Wakati msomaji wa taarifa ya habari saa mbili usiku jana anasoma alisema hivi "Mengi amesema kuwa watanzania waige mfano wa rais kikwete katika kuchukia umaskini" wakati najiandaa kumuondoa Mengi kwenye list yangu ya watu ambao niliwaamini angalau kidogo, mengi akawekwa hewani hakusema kitu chochote wala kutaja jina la kikwete na aliongelea kitu tofauti kabisa. Hivi hili hawa ITV hamkuliona wakati mnaandaa taarifa ya habari??? Taarifa ya habari hata sisi ambao sio professionals wa habari tunaweza kuwafundisha, wasomaji wa taarifa ya habari huwa hawana mvuto, wamenuna, wanamawazo mengi mpaka wanakosea kosea. Waigeni TBC japo wanaripoti utumbo lakini wanatabasamu hata kidogo . . .
Mkuu Joniwapili, uandaa wa taarifa za habari wa Redio na TV ni professional ya watu inayofuata misingi yake.
Kwa kawaida habari huusisha "reportage" hii ni ripoti ya kilichozungumzwa na kujumuishwa na "actualities" yaani sauti halisi ya mzungumzaji akizungumza, hii inaitwa "insert".
Kwenye reportage, kwa kawaida wazungumzaji huzungumzia mambo mengi, mwandishi atayarekodi yote na kisha kuamua atoke na angle gani!. Akishaamua angle anaandaa kitu kinaitwa "catch line" kwenye gazeti ndio headline "Mengi Ampongeza Kikwete".
Hii catch line inafuatiwa na "intro" hii ni para ya kwanza inayozungumzia subject matter, ambayo itafuatiwa na para nyingine kukamilisha, the 5Ws + H, (Who, What, When, Where, Why+How).
Baada ya kukamilika hayo ndipo hufuatia "insert" ya sauti ya mzungumzaji. Kanuni ya insert sio lazima anazungumzie yele yale yaliyoelezwa kwenye intro, "insert" inaweza kuzuzungumzia jambo jingine lolote kwa lengo la kuishibisha ile habari!, hivyo ITV wako very right!.
Hilo la kusmile, inategemea "contents" kama ni za kupendeza, mtangazaji ata smile, kama ni very seriuus mtangazaji anakuwa serious na kama ni za kuhuzunisha mtangazaji atahuzunika!. Hii tuhuma
wasomaji wa taarifa ya habari huwa hawana mvuto, wamenuna, wanamawazo mengi mpaka wanakosea kosea
ni too general as if ndio wote!, inaweza kuwa "its one isolated incident" usiishambulie ITV kwa kosa la mtangazaji mmoja!
Makosa ya kibinaadamu kwa kawaida yako yanavumilika ili sio kwa kiwango cha kuwaita "makanjanja"!.
Uandishi ni fani ya watu, nakerwa sana na watu wanaowabeza wenzao kwa kuwaita "makanjanja" kila uchao, japo nakiri level ya wengi wa waandishi wetu iko chini ukilinganisha na majirani zetu, kwa sababu wenzetu wali invest kwenye elimu ya waandishi, sisi ndio tuna invest sasa!.
Msomaji, mtazamaji na msikilizaji ana haki ya kulaumu na kuelezea kero yake asipofurahishwa, ila kwenye kulaumu huku, pia muwatendee haki waandishi!. mfano lawama hizi, mleta mada hajui chochote, kazi kujifanya "much know!"
Huku sio kuwatendea haki ITV japo nao wana madudu yao ila sio haya!.
Pasco