Itakavyoandikwa Historia ya Tanzania mwaka 3015

Itakavyoandikwa Historia ya Tanzania mwaka 3015

GAZETI

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2011
Posts
5,292
Reaction score
6,773
Wakuu hii ni sehemu ya au ukurasa wa moja ya Vitabu vya historia ya Tanzania
mwaka 3015.


Kwa hiyo Tunaona wazi kuwa kizazi cha karne ya 20 kurudi nyuma kilikuwa
kizazi chenye akili na fikra sahihi kuliko hiki cha karne ya 21. Ukiwa na mtazamo
wa haraka unaweza kuhisi kuwa kizazi cha karne ya 21 ndicho kilichokuwa
na watu werevu zaidi.

Ukweli ni kuwa kizazi cha karne ya 21 kilikuwa na viongozi wakatili tena wa ajabu
ambao walithubutu kuwahimiza hata askari kuwa wapige raia.
Huu ukosefu wa rasilimali tulionao ni makosa ya viongozi hao ambao walizigawa
rasilimali zetu kwa mataifa ya Ulaya, Amerika na Asia.

Viongozi wa karne za nyuma walithubutu kupambana na wakoloni hawa wa
kimagharibi ili kulinda mali na utu wao ingawa walikuwa na silaha hafifu sana
Kinyume cha viongozi wa karne ya 21 ambao walidiriki kuwaamrisha raia kupiga
Deki barabara, kufunga biashara zao pia kuwaficha hata walemavu katikati ya
miji wakidai kuwa hao nao ni sehemu ya uchafu.

Ni kizazi ambacho kilikuwa na viongozi waliojidhalilisha wao na viongozi
wao kwa kuwanyenyekea viongozi wa magharibi kana kwamba ni miungu
lakini jambo la kushangaza ni kuwafanyia yote haya wakati wao ndio walikuwa
wahitaji wa kubwa wa rasilimali zetu ambazo kwasasa ziko huko ulaya.

Kizazi hicho ndio kimekuwa chanzo cha nchi yetu kuwa na makorongo na mashimo
ya ajabu. Miaka hiyo Tanzania ilikuwa na wanyama kama Twiga, Tembo na wengi
wengineo lakini wote walisafirishwa na kupelekwa mataifa ya Ulaya na Uarabuni
Mababu zetu hao hawakufikiria kabisa kama kuna kizazi kingine kinakuja na watahitaji
rasilimali za nchi yao..............................

Wakuu kitabu ni kirefu nimechukua sehemu tu ya ukurasa.
 
very interested story, ninahofu kama watapata muda wa kusoma au ndio utumwa, ama ukoloni mambo leo utakuwa umekolea.
 
Back
Top Bottom