Israel Mwenda umekubali kukaa miezi 6 bila timu?

DELETED ACCOUNT

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2010
Posts
9,805
Reaction score
15,476
We dogo una vielement vya kutojitambua au labda unajichukulia poa kiasi kwamba timu nazo zinakuchukulia poa.

Umeingia anga za usajili wa kimhemko wa Yanga ambao siku hizi wanasajili wachezaji ili kuikomoa Simba.

Huko ulipokwenda umekuta mambo hayaeleweki, timu haiwezi kusajili ina madeni mengi kama ya serikali. Ungekuwa na manager anayejitambua angeuliza hilo kwanza kabla haujatia saini.

Wamekupa mkataba wa miezi 6 ila hakuna mashindano utacheza maana haupo katika usajili rasmi wa NBC wala CAF. Baada ya miezi 6, kiwango chako kitakuwaje?

Soma Pia: Beki wa zamani wa Simba SC, Israel Mwenda atua Yanga kwa Mkopo akitokea Singida Big Stars

Mwisho wa msimu hao Yanga watakutupa maana lengo halikuwa kukusajili bali kukuharibia ili Simba isikurudishe. Picha la Baleke linaenda kukurudia wewe.

Pole sana. Binafsi niliona ulifaa kuwa mbadala sahihi wa Kapombe ila ndiyo hivyo haukuwa na subra.

PS. Kama vipi na wewe unga tela nenda zako FIFA kajikusanyie maokoto.
 
Kwa hiyo atachukua namba ya nani, Yao au Kibwana? Na atacheza wapi bila kusajiliwa?
Mwenda anacheza mbele ya hao wote nadhani uongozi unafanyia kazi hayo mambo kama walimchukua na wanamlipa lazima atacheza
Naangalia hapa marudio ya game ya Jana mwenda anahitajika sana
 
Ila si tulikubaliana hakuna mchezaji wa Simba anaweza pata namba pale Yanga? Zimebaki siku mbili dirisha lifungwe, ngoja tusubiri tuone.
 
Wapo wanaweza kupata number Zimbwe Kapombe Kagoma hata fadlu tunaweza kumpa yanga under 20
Nb:Mwenda ni mchezaji wa Singida
 
Nainjoy kuwavuruga hawa vyura. Hapo nasubiria mwarabu amalize kazi kwa mvurugano mkuu. Robo fainali iz not 4 everibade.
Ule uwanja unapikwaa yani wikii hii ni machinjio ya wanyama...damu lazima imwagike tuu mle..mpk tukicheza jumapili tutaona vumbi...hahaaa chezea robo fainale... 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
 
Wanafungika vizuri tu pamoja na makafara yao
 
Dogo nilimuonya. Yanga imeona aibu kujaza wachezaji wa Simba, imeamua kuwapunguza ili kutoa nafasi kwa Zimbwe. Sikujua hii timu wana mshipa wa aibu, nimeshangaa sana.
 
Aisee kwa nini umebadili username yako kutoka SAYVILLE mpaka PASADENA? Maana na nduhi yako OKWIBOBAN SUNZU naye ameamua kujiita Kipenzi Changu!! 😱
Pili ukubali tu utabiri wako haukutimia. Kwa sababu baada tu ya usajili dogo IZRA alijimilikisha namba mbele ya Kibwana na pia majeruhi Yao Kwasi.

Nina uhakika pia kwa kiwango alichokionesha pale Yanga ndani ya muda mfupi, uongozi wa timu chini ya rais Hersi Said utakaa mezani na mchezajo ili kifikia muafaka wa kumaliza kwenye ishu yake ya uhamisho.

Binafsi bado ninatamani kumuona Israel Mwenda msimu ujao akiwa na jezi ya Yanga. Na pia ninamuinga mkono kwenye kudai hela yake ya usajili kutoka Yanga baada ya Yanga kumalizana kinyemela na Singida Black Stars, huku mchezajo akiwa hajaambulia chochote.

Yanga impe huyu dogo hela yake ya usajili ili msimu ujao aendelee kukinukisha.
 
Mwenyewe umekiri kuwa mpaka sasa Yanga imemtapeli Mwenda halafu unasema utabiri haujatimia.

Hata kupata namba mbele ta wale aliowakuta inaendana na kile ambacho nimekuwa nasema na niliwapinga nyie mashabiki maandazi mnaosemaga hakuna mchezaji wa Simba anayeweza kupata namba kikosi cha kwanza cha Yanga.
 
Israel Mwenda ilikuwa rahisi kwake kupata namba kwenye kikosi cha kwanzs kwa sababu Yao Kwasi alikuwa nje kutokana na majeraha ya muda mrefu. Usijipe uspecial usio na ulazima.
 
Kwani hiyo namba ilikuwa inachezwa na Yao peke yake?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom