Mandakakawa
Senior Member
- Mar 29, 2017
- 113
- 56
Ni kweli kipato cha mwalimu sio kikubwa lakini serikali yetu pendwa hususani ya mkoa wa Dar es Salaam ingetafuta mbinu nyingine ya kuwasidia walimu hususani kwenye suala la usafiri na sio hii ya kuwaambia wasilpe nauli kwenye daladala wanazopanda na wanafunzi wao.
Leo katika harakati zangu za kuingia mjini kati kutafuta riziki ya leo yangu mimi na kesho kwaajili ya familia nikianzia huko pembozoni mwa jiji niko kwa daladala zisizokuwa na route rasmi nauli yake 500 ghafla konda anaanza kuokota mia tano tano zake na 200 kwa wanafunzi mara anafika kwa mdada mtanashati konda anamuomba nauli dada wa watu anatoa anazama kwa handbag anatoa kitambulisho.
Haki ya Mungu mineno iliyotoka kwenye mdomo wa Konda ni ya udhalilishaji mkubwa. Hebu fikiria pale yupo na wanafunzi wake, hivi huko mashuleni heshima kati ya wanafunzi na walimu ipo kweli?
Wazo ni zuri sana ila linitakiwa lifanyiwe kazi zaidi hasa kwa walimu wa mijini.