Itoshe kusema kwamba Serikali Awamu 5 ina Sura 2 (Double Standards)

tajirijasiri

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
2,863
3,851
Msema kweli ni mpenzi wa Mungu.
Bila kupepesa Maneno, Serikali ya awamu 5 ina sura mbili, na tabia ya namna hiyo huwa tunaiita unafiki/Udumilakuwili/Udananda/Double standards.

Mifano:-
1. Unawezaje kusema unawajali wananchi wa Chini huku Serikali yako inafukuza Chuo watoto 7,000 wa maskini (Sakata la Udom), ili hali Serikali hiyo hiyo iliwadahili?!?!

2. Unawezaje kusema unapambana na Rushwa na Ufisadi huku unaachia Escrow, Lugumi, Nyumba za Umma, Meli Chakavu, Richmond/Dowans, Mabehewa fake, Kiwira, Kagoda, Meremeta, EPA, Uchakachauji Uchaguzi na Katiba, Kuhamisha matumizi ya fedha za umma bila idhini ya Bunge, Kupuuza Sheria, Kanuni, na taratibu za Utumishi wa umma ktk kuwawajibisha wakosaji n.k.!?!?!

3. Unawezaje kusema unawajali wafanyabishara na wenye viwanda, huku juzi juzi kwenye sakata la Uhaba wa Sukari, wewe na Serikali yako mmewatisha kwa kauli ya ".... Wanacheza na Maisha yao". Wakati Uhaba huo ulisababishwa na maamuzi ya kukurupuka kuzuia Uingizaji sukari nchini ili hali uzalishaji wa ndani hautoshelezi!?!?!

4. Unawezaje kwenda kwenye Luninga kutangaza juu ya kutokutumika Pump za Mafuta Bandarini, kisha kusimamisha watendaji, halafu siku chache baadae kimya kimya ukaruhusu zisitumike, bila kurudi kwenye Luninga?!?!

5. Unawezaje kumuacha Mbunge wa CCM, aliyezalilisha wanawake Bungeni, kisha ukawafukuza wabunge wa Upinzani, waliokuwa wakitetea Haki ya kupata Habari (Bunge live) na Kupinga Ufisadi wa Lugumi?!?!

Tuache tabia hizi.
 
Back
Top Bottom