Itawezekana mimi na yeye kuoana kweli?

Itawezekana mimi na yeye kuoana kweli?

rubylove

Senior Member
Joined
Jun 1, 2015
Posts
127
Reaction score
42
Mimi ni msichana nina miaka 22, nilipoanza kusoma kidato cha 1,nilikuwa nakaa na dada angu tumezaliwa baba 1mama1 pamoja na shemeji yangu asa hapo nyumbani alikuja mtoto wa mjomba wake na shemeji yangu, ambae wamechangia babu ila bibi tofauti nae alikuja kusoma. Kadri tulivyokuwa tunakaa ndo tukapendana na tulipendana kwelikweli ila bila ya kujihusisha na ngono na tuliahidiana kwamba mpaka tutakapo maliza masomo yetu tuje tuoane.

Tulipomaliza masomo ya kidato cha nne tulijihusisha na mapenzi na yeye ndio mwanaume wangu wa kwanza( alonitoa bikra.)kwa kweli alinipenda sana na mpaka leo ananipenda sana huo uhusiano wetu ndugu baadae walikuja kugundua ndugu zake wananipenda na wanapenda sisi tuje tuoane.

Ila kwa upande wangu na hasa wazazi wangu hawataki mimi na yeye tuje tuoane na tusitishe mahusiano yetu niliwahi kumwambia mwenzangu tuachane, alilia sana mimi pia nampenda sana na ukizingatia ndo mwanaume wangu wa kwanza tunaruhusiwa kuoana au ni vibaya.? Mawazo yenu tafadhali

Naombeni ushauri wenu
 
Wazazi wako ongea nao kwa uwazi kwamba mwisho wa sikuwewe ndo mchaguzi wa mwisho na muidhinishaji wa mwisho kuhus kuchaguA mwenza wako wa baadae waambie ni ww utakaa na huyo MTU sio wao wabakie Kama washaur wakuu kwako wazaz wetu ni waelewa Sana ikiwa tu utaongea nao kwa utaratibu unaotakiwa
 
Sina cha kuongezea madam umemalizaa kilaa kitu.
 
...ila kwa upande wangu na hasa wazazi wangu hawataki mimi na yeye tuje tuoane na tusitishe mahusiano yetu

Ndugu zako wanatoa sababu gani za kukataa ninyi kuelekea ndoa?
 
Wanamkataa tu bila sababu kweli au? hebu tueleze hoja zao nini?
 
Wazazi wako ongea nao kwa uwazi kwamba mwisho wa sikuwewe ndo mchaguzi wa mwisho na muidhinishaji wa mwisho kuhus kuchaguA mwenza wako wa baadae waambie ni ww utakaa na huyo MTU sio wao wabakie Kama washaur wakuu kwako wazaz wetu ni waelewa Sana ikiwa tu utaongea nao kwa utaratibu unaotakiwa

Wewe ndie amabaye utakaa nae na sio wao waambie na waombe wakubali na waheshim hisia zako..Nawatakia ndoa njema
 
Mbona hapo hakuna tatizo kaana nao tu na ikibidi wawepo na watu wengine wa heshima kwenye jamii yenu posa itakubaliwa tu..
 
rubylove

Haramu kuoa/kuolewa naye ni yule uliyezaliwa naye tumbo moja na yule mnayeshea naye baba.
 
Last edited by a moderator:
Afu' hizi mada zenu siku za kupendana na kutaka kuwa pamoja ndugu kwa ndugu wa damu moja mmeshaona fasheni?? Hili nalo mtahitaji hadi wazungu wafanye utafiti na kutuambia kuwa si sawa na hata wao hawafanyi? ...kama kweli huko mbeleni kuna moto basi kuna watu watakuwa kuni za kuchochea.
 
sijui umesoma mada vizuri
 
Wazazi wako ongea nao kwa uwazi kwamba mwisho wa sikuwewe ndo mchaguzi wa mwisho na muidhinishaji wa mwisho kuhus kuchaguA mwenza wako wa baadae waambie ni ww utakaa na huyo MTU sio wao wabakie Kama washaur wakuu kwako wazaz wetu ni waelewa Sana ikiwa tu utaongea nao kwa utaratibu unaotakiwa
Asante kwa ushauri ntaufanyia kazi.ntaongea nao tena.
 
rubylove

Haramu kuoa/kuolewa naye ni yule uliyezaliwa naye tumbo moja na yule mnayeshea naye baba.

nashukuru kwa ushauri.ntajaribu kuongea nao japo wanielewe
 
Last edited by a moderator:
sababu ya wao kukataa.ni kwamba haiwezekani mm na dada angu kuolewa nyumba moja.

Hii sababu nyepesi mno...

Hata huo undungu wa shemejiyo na huyo kijana upo mbali...

Fanya hima uwaeleweshe wazazi wako...
 
Haitawezekana kabisaa kwa sababu moja tu kuwa wasichana wengi hawaolewagi na wanaume waliowatoa bikira.....mfano ni mimi mwenyewe wasichana 8 niliwatoa bikira na sijawaoa nimeoa ambaye alishatolewa na dume mwingine ambaye alimuacha kama mi nilivyoachana na hao 8.
 
Miaka 22 unawaza kuolewa???
Sio siri ndo maana wazazi hawataki uendelee na huoo uhusiano.
Soma kwanza ukimaliza ukawa na maisha yako wazazi hawatoweza kukataa kamwe...
 
Haitawezekana kabisaa kwa sababu moja tu kuwa wasichana wengi hawaolewagi na wanaume waliowatoa bikira.....mfano ni mimi mwenyewe wasichana 8 niliwatoa bikira na sijawaoa nimeoa ambaye alishatolewa na dume mwingine ambaye alimuacha kama mi nilivyoachana na hao 8.

Daaaah yani ww ukiwa Dr wa magonjwa ya binadamu wagonjwa watakufa sana duuuuuuuuuu....!
 
Back
Top Bottom