Israel imepata hasara ya trilioni 5 za kitanzania katika vita vya Gaza

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,083
18,177
Israel imepata hasara ya zaidi ya dola bilioni 2 sawa na trilioni 5 za kitanzania katika vya Gaza

Vita vya siku 12 vya utawala haramu wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza vimesababisha hasara kubwa ya kiuchumi hasa kwa Israel.

Kwa mujibu wa taarifa vita hivyo vimesababisha pia hasara kubwa kwa Wapalestina katika Ukanda wa Gaza.

Maafisa wa Gaza wanasema zaidi ya nyumba 1,447 zimeharibiwa kikamilifu katika vita hivyo huku nyumba zingine 13,000 zikiwa zinahitajia ukarabati. Halikadhalika wakuu wa Gaza wanasema utawala katili wa Israel ulilenga kwa makusudi miundomsingi na maeneo ya kutoa huduma kwa umma na hivyo kusababisha hasara kubwa katika mtandao wa kusambaza majisafi na barabara.

Raed al Jarrar Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Uchumi huko Gaza amesema viwanda 50 vimeharibiwa katika hujuma ya siku 12 ya Israel katika eneo hilo. Amekadiria kuwa Gaza imepata hasara ya dola milioni 322 katika hujuma ya kinyama ya utawala dhalimu wa Israel.

Katika upande wa pili, kufuatia oparesheni za ulipizaji kisasi za wanamapambano wa Kiislamu wa Gaza ambazo zimetekelezwa kwa kutumi makombora, utawala haramu wa Israel umepata hasara kubwa.

Mohammed Abu al-Rezzaq" ameandika katika jarida la Al-Khaleej Online kuwa, utawala wa Kizayuni wa Israel umepata hasara kubwa kutokana kushambuliwa vituo vyake muhimu huku sarafu ya utawala huo ikiporomoka.

Wizara ya Fedha ya utawala haramu wa Israel imekadiria kuwa, utawala huo umepata hasara ya zaidi ya dola bilioni 2.

Hali Tel Aviv baada ya kombora la wanamapambano wa Palestina kutua

Mbali na hayo utawala wa Israel umepata hasara kubwa ya muda mrefu kwani idadi kubwa ya wawekezaji wa kigeni sasa wataondoka kutokana na kukosa dhamana ya usalama. Asilimia 17 ya viwanda kusini mwa Israel na Tel Aviv vimefungwa kutokana na hofu ya makombora ya Wapalestina.

Weledi wa mambo wanasema hasara ya vita hivyo ni kubwa na itabainika kadiri siku zinavyosonga mbele.

Uchumi wa utawala haramu wa Israel ulikuwa umekadiriwa kustawi kwa aislimia 6.3 mwaka huu wa 2021 lakini sasa hilo haliwezi kufikiwa kutokana na hasara ambayo utawala huo umepata kutoka kwa wanamapambano wa Palestina katika vita vya Gaza.
 
Vita vina gharama, vipi Gaza je??
Hakika..

Nahisi Gaza itakuwa double kwa sabbu wenyewe walituma makombora yenye idadi kubwa + kuharibiwa miundombinu na waIsraeli.

Ila taarifa ndio mwarobaini wa hili
 
Back
Top Bottom