IWE MVUA IWE JUA, FOMU YA UBUNGE YACHUKULIWA JIMBO LA VUNJO.

IWE MVUA IWE JUA, FOMU YA UBUNGE YACHUKULIWA JIMBO LA VUNJO.

KIJICHO PEVU

Member
Joined
May 4, 2024
Posts
69
Reaction score
49
IWE MVUA IWE JUA, FOMU YA UBUNGE YACHUKULIWA JIMBO LA VUNJO.

Maelfu ya wananchi wa Jimbo la Vunjo wamejitokeza kwa wingi kushuhudia tukio la kihistoria la Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Enock Koola, akichukua fomu ya kugombea nafasi ya Ubunge.

Shughuli hiyo iligeuka kuwa sherehe ya mshikamano, ambapo wananchi wa makundi yote – vijana, wazee na kina mama – walionyesha furaha na matumaini makubwa. Wengi walimuelezea Koola kama mgombea wa kizazi kipya, mwenye maono na anayegusa maisha ya wananchi moja kwa moja.

Mwandishi wa gazeti hili alipata nafasi ya kuwahoji baadhi ya wananchi waliokuwepo katika tukio hilo la uchukuaji wa fomu, nao walieleza hisia zao kwa maneno haya:

“Kwa mara ya kwanza tunaona mgombea ambaye si wa maneno tu bali wa vitendo. Tuna imani naye kwa sababu anatoka kwetu na anatambua changamoto zetu,” alisema Maria John, Mkazi wa Kata ya Uru Kusini.

“Sisi vijana tunamtazama Koola kama mfano wa kiongozi wa kizazi kipya. Tunaamini ataweka nguvu kwenye ajira na michezo,” alisema Julius Mosha, Mkazi wa Kata ya Kibosho Kati.

“Ni mtoto wa Vunjo na tunaona anajua matatizo yetu ya kila siku, hasa kilimo. Tunamuunga mkono kwa moyo wote,” alisema Mzee Andrew Mlau, Mkazi wa Kata ya Kahe.

Wachambuzi wa siasa za ndani ya Vunjo wanasema tukio la kuchukua fomu kwa Koola limeibua mshikamano mpya, huku wananchi wakimwita “Mgombea wa Mioyo ya Wana Vunjo.”

Kwa maoni ya wengi, hatua hiyo ni ishara kwamba Vunjo iko tayari kumpa nafasi mgombea kijana, mwenye maono na moyo wa wananchi wake
 

Attachments

  • IMG-20250826-WA0196(2).jpg
    IMG-20250826-WA0196(2).jpg
    183.1 KB · Views: 15
  • IMG-20250826-WA0196(1).jpg
    IMG-20250826-WA0196(1).jpg
    183.1 KB · Views: 13
  • IMG-20250826-WA0195(1).jpg
    IMG-20250826-WA0195(1).jpg
    224.7 KB · Views: 14
  • IMG-20250826-WA0197(1).jpg
    IMG-20250826-WA0197(1).jpg
    239 KB · Views: 9
  • IMG-20250826-WA0200(1).jpg
    IMG-20250826-WA0200(1).jpg
    186.1 KB · Views: 13
  • IMG-20250826-WA0199(1).jpg
    IMG-20250826-WA0199(1).jpg
    122.7 KB · Views: 14
  • IMG-20250826-WA0198(1).jpg
    IMG-20250826-WA0198(1).jpg
    110 KB · Views: 13
  • IMG-20250826-WA0202.jpg
    IMG-20250826-WA0202.jpg
    194.4 KB · Views: 15
  • IMG-20250826-WA0201.jpg
    IMG-20250826-WA0201.jpg
    164.1 KB · Views: 12
Hivi mnapokuwa mnasema vijana, Huwa hamuwajumuishi wanawake vijana ? Maana naona vijana na wanawake ...! Hapo kuwa Wazee lakini pia unaona tena unasema Akina mama. Kwani ukisema Vijana wa kike na kiume na wazee wa kike na kiume kuna kitu kitakua kimepoteza maana ??
 
Back
Top Bottom