Wakoloni walipoamua kututawala si kuwa walipenda,bali kutokana na raslimali nyingi tulizokuwa nazo waafrika.watu hawa waliona hata kama watatumia nguvu kubwa, hakukuwa na hasara
Wapo waliwekeza kwenye migodi,wengine kwenye ardhi nzuri yenye rutuba.
Harakati za kudai uhuru toka 1922-1984, nchi nyingi,ziliomba kuwa huru,tonge nono liliwaponyoka,ni kwa kuwachonganisha waafrika wenzao wauane ili kumpachika mrithi wao.
Sehemu nyingi hadi wanaondoka wameacha makovu ya ukabila,rushwa na kila aina ya uvunjifu wa amani.Kuna wakati wanamuunga mkono mtu ambaye wanajua watamtumia kunyonya raslimali zetu hasa kiomgozi huyo akiwa na tamaa ya mali.
Miaka imeenda,nchini Tanzania Mwl aliwahi kuuliza,wakati akiongea mkoami Mbeya kuwa mtu anapohangaika kwa gharama kubwa kuingia Ikulu( mahala patakatifu), mtazameni kwa umakini mkubwa kwani Ikulu hakuna biashara pale ni kupambana na matatizo sugu ya wananchi.
Aliwahi kuonya,matumizi makubwa ya fedha kwani ipo hatari ya kugeuza ikulu sokoni.