Israel inaomba silaha!!

Hakuna kosa. Ila kuna watu humu bila hata soni eti wanasemaga Israel ni zaidi ya Marekani katika kila kitu ikiwamo uchumi, nguvu za kijeshi, influence, na kadhalika, kitu ambacho si cha kweli hata kidogo.


Mkuu hujalijua vizuri hili Taifa, hiyo ni janja tu. Utaona mwenyewe, ! si hapo wameomba? subiri waingie vitani ndipo utagundua ilikuwa geresha
 
Hakuna kosa. Ila kuna watu humu bila hata soni eti wanasemaga Israel ni zaidi ya Marekani katika kila kitu ikiwamo uchumi, nguvu za kijeshi, influence, na kadhalika, kitu ambacho si cha kweli hata kidogo.

Kwa hiyo wewe unakosa usingizi kwa kuwa tu fulani wa JF amesema mkeo sio mzuri kama mke wake?

INFLUENCE: Hapa ungetueleza influence kwa nani na kwa lipi. Kwa mfano: Israel ina influence kubwa Marekani kuliko Tanzania.
 
Mkuu hujalijua vizuri hili Taifa, hiyo ni janja tu. Utaona mwenyewe, ! si hapo wameomba? subiri waingie vitani ndipo utagundua ilikuwa geresha

Sijalijua vizuri taifa lipi? Israel? Kama ni hao basi hawana lolote zaidi ya kuwa hyped na wanazi wa kidini.

Bila Marekani kuwabeba hawana lolote hao.
 
Umenikuna! Sina cha kuongeza wala kupunguza.
 
Kwa mtu asiyejua siasa za mashariki ya kati anaweza kushawishiwa na ulichoandika. Kumbe ni UTUMBO tu. Nani asiyejua kuwa Jeshi la Israel (IDF) ndiyo jeshi makini zaidi na committed kuliko jeshi la taifa lolote duniani including Marekani! Ukisoma historia ya IDF na mambo waliyofanya maeneo mbalimbali duniani utabaki kinywa wazi na kama una akili nzuri utajiuliza kama matendo hayo yalikuwa yanafanywa na binadamu au la. Ipo mifano mingi sana mojawapo ikiwa ni 90 minutes to Entebbe na kulipuliwa kwa ndege za kirusi zikiwa Egypt zikijiandaa kushambulia Israel. Endeleeni kujipa moyo kwamba Israel hakina kitu wakati mataifa yote ya kiarabu pamoja na hasira zao za kujitoa muhanga, wameshonwa mdomo na hawakohoi hata sekunde mbele ya wayahudi.
 

Israel bila misaada hakuna kitu hapo...ni USA ndio msingi wa mafanikio ya Israel otherwise ingekuwa sawa na kenya
 

Uvamizi wa Entebbe nao unauhesabu? Wacha maskhara bana.

Halafu kama hao wa Israel are all that, kwa nini wanaenda Marekani kuomba misaada ya zana za kijeshi? Si watengeneze tu za kwao...
 
Sijui nianzie wapi,ila wale Waisrael wapo juu sana wana silaha nzito sana lakini cha ajabu hawakuweza na hawataweza kuwamaliza Wapalestina,unajua Sababu ni IPI? Soma kitabu Cha Mwanzo kuanzia sura 16,utajua ya kuwa Abramu alifanya Makosa gani,na adhabu yake ni chuki kwa Vizazi vyake Vinne kwa hao waarabu. Kingine ni kwamba HAKUNA uganga wala Uchawi mbele ya Israel. Hakuna VITA ambayo Israel alipigana na akashindwa.
 

Kama wanazo kwa nini wanaenda Marekani kuomba?
 
Kama wanazo kwa nini wanaenda Marekani kuomba?
NN this time Israel are bluffing and Iran can see right through them,they have no capability to take out Iran's nuclear sites(at least 12 sites) all over Iran. They can maybe bomb 1-2 stes that may only anger Iran to break from the IAEA and make all dialogue imposible.
 
Israel bila Marekani haiwezi ku survive huko Mashariki ya Kati. Kijeshi karibu kila kitu wanategemea toka Marekani.

Ni vigumu kutenganisha mataifa haya mawili mkuu. Utafiti wa ndege unazozisema unafanyika Israel, ndege za kivita zisizo na rubani tafiti zake pia Israel halafu teknolojia inasambazwa marekani. Intelijensia ya jamaa iko juu sana hata marekani wanawatumia sana katika shughuli zao. Nchi za mashariki ya kati hazina uwezo wa kuisumbua Israel hata bila marekani isipokuwa historia inaonesha kuwa marekani ndio walioikomboa Israel toka kwenye janga la Hitler wakati wa vita kuu vya dunia na hii ni mipango ya Mungu.

Umesoma habari za Iron dome inayotumika kuzuia rockets? watafiti na wavumbuzi wakubwa ndio wao. Hivyo Marekani huwatumia wao katika mambo hayo na wao wanafaidika kutoka katika mabraza zao marekani. Israel wanataka kuivamia Iran, ila nfikiri mjomba Obama anajiandaa na uchaguzi ndio maana kawaambia tulieni kwanza.
 
Hakuna kosa. Ila kuna watu humu bila hata soni eti wanasemaga Israel ni zaidi ya Marekani katika kila kitu ikiwamo uchumi, nguvu za kijeshi, influence, na kadhalika, kitu ambacho si cha kweli hata kidogo.

Hebu look at this:
Ilichukua siku 6 kwa Israel kupiga Nchi tatu za Kiarabu: The Six-Day War Six-Day War - Wikipedia, the free encyclopedia

Je, Marekani, imechukua miaka mingapi kuipiga nchi moja tu, Afghanistan? Newt Gingrich: End the war in Afghanistan | Washington Times Communities Jamaa wanataka kumwaga manyanga hapa.

Kwahiyo, kuwa na vifaa na jinsi ya kutumia vifaa ni vitu viwili tofauti. America wana Vifaa vikali na inawachukuwa miaka kibao kuwathibitu Afghanistan in constrast, Myahudi anaomba Marekani Vifaa na anachukua Siku 6 kuwatwanga Wamanga 3.
 
Nani asiyejua kuwa Jeshi la Israel (IDF) ndiyo jeshi makini zaidi na committed kuliko jeshi la taifa lolote duniani including Marekani!
Duuh... unanikumbusha mbali na story hizo, kuna moja hiyo Muhammed Ali aliwahi kupigana na world champ mmoja huyo ni noomer unaambiwa, ikabidi jamaa afungwe mkono wa kushoto kwa kamba mgongoni, that was the only way to get the fight deal going, halafu jamaa alipoanza kuelemewa kocha wake akaita leeeeft! jamaa akakata kamba unaambiwa, basi ile uuuu wuuuup! ....Muhammed Ali kainama, holaaa!... jamaa kapiga mlingoti wa ulingo, mlingoti ukapinda unaambiwa.... na ngumi zikamalizwa hapo hapo...!

Ndio story hizi za Israel zina fall kwenye category hiyo hiyo, ila kuna watu wazima bado hawajazishtukia mpaka leo.
 

Weka source zako hapo.
 
Weka source zako hapo.

hebu nenda kawaombe radhi raia wa afghanistani, taifa kubwa gani linaua raia badala ya kupambana na wanajeshi!

ps. kuna mada humu jf inakusubiri inayoonesha kuwa marekani ni namba tatu kwa jeshi nyuma ya mchina na mrusi.
 
hebu nenda kawaombe radhi raia wa afghanistani, taifa kubwa gani linaua raia badala ya kupambana na wanajeshi!

ps. kuna mada humu jf inakusubiri inayoonesha kuwa marekani ni namba tatu kwa jeshi nyuma ya mchina na mrusi.

Hiyo youtube video ni propaganda tu. Kama kweli Wachina wako juu wajaribu kuiteka Taiwan waone.
 
kama hii thread angeanzisha mtu anaefahamika kuwa ni muislam
basi kusingekuwa na point zoote zilizopo zaidi ya matusi tu kwa dini na kukashfiana
but kwa kuwa NN anajulikana sio muislam
ameweza kuongea kitu ambacho kiko wazi na watu wameshindwa kwa hoja
Israel haina lolote.....bila Marekani....
 

There you go big Bossman!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…