Itumie intaneti, isikutumie

Itumie intaneti, isikutumie

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
53,287
Reaction score
72,512
Kuna watu ikipita siku, saa, dakika au hata sekunde bila kuwasha data wanajihisi kama wanahisi kufa hivi.

Wengi wa watu wa namna hii ni watu ambao intaneti inawaendesha na baada ya kuitumia wao wameanza kutumiwa na intaneti.

Hebu jiulize intaneti kwako inatumika kwa matumizi gani?

Je ni kuperuzi habari na kutaka kuwa updated?

Je ni kujifunza vitu ambavyo ni vya manufaa.?

Je ni kupost picha na kulike?

Je ni kutizama video za miziki mipya na video za vichekesho?

Je nikuandika meseji za vituko na kuzitoa group moja kuzipeleka pengine?

Je ni kutangaza biashara zako na kufanya mauzo?

Ukweli ni kwamba asilimia kubwa ya watu wamekuwa wakifanya mambo ya ajabu kupitia intaneti. Intaneti haiwafaidishi bali inawadumaza na kuwafanya wajinga. Lakini upande mwingine kuna watu waliojua umuhimu wa intaneti na Leo hii wamekuwa watu wakubwa kupitia intaneti na mitandao ya kijamii. Richard Branson mwandishi wa kitabu cha Screw it, Let's do itanasema "intaneti imefungua milango mingi. Kuna kazi na chansi nyingi za kufanya mauzo mtandaoni. Imebadili maisha ya watu wenye mawazo na nguvu."kwa mantiki hiyo unaweza kuona kwamba watu wenye mawazo na nguvu ndio wameweza kufaidika kutumia intaneti.

Je wewe una mawazo na nguvu?
Kumekuwa na ukosefu wa ajira hapa nchini lakini vijana wengi wasomi wamechelewa kuijua fursa hii ya intaneti na kuichangamkia. Intaneti imekuwa sehemu kubwa ya kujifunza lakini ni watu wachache wamechukua muda wao na kufanya hivyo.

Leo hii nikitaka kujua wewe ni mtu wa namna gani naweza kukufahamu kupitia akaunti za mitandao ya kijamii. Kwa mfano picha 3 tu za mwanzo za Instagram yako zinaeleza kwamba wewe ni nani!. Ndiyo maana Leo hii kwenye usaili makampuni mengi yanaangalia mtu wanayetaka kumpa ajira anaweka nini mtandaoni na wanaweza kujua anafaa au hafai.

Hivi unajua wewe msomi kuna watu wangependa kujua mambo mengi na ujuzi Fulani ambao unausomea lakini wanaukosa. Na ukiweza kutoa ushauri wa kitaalamu kupitia mitandao ya kijamii na wakaja kukulipa pesa. Kumbuka hii haihitaji uwe umehitimu chuo, unaweza kuanza toka ukiwa hapo chuoni. Nakukumbusha tu kwamba Mark Zuckerberg alianza kutengeneza Facebook akiwa bado anasoma chuo. Wewe pia unaweza kuanza kuonesha ujuzi wako kupitia intaneti na unaweza kutengeneza pesa kubwa.

Unaweza kusema muda hamna wa kufanya mambo kama hayo. Hebu nikuulize?
[emoji420] Unapata wapi muda wa kufuatilia tamthilia na kuangalia movies na series?
[emoji420]. Unapata wapi muda wa kutizama mpira na kuchambua kwa kina soka kufikia level za kina Shafii Dauda?
[emoji420] Unapata wapi muda wa kutiza video mbalimbali za vichekesho na muziki YouTube?
Tambua kwamba hao unaowatizama na kuwafatilia wameweka juhudi na kupiga kazi haswa ndiyo maana Leo unaweza kuwaona kama walivyo.

Leo hii amua kutumia mitandao ya kijamii kwa manufaa yako ya Leo na kesho kutwa. Ukibaki kuzubaa utaona wenzako siku za mbeleni wanafurahi wewe unasema ningejua.

Jua kwamba kila picha unazoweka Instagram au Facebook ili watu waje kulike na kukomenti kuna watu wanaingiza pesa kupitia like na komenti unazopata. Wewe unaishia kusifiwa tena wakati mwingine sifa za kinafiki. Sina maana kwamba uache kuweka picha mtandaoni lakini nataka ufikiri kwa jicho la kipekee, wewe utawezaje kufaidika na mitandao ya kijamii na intaneti.

Watu wengi mitandao ya kijamii na intaneti vinatufaidi badala ya sisi kuvifaidi.

Jiulize je? Kila bando ninayoiunga ninapata faida nayo au nakula tu hasara.

Changamkia fursa ya intaneti. Itumie intaneti na hakikisha haikutumii.

Naomba nikuache na msemo wa Robert Kiyosaki "Leo hii unaweza kufanya biashara kirahisi zaidi ya ilivyokuwa hapo zamani. Ukiwa na simu tanashati(smart phone) unaweza kuuza chochote. Kama unamiliki simu tanashati (smart phone) na haujawahi kuuza chochote, tambua yakwamba unafanya makosa makubwa."

Mafanikio yako mikononi mwako.

Copy and Paste (bideism blog)

Share kwa marafiki zako kuwakumbusha jambo hili. Imani yangu ni kwamba mafanikio ni kitu cha kushirikishana.
 
Umerudi na taarifa muhimu sana kwa watz na watumiaji wote wa mitandao.Ukitaka kujua hilo mtoa mada jaribu kuangalia wanachokiangalia abiria ktk simu zao ndani ya mabasi ya mwendokasi asubuhi au jioni ile mshanano unapokuwepo.....
 
Kumbe Joseverest unakuwaga na point
 
Back
Top Bottom