ITV huu ni unafiki Mkubwa

ITV huu ni unafiki Mkubwa

Sijaona ubaya wa ITV katika hili, kumbuka kila Media ina Policy zake ningekubaliana na wewe kama ungesema wabadilishe sera wanazozitumia coz kwanza walikuwa LIVE so haina umuhimu zaidi kutumia hiyo habari tena kwenye taarifa ya habari (KWASABABU watazamaji wengi walijua kuwa watakuwa LIVE), Pili kuna aina tofauti za wasikilizaji/Audience (i) Primary audience (ii) Secondary audience kwahiyo kuna watu wakiona repition of the story wanakereka sana.

Sijajua wewe upo kwenye kundi gani hapo la wasikilizaji.

Nadiriki kuwaita hivyo kutokana na jinsi walivyofanya coverage ya kufukia fukia tukio la vurugu lililotokea la jana Ubungo plaza. ITV walianza kurusha tukio hili mnamo saa 9 jana na nilikuwa nafuatilia hatua kwa hatua hadi vurugu zinatokea na Renfred Masako kusitisha matangazo ya LIVE. Cha ajabu kwenye taarifa ya habari wameshindwa kuwaeleza Watanzania kwa kina kuhusu zile vurugu ambazo ITV wana video na picha zake zote .

Badala yake wametangaza kuwa mdahalo ulisitishwa bila kuelezea vurugu zilizopelekea mdahalo huo kusitishwa. Kwa mtu ambaye hakuona asingejua intensity ya zile vurugu kama angesikiliza ITV na Nipashe. BBC leo asubuhi wameeleza vzuri sana kuhusu hizi vurugu tofauti na ITV waliokuwepo kuanzia mwanzo hadi mwisho.

Maswali yangu ni haya:

1. Mnaficha details hizi kwa manufaa ya nani?
2. Mnamsaidiaje Mtanzania kujua kinachoendelea kwa uhalisia wake kama hata matukio yaliyo obvious mnayaficha?
3. Kwani nyie ndio mliomtuma Makonda hata muogope kueleza ukweli?
4. Tukio lilijitengeneza lenyewe iweje muogope kisa eti mtaambiwa mnachochea vurugu kama si kutojua mnachokifanya?
5. Mtajiitaje chombo cha jamii wakati jamii mnaificha mambo ambayo ni obvious?
6. Jamii itawezaje kubadilika na kujitafakari kwa ajili ya kufanya maamuzi wakati triggers au vichocheo muhimu vya kufanya maamuzi mnavificha waziwazi?
7. Ni madhara gani mngeyapata kama mngeeleza ukweli kuhusu kilichotokea?

Kama ninyi mnasema mnawahabarisha watanzania basi toeni habari kwa uwazi acheni kuficha au kutoa habari kinafiki .

Kwa kilichotokea jana ITV mmekuwa wanafiki na waoga mkatoa just 30% ya kilichotokea. Kwa staili hii watanzania hawatajua kinachokula nchi yao.

Tunaomba mjirekebishe la sivyo hamtakuwa tofauti na TBC1.
 
Mh mi hata sitamani kuchangia kitu maana siku hizi ukifungua domo tu unalo,utashangaa hata umebebeshwa gunia lisilo lako.
Wameogopa yasije wakuta yale ya kuitwa wachochezi kama yule mzee mbondaji anaesubiria lihukumu lake.
Mpaka nakumbuka like song la kenya NCHI YA KITU KIDOOOO.. . . . . . . . . Utamalizia tu hapo.
Usiogope sana maana zimebaki 31 na 30 kumi na moja na 28 moja ktk 2015 katika kufanya suluhisho .
Jamani ye,alie makini atanipa vizuuuri.
Yule avumae baharini kwani nae keshaingia kwenye sirikali ya kufunika ukweli na funua uongo ?.
Mwisho.
Sijakuelewa, unamaanisha tumebaki waoga, watukuza uongo, wanafiki na wenye hila? Ebu fafanua vizuri
 
Back
Top Bottom