Nuclear missile haina haja. Tufanye assumptions kwamba Israel wamekuwa vilaza wakadondosha nuclear missile. Unasema ni miniature warhead, sio? Tungepata matokeo yafuatayo machache yake ni:
1. Radioactive fallout. Hakuna technology yoyote ile duniani ya kutenganisha nuclear warhead na radioactivity, na haitokaaa itokee. Hii ni sawa na kutenganisha damu na Haemoglobin, ukishaondoa HB damu inakuwa fluid au jina lingine. Nuclear inatengenezwa na radioactive materials tu ambazo lazima zionekane baada ya shambulizi au hata ajari. Kwenye hili tukio, vipimo havijaonesha mionzi.
2. Electromagnetic pulse. Hii inasababisha vifaa vyote vya electronic kama simu, saa, TV, radio, stations mbalimbali, etc kuzima kutokana na nguvu ya atomiki. Baada ya tukio na wakati wa tukio uliona video zinarekodiwaa na simu zilipigwa.
3. Mushroom crowd ambayo inadumu dakika nyingi angani. Tafuta video za Tsar bomba (most powerful nuclear detonation) kule Soviet Union au tafuta video za testing kule Nevada desert, USA. Crowd inakaa sana, hapa hatukuona mushrooms crowd hata kwa sekunde kumi.
4. Nuclear epicenter (ground zero). Ingetokea shimo kubwa kabisa lililotokana na explosion. Tafuta hata video ya drill za Iskander tactical missile za Russian military uone mlipuko wa zile conventional warhead zinavyochimba shimbo la zaidi ya mita 15 upana na mita 8 kimo. Hapa unayosema nuclear hakuna hata kashimo kakugicha kuku.
Hata lile jengo lefu lililoonekana mlipuko unaanza lilibaki sasa sijui nuclear yako ni ya kizembe kiasi gani.
View attachment 1529279View attachment 1529280