 72Advanced Light Strike Vehicle) nikaapa kwamba lazima nije nitengeneze gari laaina hiyo,” anasema Kaparata.
Hata hivyo, anasema kwamba, alitumia muda wa wiki mbilikutengeneza chassis ambayo alihakikisha inanyooka na kukaa sawa kabla yakuendelea na utundu mwingine.
“Hivi sasa nikitembea na gari yangu, hata kama tumeongozana namagari mengine ya kifahari, watu wataitazama gari yangu mitaani na wamevutiwanayo huku wengine wakinitaka nitengeneze mengine niyauze,” anasema.
Anasema wakati anaanza kuitengeneza gari hiyo vifaa pekeealivyokuwa navyo ni drill machine, grander na welding machine – vifaa vitatutu, ambapo mabati na vifaa vingine alivinunua.
Kwa kuwa yeye si fundi mchundo, mabati na vifaa vinginealiyapeleka kwa mafundi mchundo ambao walimkunjia kwa muundo na vipimoalivyovitaka yeye.
“Lakini nimeingia hasara kubwa kwa sababu wakati mwingineunampelekea mtu akukunjie bomba au bati, lakini anakosea, inabidi kulitupa nakutafuta jingine.
“Nilipokuwa nayabeba mabati kupeleka kwenye viwanda kwa ajiliya kukunja wengi waliniona kama mwendawazimu, wengine wakanikatisha tamaa nakusema magari wanatengeneza Wazungu miye Mswahili maskini wapi na wapi!”anasema.
Hata hivyo, anamshukuru mkewe Elizabeth William aliyemzaliawatoto Beatrice (14), William (10) na Neema (2) ambaye alikuwa akimtia moyokila wakati aendelee na ubunifu wake.
“Unajua hata kule kwenye viwanda nilikokuwa napelekahawakuamini, kwa sababu nilipoyabeba mabati wengine walidhani nakwendakutengeneza ndoo, lakini baada ya mabati hayo kukunjwa kama nilivyotaka, wotewalishangaa,” anasema.
Ukilitazama gari hilo kwa mbali unaweza kudhani ni aina mpyaya Jeep ingawa muundo ni tofauti kabisa, na kama utalikaribia utashangaa kuonavikorombwezo vingi.
“Hiki kioo cha mbele ni cha Land Cruiser ila nimekata mashavuya pembeni. Indicator ni za Bajaj aina ya TVS, shoo ni za vifaa mbalimbali vyamagari. Nimeweka vent kama za Ranger za kuingizia hewa kwenye air cleaner namengine kibao,” anasema.
Kaparata anasema kwamba, ubunifu ni gharama kubwa, lakinimahali alipofikia kwa sasa anajiona kama ni mhandisi aliyebobea ingawa kikwazoni mtaji pamoja na kutambulika na mamlaka zinazohusika.
“Mheshimiwa Rais Magufuli amesema anataka kuona Tanzania yenyeviwanda ambayo ndiyo nia pekee ya kutengeneza aira kwa sisi vijana, sasa miminimeamua kuanza bila kupata msaada wa mtu yeyote mpaka nimekamilisha,ninachokihitaji kwa sasa kwanza ni kutambuliwa na serikali kwa ubunifu wangu,halafu niweze kupatiwa mtaji na mazingira bora zaidi ya kufanyia kazi.
“Kama leo nitaamua kutengeneza gari nyingine kama hii,ninaamini ndani ya mwezi mmoja nitakuwa nimeitengeneza na itakuwa bora kulikohii kwa sababu nimejifunza makossa yote wakati nahangaika na hii hapa,”anaongeza.
Gari la kifahari la Kaparata limeacha gumzo kwa wageniwanaoshiriki na wanaotembelea maonyesho ya biashara ya kimataifa – Saba Saba,hususan Banda la SIDO.
“Kwani linauzwa kiasi gani? Hili linafaa sana kwenda naloshamba,” alisema mwananchi mmoja. Mwingine akasema: “Hili ni zuri kama gariaina ya Jeep, la kutokea na familia kwenda kupunga upepo.”
Naam. Walikuwa ni wananchi waliotembelea Banda la SIDOalikoliegesha gari hilo kwa maonyesho pamoja na bidhaa zake nyingine, kwa kuwayeye ni miongoni mwa vijana wanaonufaika na fursa za Shirika hilo la ViwandaVidogo ambalo linawakusanya wajasiriamali na wabunifu pamoja ili kuonyesha kazizao.
Yeye anafanyia shughuli zake katika eneo la SIDO Vingunguti nahata gari hilo ndiko lilikotengenezewa.
“Sikubahatika kusoma hata darasa moja kutokana na matatizo yakifamilia, huu ni utundu wangu ambao nimekuwa nao tangu nikiwa mdogo. Nilianzakutengeneza magari ya kuchezea kwa kutumia mabati, lakini daima ndoto zanguzilikuwa kutengeneza gari langu mwenyewe, nashukuru Mungu ndoto hizozimetimia,” anasema Jacob ambaye alizaliwa Mpanda mkoani Katavi kabla yakuhamia Kigoma ambako baba yake Mzee Louis Jacob alikuwa dereva katika Mamlakaya Pamba.
Akiwa mtoto wa saba kati ya watoto nane, Jacob anasema kwambani wawili tu kati yao waliowahi kuingia katika vyumba vya madarasa ambao nidada yake wa pili kuzaliwa ambaye aliishia darasa la nne na kaka yake wa tatukuzaliwa aliyemaliza darasa la saba.
Anasema, baada ya wazazi wao kutengana mwaka 1993, mama yaoaliamua kuwachukua yeye na ndugu zake na kurudi Mpanda ambako maishayaliendelea kuwa magumu mno.
“Elimu ya zamani, hasa ya darasa la sababu, haikuwezakumfikisha popote hata yule kaka yangu, kwa hiyo tulijikita katika shughuli zashamba tu,” anaeleza.
Hata hivyo, anasema kwamba licha ya kutoingia darasani, hivisasa anajua kusoma baada ya kufundishwa kusoma a, e, i, o, u na mpwawe SarahWilliam mwaka 1993 na yeye akaziunganisha herufi hizo.
Kaparata anasema kwamba, mpaka anakamilisha kutengeneza garilake hakuchukua hata senti tano ya mtu bali ni fedha zake mwenyewe kutokakatika vyanzo vingine.
Anasema kwamba, wengi walimcheka na kusema kama anazo fedha zakuchezea bora akawape maskini kwa vile asingeweza kufanikiwa kutengeneza gari,lakini kwa kuwa alikuwa na ndoto zake akaamua kuyapuuza maneno yao na kukwanguakila akiba aliyokuwa nayo kutimiza hayo malengo.
“Mimi ninafanyia kazi zangu pale SIDO Vingunguti, zaidinatengeneza mashine za kutotolesha vifaranga ambazo kidogo kidogo ndizozinazoniingizia fedha, hivyo hata fedha za kutengenezea gari hili zimetokana nakazi hizo,” anasema.
Anaongeza kwamba, licha ya kutokusoma, lakini utundu naubunifu wake vinamwezesha kuendesha maisha yake na amekuwa tegemeo kubwa kwandugu zake wote.
Amewaasa vijana wengine waliosoma na hawana ajira pamoja nawale ambao hawakubahatika kupata elimu kutokukata tamaa, bali wanaweza kutumiavipaji na nguvu walizojaaliwa na Mwenyezi Mungu kufanya maendeleo.