njiwaji
JF-Expert Member
- Jul 15, 2015
- 279
- 202
Leo jioni kuanzia saa mbili kasoro ishirini, yaani saa moja na dakika arobaini (1:40 or 7:40pm) satelaiti angavu sana iitwayo International Space Station (ISS) intaonekana angani, ikitokea upeo wa kaskazini-magharibi.
Ramani hizi zinaonesha njia yake angani kwa miji mbali mbali na maeneo ya jirani yao.
Cha kushangaza ni kwamba mwanga mkali wake utakatika ghafla baada ya kutembea nusu to ya anga kwa dakika mbili hivi kwa sababu ya kuingia katika kivuli cha Dunia.
Kila ramani inaonesha njia, muelekeo pamoja na muda kamili wa kuchomoza na kupotea angani kwa kila mji na jirani zake
Kwa Dar es Salaam: inapanda juu kiasi kwa dakika mbili halafu inapotea ghafla.
Kwa Morogoro: inapanda juu karibu na utosini halafu ina potea
Kwa Mbeya: haipandi juu sana na itakuwa jirani na upeo wa kaskazini mashariki
Kwa Mwanza: inapita anga lote kuanzia kaskazi magharibi hadi karibu na kusini.
Kwa Arusha: Inapanda juu angani hadi utosini na inapita jirani sayari ya Mushtarii(Jupiter) kabla ya kupotea ghafla
Kwa Mtwara: - haipandi juu sana