Uchaguzi 2020 Jackson Kangoye agoma kumuunga Michael Kembaki Tarime, ashangaa undumilakuwili na uongo wa Bashiru na Polepole

Status
Not open for further replies.

Musachawenyu

Member
Aug 6, 2020
18
16
Maumivu ya uteuzi wa wagombea ubunge ndani ya CCM bado unaendelea. Japo wengi hawasemi wazi lakini chini kwa chini kuna mgogoro mkubwa.

Katika Jimbo la Tarime mjini, aliyeongoza kura za maoni ni Jackson Kangoye na aliyemfuatia ni Michael Kembaki ambaye ndio aliyeteuliwa kuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo.

Maamuzi hayo hayajapokelewa vyema na Jackson kwani anaamini kama tatizo ni utoaji wa rushwa wote wawili walikuwa wanatoa rushwa, hivyo angeteuliwa mtu mwingine walau angeelewa kwani kilichofanyika hakielewi na hakina maana.

Kama viongozi wetu, kuanzia Rais Magufuli, Dr. Bashiru na Polepole wangekuwa wanasimamia kauli zao basi tungetamani kuona haki inatendeka na kukata wote waliotoa rushwa, kwanini iwe kwangu tu? Alisikika Jackson akiwaeleza watu wake wa karibu.

Hadi sasa Jackson hajapongeza uteuzi wa Bwana Kembaki na yuko radhi kumsaidia Esther Matiko kwa njia zote na kimya kimya.

Maamuzi hayo yameiumiza sana familia ya Kangoye kwa sababu baba yake Jackson, Mzee Ryoba Kangoye amegombea mara 4 bila mafanikio na mwaka 2015 alishindwa na John Heche, hivyo akaamini mwaka huu walau mwanae anaweza kushinda na kuifuta familia machozi.

Viongozi wetu kina Bashiru na Polepole ni waongo na hawapaswi kuaminika tena kwani ahadi zao za kukata wala rushwa wote zilikuwa za upotoshaji na zisizo na ukweli wowote. Alisema, Charles, aliyekuwa mpambe mkubwa wa Jackson Kangoye.

CCM Tarime mara nyingi inashindwa sababu ya migawanyiko Tarime, tunasubiri kuona kitakachotokea mwaka huu 2020 kuona kama yale ya 2015 yatajirudia tena.
 
Hatapata uteuzi kwenye nyazifa zingine, this is black mailing. Utadhani wote watateuliwa. Kwa wapenda madarkaa kauli ya Polepole itawafanya waugulie ndani kwa ndani na uteuzi hawata pata.
 
Hivi huku duniani kazi ni ubunge tu? Mbona watu wanahamanika sana?

Mbona Sisi walimu tu na maisha yanaenda. Jamani tuache ujinga tufanye kazi na wakati mwingine ona afadhari kwenda kumpigia mwenzako kura
 
Nafikiri shida kubwa ni uongozi mbovu wa viongozi wa CCM kwani walichohubiri na kutenda ni vitu viwili tofauti.
 
Hivi huku duniani kazi ni ubunge tu? Mbona watu wanahamanika sana?

Mbona Sisi walimu tu na maisha yanaenda. Jamani tuache ujinga tufanye kazi na wakati mwingine ona afadhari kwenda kumpigia mwenzako kura
Vipi mzee wa Toronto, Mwandli atamuunga mkono Dr. Moleli?
 
Sio kweli kwamba ccm wanashindwa Tarime kwa sababu ya mgawanyiko. Ukweli ni kwamba ccm watu wameichoka mno.

Vijana waliozaliwa miaka ya themanini kuja huku ndio body kubwa ya wapiga kura na toka wamezaliwa hadi sasa eti chama ni hicho hicho, yani wamekinaiwa sana tu na wanataka mabadiliko.
 
Isiwe taabu, NEC Dodoma imemwaga mboga. Sasa wapiga kura tumwage dona. Kama mbwai na iwe mbwai. Acha CCM ife
 
Familia ya Kangonye nimeihurumia sana...kimkakati CCM wangemrudisha wakili heche awapasue mchana kweupe ushindi ni mipango.
 
Maumivu ya uteuzi wa wagombea ubunge ndani ya CCM bado unaendelea. Japo wengi hawasemi wazi lakini chini kwa chini kuna mgogoro mkubwa.

Katika Jimbo la Tarime mjini, aliyeongoza kura za maoni ni Jackson Kangoye na aliyemfuatia ni Michael Kembaki ambaye ndio aliyeteuliwa kuwa mgombea ubunge katika jimbo hilo.

Maamuzi hayo hayajapokelewa vyema na Jackson kwani anaamini kama tatizo ni utoaji wa rushwa wote wawili walikuwa wanatoa rushwa, hivyo angeteuliwa mtu mwingine walau angeelewa kwani kilichofanyika hakielewi na hakina maana.

Kama viongozi wetu, kuanzia Rais Magufuli, Dr. Bashiru na Polepole wangekuwa wanasimamia kauli zao basi tungetamani kuona haki inatendeka na kukata wote waliotoa rushwa, kwanini iwe kwangu tu? Alisikika Jackson akiwaeleza watu wake wa karibu.

Hadi sasa Jackson hajapongeza uteuzi wa Bwana Kembaki na yuko radhi kumsaidia Esther Matiko kwa njia zote na kimya kimya.

Maamuzi hayo yameiumiza sana familia ya Kangoye kwa sababu baba yake Jackson, Mzee Ryoba Kangoye amegombea mara 4 bila mafanikio na mwaka 2015 alishindwa na John Heche, hivyo akaamini mwaka huu walau mwanae anaweza kushinda na kuifuta familia machozi.

Viongozi wetu kina Bashiru na Polepole ni waongo na hawapaswi kuaminika tena kwani ahadi zao za kukata wala rushwa wote zilikuwa za upotoshaji na zisizo na ukweli wowote. Alisema, Charles, aliyekuwa mpambe mkubwa wa Jackson Kangoye.

CCM Tarime mara nyingi inashindwa sababu ya migawanyiko Tarime, tunasubiri kuona kitakachotokea mwaka huu 2020 kuona kama yale ya 2015 yatajirudia tena.
Mchujo wa kamati kuu ya CCM umejaa mapungufu mengi ikiwemo mwenyekiti kutembea na majina ya wateule wake mifukoni, wengi wameonewa kisa polepole kapewa Rushwa na baadhi ya watia nia kura za maoni, ukiacha kikundi cha wachache rafiki wa mwenyekiti wa CCM wengine wasiojulikana vizuri ilibidi kumpelekea polepole takrima ndipo anawasaidia kupeta, CCM ni ile ile Ukoo ule ule kamati kuu siyo malaika siyo mungu wamejaa mapungufu mengi mno
 
Familia ya Kangonye nimeihurumia sana...kimkakati CCM wangemrudisha wakili heche awapasue mchana kweupe ushindi ni mipango.
Report za Takukuru ziliwalenga wale bahili wa kuwaona maafisa wa Takukuru na pia zipo report za kutengeneza kwa makusudi kuwakomoa wengine, kwenye kura za maoni ndipo kuna vioja visivyokwisha
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom