Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela kupitia Chama cha Alliance For Democratic Change (ADC), Shabani Itutu ameitaka Serikali itoke hadharani kukemea matukio ya utekaji yanayoendelea kuripotiwa nchini
Akizungumza na wananchi kwa nyakati tofauti kwenye ziara ya kampeni ya mtaa kwa mtaa katika kata ya Kahama, Busweru, Kangahe, Kirumba na Kitangiri, Shabani Itutu amedai kitendo cha Serikali kuendelea kukaa kimya kinaweza kupelekea kushamili kwa matukio hayo na kuonekana ya kawaida katika jamii hali itakayokuwa inahatarisha usalama na amani nchini
"Toka utekaji utokee sijaiona Serikali ikitoka hadharani kukemea utekaji, tunaiomba Serikali itoke hadharani ikemee utekaji, watoto wa wenzao wa maskini wanatekwa huku wakiacha masikitiko kwa familia zao wakati walikuwa wakitegemewa," amesema Itutu
Ameongeza kuwa "Utekaji umetawala hii nchi lazima tuukemee kwa pamoja tusipokemea utekaji utakuja kuvunja amani ya nchi, watu wataona utekaji ni jambo la kawaida, utekaji unaumiza sana chukulia ametekwa baba, dada, kaka, shangazi yako halafu watu wanadunda hawachukui hatua yoyote,"
Hata hivyo Itutu amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kuchagua viongozi watakao waletea maendeleo huku akiwataka wananchi kuwapuuza wale wote wanaokusudia kufanya maandamano