Israel ilipokutana na SAMs za Kirusi

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,889
Juzi kati nimemaliza kusoma kitabu kuhusu Yom kuppur war. Baada ya kipigo kikali cha mwaka 1967 wamisri wakakaa na kujitafakari. wakagundua nguvu kubwa ya Israel ipo kwenye jeshi lao la anga na kwakiasi Armored corps(jeshi la vifaru). Kwahiyo wakatafuta mbinu za kudeal na hizi ishu mbili. Kwenye vifaru wakaagiza ant tank missiles kwa wingi sana kutoka Urusi.

Hizi pamoja na RPGs walipewa wanajeshi wa miguu na zilipiga vifaru vingi sana hadi wayahudi wakashangaa. Karibu vifaru 800. Kulinda anga wakaagiz Surface to air missile(SAM6) kutoka Urusi. jeshi la Israel lilikuwa na na ndege kama 270. Kati ya hizo karibu 100 zilidunguliwa na SAMM za waarabu. Waisrael wanategemea sana jeshi la anga hivyo hizo SAM zilikuwa bonge la kitisho. Bila ya uzembe wa waarabu kwenye dog fight ile vita ingeweza kuwa na matokeo mabaya sana kwa Israel.Vita iliisha kwa suluhu japo wayahhudi walikuwa wanaelekea kushinda.

Baada ya vita wayahudi wakaanzishaa mkakati wa kuzishinda SAM za mrusi. Mwaka 1982 kwenye vita ya Lebanon wakakutana nazo. Kwa kutumia mbinu complex wakaziharibu 29 kati ya 30 bila kupoteza ndege hata moja. Ikawa zamu ya wasoviet kuchanganyikiwa maana ulinzi wa anga lao ulitegemea hizi. Wakatuma watu kuona kilichotokeaa. NATO nao wakaenda kujifunza kilichotokea, wakati wa kufunga anga la Libya Gaddafi akatumia S6, hakupiga hata ndege moja.

Hizo S6 zilikuwa na range ya 6miles ,Leo Urusi wana S-400 zenye range ya 400m, zinapiga hadi ballistic missiles. US alimmind Turkey kwa kutaka kununua hizi, India naye alipigwa mkwara. Nafikiri enzi za kuwa na air superiority zinaelekea mwisho.
 
Kwa namna Israel ilivoongelewa kwa miaka na vizazi vingi huenda Kuna kitu zaidi ya maneno yaliyosemwa
"wako tofauti?",
mbona kataifa kadogo kama mkoa wa Rukwa kanazungumzwa Sana?
Ukiondoa yanayosemwa kwenye maandiko juu yao, Kuna kingine kipya kinachowabeba kiuwezo kiasi kwamba wawe Taifa la kuangaliwa na kuigwa Sana?
 
Kwa namna Israel ilivoongelewa kwa miaka na vizazi vingi huenda Kuna kitu zaidi ya maneno yaliyosemwa
"wako tofauti?",
mbona kataifa kadogo kama mkoa wa Rukwa kanazungumzwa Sana?
Ukiondoa yanayosemwa kwenye maandiko juu yao, Kuna kingine kipya kinachowabeba kiuwezo kiasi kwamba wawe Taifa la kuangaliwa na kuigwa Sana?
Vita ya sasa ni teknolojia,Israel rafiki zake ni watu wenye maendeleo makubwa kwenye teknolojia
 
Hizo Ant tank missiles wanaita SAGA vidogo lakini mtikisiko wake waisrael walirudi kudefence kwa mara ya kwanza
 
Urafiki hugharimiwa na maslahi ya vitu, udugu na utegemezi, je mbona hawakorofishani, (considering democratic governments led by different sides of leaning),
Vita ya sasa ni teknolojia,Israel rafiki zake ni watu wenye maendeleo makubwa kwenye teknolojia
 
Back
Top Bottom