Itv yamwachisha kazi mke wa mbunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Itv yamwachisha kazi mke wa mbunge

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Mar 11, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  [​IMG]

  Na Mwandishi Wetu
  Uongozi wa ITV/Radio One, unadaiwa ‘kumtema’ kazi ripota wake wa Morogoro, Amina Said ambaye ni mke wa Mbunge wa Mvomero, Suleiman Morad Sadiq, Risasi Mchanganyioko lina ‘fulu data’...
  Mtangazaji huyo amejikuta akipoteza ajira baada ya kujikita katika ulingo wa siasa, jambo ambalo uongozi wa kituo hicho haukuliafiki.

  Sosi wetu alikwenda mbele zaidi na kuweka ‘pleini’ kwamba, kujikita kwa Amina katika siasa kulimpa nafasi ya kujinyakulia uongozi wa ngazi za juu katika Chama cha Mapinduzi (CCM) kupitia UWT, jambo ambalo uongozi wa ITV/Radio One ulimpa nafasi ya kuchagua, ama kuendelea na kazi au kubaki kwenye siasa.

  Ikadaiwa kwamba, katika uchaguzi huo, Amina alijaza mtihani huo kwa majibu ya ‘aa na bee’ yote ni sawa, hivyo kutoa ‘chansi’ kwa uongozi huo kumuamulia.

  “Kwenye mkataba wa Amina alisaini kama mfanyakazi ‘full taimu’ wa ITV/Radio One, lakini miezi kadhaa iliyopita iligundulika kuwa ana majukumu mengine ya kisiasa.

  Akiongea na Mwandishi wa gazeti hili jijini Dar hivi karibuni, Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One, Joyce Mhavile alithibitisha kuachishwa kazi kwa Amina kwa kile alichoeleza kuwa, ‘prizenta’ huyo alibainika kujihusisha na siasa kinyume na maadili ya kazi.

  Aidha, Mhavile alisema kuwa, kwa kawaida uongozi wa ITV na Radio haupendi wafanyakazi wake kujikita kwenye siasa wakati wa majukumu, “hilo lilichangia kupoteza kibarua chake,” alisema.

  Wiki chache zilizopita, gazeti dada la hili, Ijumaa liliripoti habari ya Amina kushikilia uongozi wa CCM baada ya kujiridhisha na maelezo ya Mbunge Sadiq kuwa, yeye yupo karibu na Amina kwa sababu ni kiongozi wa CCM, mkoa wa Morogoro.

  Katika habari hiyo, ilielezwa kwamba, Amina amekuwa akisaini vitabu vya chama hicho kwa jina la Mrs. Mbunge ambapo Sadiq alipotakiwa kutoa maelezo alisema: “Hii sasa ni hatari, yaani mpaka taarifa za ndani ya chama zinaletwa kwako mwandishi, kweli hali imekuwa mbaya Mvomero.”

  Katika habari nyingine ya gazeti hilo, ilielezwa kwamba, siku chache baada ya mbunge Sadiq kuibuka na kudai kuwa, Amina ni mkewe halali, ndugu wa mwandishi wa Kampuni ya The Guardian Limited, Abdul Mitumba ambaye ndiye mume wa kwanza wa Amina, waliliambia gazeti hilo kuwa hawaielewi ndoa ya mbunge na mtangazaji huyo kwa sababu ina ‘kahistoria’ ambako si kazuri.

  Ndugu hao walinukuliwa wakisema kwamba, kabla ya Amina kuolewa na mbunge Sadiq, alikuwa ni mke halali wa Mitumba kwa ndoa iliyofungwa baada ya kutimiza taratibu zote za dini ya Kiislamu lakini ‘alimtosa’ katika mazingira yenye ‘viulizo vingi’.

  Walisema, mazingira ya Amina kumwacha Mitumba yalikuwa ya kushangaza kwa sababu ilikuwa ni miezi michache tangu alipotoka kupata ajali mbaya ya gari, iliyokaribia kuchukua uhai wake.
   
Loading...