afsa
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 1,986
- 1,585
Baada ya kufuatilia sakata la Daudi A. Bashite, nimejiridhisha kuwa Serikali yetu inawadanganya watanzania na watumishi wa umma.
Suala la uhakiki lilianzishwa na Rais mwenyewe. Alienda mbali akamtumbua Anna Kilango aliyedanganya kuwa hakuna watumishi hewa wala waliogushi vyeti. Hapa Rais nilimpongeza kwa muadhibu aliyedanganya umma wa watanzania.
Kutokana na kadhia hii watumishi wasio na chembe ya u hewa na vyeti fake wamekosa haki zao za kitumishi zifuatazo;
1. Wamenyimwa/wamekatiliwa kuhama kwa sababu za uhakiki wa vyeti fake na watumishi hewa kila kitu kimesimama kwa watumishi hawa wasio na hatia ambao wameshakamilisha taratibu za kuhama. Hawawezi kufanya maendeleo yoyote kwa kuwa hawajui kesho nini hatma ya uhamisho wao. Ndoa zao zinamegwa. Wanafanya kazi kwa stress nk.
2. Hadi sasa wamesitishiwa kupanda madaraja, vyeo na nyongeza ya mshahara kwa sababu ya watumishi hewa na vyeti fake.
3. Hadi sasa wamesitishiwa kulipwa stahili zao mbalimbali kwa sababu ya watumishi hewa na vyeti fake.
4. Ajira mpya kwa madaktari, waalimu nk zimesitishwa kwa sababu ya watumishi hewa na vyeti fake.
Haya yote waliositishiwa watumishi na watanzania nimejiridhisha kuwa hayana uhusiano na uhakiki wa watumishi hewa na vyeti fake kwa sababu zifuatazo;
1. Kuachwa kwa Mkuu wa mkoa wa Dar-es-salaam anayesadikiwa kughushi vyeti aendelee kuhudumu kama Mkuu wa mkoa.
2. Kukaa kimya kwa Rais bila kuwashughulikia wale wote waliotuhumiwa kughushi vyeti waendelee kuhudumu ktk serikali yake huku wale wasio na watu wa kuwakingia kifua wakitimuliwa na kufunguliwa mashtaka mfano walimu, manesi nk.
3. Kumuteua tena Anna Kilango aliyedanganya umma bila kutueleza watanzania nini kilitokea akamtumbua na nini kimejiri akamteua muongo tena.
Baada ya kujiridhisha kuwa hakuna nia thabiti ya uhakiki kama kigezo cha kuwakatalia kuhama watumishi, kuwasitishia stahili zao, kuwasitishia ajira vijana ,uhakiki huu uache hauna tija kama unaangalia nani ashughulikiwe na nani aachwe.
Mwisho Naomba serikali itoke hadharani iseme kwa nini watumishi hawaruhusiwi kuhama hata kama wanajihamisha, kwa nini hawalipwi stahili zao na kwa nini hawawaajiri vijana wetu.
Hii ya watumishi hewa na vyeti fake sio sababu ya kusitisha hayo yote, toeni sababu nyingine tutawaelewa na kuwavumilia.