IT team ya CCM vs IT team ya WAZALENDO hapa JamiiForums!

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,056
10,721
Kweli CCM imeishiwa sana!.

Kilichobaki ni kutumia nguvu tu ya vifaru na mabomu. Hakuna hoja wala ushawishi.

Humu ndani wameajiriwa watu wanaoitwa wataalam wa IT (kwa mujibu wa Kikwete), eti kazi yao ni kutengeneza propaganda dhidi ya upinzani (LOL).

Kichekesho, hawa jamaa ni hovyo kuliko maelezo. Mara nyingi huja na hoja za hovyo, muflisi na uzushi wa hali ya juu.

Ukweli ni Wapuuzi wa kupuuzwa!
Mfano leo nimesoma mabandiko yao eti Katibu mpya wa CHADEMA alishiriki mgomo ama kuchochea mgomo wa Madktari Muhimbuli ambao mgomo huo ulilenga KUDAI MASLAHI BORA na MAZINGIRA MAZURI YA KUHUDUMIA WATANZANIA.

Najiuliza, Kama Muhimbili hapakua na tatizo Magufuli alikwenda pale mara mbili mbili kufanya nini?!

Acheni unafiki. Mwisho wa siku mtamuaibisha Magufuli kwa swaga zenu za Bagamoyo!
 
Kwamba huo mgomo haukuwa na madhara ???are you serious..?
Nimekwambia hakuna mgomo ambao hauna madhara. Walipogoma Madereva kuna watu walikufa kwa kuwa walishindwa kwenda kufanyiwa matibabu kwa wakati, lakini viongozi wa mgomo ule ndiyo walikuwa mstari wa mbele kumpigia kampeni Magufuli, jee na wao CCM waliwatumia bila ya kujali madhara yaliyosababishwa na mgomo wao?
 
Kwamba huo mgomo haukuwa na madhara ???are you serious..?
waligoma kwa sababu serikali ya CCM ilikuwa inawalaza wagonjwa chini pale muhimbili. ..pia kwa sababu serikali ya CCM ilikuwa inahujumu ufanyaji kazi wa CT Scan pale muhimbili
 
Kweli CCM imeishiwa sana!.

Kilichobaki ni kutumia nguvu tu ya vifaru na mabomu. Hakuna hoja wala ushawishi.

umu ndani wameajiriwa watu wanaoitwa wataalam wa IT (kwa mujibu wa Kikwete), eti kazi yao ni kutengeneza propaganda dhidi ya upinzani (LOL).

Kichekesho, hawa jamaa ni hovyo kuliko maelezo. Mara nyingi huja na hoja za hovyo, muflisi na uzushi wa hali ya juu.

Ukweli ni Wapuuzi wa kupuuzwa!
Mfano leo nimesoma mabandiko yao eti Katibu mpya wa CHADEMA alishiriki mgomo ama kuchochea mgomo wa Madktari Muhimbuli ambao mgomo huo ulilenga KUDAI MASLAHI BORA na MAZINGIRA MAZURI YA KUHUDUMIA WATANZANIA.

Najiuliza, Kama muhimbili hapakua na tatizo Magufuli alikwenda pale mara mbili mbili kufanya nini?!

Acheni unafiki. Mwisho wa siku mtamuaibisha Magufuli kwa swaga zenu za Bagamoyo!

Naona wengine wanajichanganya wanasema eti ni TISS ndani ya cdm!!
 
Inakuaje Mbowe haamini Viongozi wenzie ndani ya Chadema kiasi kwamba huchagua viongozi na wagombea kutoka nje ya Mfumo wa Chama?
Mgombea Urais ( Lowassa) kamtoa CCM
Mgombea Mwenza (Juma Duni) kamtoa CUF
Mgombea uspika kamtoa CCM
Makamu Mwenyekt (Salum mwalimu) kamtoa Vodacom akiwa Afisa habari
Sasa leo kawaletea Katibu kutoka kwny NGO.
Kama Mwenykt haamini viongozi wenzie iweje Wananchi wawaamini?
 
Back
Top Bottom