Ismail Jussa: Chama Mbadala kimoja kikubwa kukusanya vipaji vyote kutoka vyama vyote makini na makundi ya kijamii na kisha...

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,014
144,372
Hizi hapa chini ni tweet mbili moja katika lugha ya kiswahili na nyingine katika lugha ya kingereza alizoziandika Ismail Jussa katika mtandao wa twitter:

"Chama Mbadala kimoja KIKUBWA kukusanya pamoja vipaji vyote kutoka vyama vyote makini na makundi ya kijamii na kisha kufuatiwa na....."

"One super alternative PARTY bringing together all the cream from all serious parties and from civil society organisations and then follows...."

Tweet hizo mbili katika akaunti yake hiyo ya twitter kaziambatanisha na picha ya pamoja ya viongozi wa umoja wa UKAWA,picha ya pamoja ya Lowassa, Mbowe na Maalim Seif, picha ya pamoja ya Maalim Seif na Zitto na picha nyingine ya pamoja ya Lissu na kiongozi mmoja wa CUF.

My take:
Hii ni hatua nzuri sana na ya kupongeza kwa upinzani katika kukabiliana na CCM ila wajiandae na hujuma za hawa jamaa kwa kutumia dola na ushawishi wa "fwedha" kuwavuruga katika jitihada zao za kuunda hicho chama kimoja kikubwa.

Pia, hatua hii ya upinzani ni ujumbe tosha kuwa Magu anawafanya wapinzani wawe wamoja zaidi (anaimarisha upinzani) na kuwafanya wawe wabunifu zaidi katika kukabiliana na mabavu ya CCM.

Tutafikaa tu.
 
Kwasasa hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo.

Kila mtu akipigana kivyake hakuna atayemshinda muovu CCM. Lakini wazalendo wa kweli na wapenda maendeleo wakiungana hakika CCM itaangukia pua.

Sio leo sio kesho lakini hakika nakuambia watesi wataaibika mchana kweupe.
Huu ndio ukweli na wakishirikisha watu kutoka taasisi zingine za kijamii itawaongezea support kubwa sana.
 
Hii ndio strategy niliyokuwa nikiingojea siku zote. Fight, fight fight and then fight.
Hizi hapa chini ni tweet mbili moja katika lugha ya kiswahili na nyingine katika lugha ya kingereza alizoziandika Ismail Jussa katika mtandao wa twitter:

"Chama Mbadala kimoja KIKUBWA kukusanya pamoja vipaji vyote kutoka vyama vyote makini na makundi ya kijamii na kisha kufuatiwa na....."

"One super alternative PARTY bringing together all the cream from all serious parties and from civil society organisations and then follows...."

Tweet hizo mbili katika akaunti yake hiyo ya twitter kaziambatanisha na picha ya pamoja ya viongozi wa umoja wa UKAWA,picha ya pamoja ya Lowassa, Mbowe na Maalim Seif, picha ya pamoja ya Maalim Seif na Zitto na picha nyingine ya pamoja ya Lissu na kiongozi mmoja wa CUF.

My take:
Hii ni hatua nzuri sana na ya kupongeza kwa upinzani katika kukabiliana na CCM ila wajiandae na hujuma za hawa jamaa kwa kutumia dola na ushawishi wa "fwedha" kuwavuruga katika jitihada zao za kuunda hicho chama kimoja kikubwa.

Pia, hatua hii ya upinzani ni ujumbe tosha kuwa Magu anawafanya wapinzani wawe wamoja zaidi (anaimarisha upinzani) na kuwafanya wawe wabunifu zaidi katika kukabiliana na mabavu ya CCM.

Tutafikaa tu.
 
Tatizo sio support. Upinzani unaungwa mkono na wananchi wengi, lkn mambo hayaendi. Mfano, zenji wananchi huwa wanachagua upinzani lkn akina jecha wanachagua sisiemu. Ukitumia njia ileile uliyotumia miaka yote utaendelea kupata matokeo yaleyale. Wapinzani wakitambua kuwa dawa ya moto siyo maji ndo mambo yatabadilika
 
Hilo wanalijua, na kupitia umoja huu, bila shaka watashirikiana kulipigania.
 
Huu ni mkakati mzuri wakupongezwa. Andaeni utaratibu mzuri wa umoja wa kitaifa utakao fufua matumaini kwa wananchi juu ya uimara ndani ya umoja wenu.
 
Hilo wanalijua, na kupitia umoja huu, bila shaka watashirikiana kulipigania.
Salary Slip sioni umoja wowote ndani ya wapinzani. Siamini kama Wapinzani wamewahi kujifunza na kuwa na umoja kwa nia thabiti. Wapinzani hawajaanza leo kuungana, walianza zamani hizo. Kumbuka wakati wa vuguvugu la vyama vingi wanaharakati wa bara walikuwa na NCCR na kule Zanzibar wakawa na KAMAHURU. Baadaye hao wakaungana na CCW cha Mzee Mapalala, lakini kwa uroho wa Maalim, Mapalala akaenguliwa toka chamani!

Sijui kama ulikuwepo na unafahamu nini kilitokea. Wapinzani wakaja wakaungana tena kwenye umoja fulani hivi nao haukufanya kazi. Wapinzani wakasema waachiane majimbo nayo ikawa shida wakati huo. Wakati wa bunge la Katiba tukaona wapinzani wakijumuika pamoja na UKAWA na wakaenda nayo hadi uchaguzi wa 2015; hii nayo haikufanya kazi kama ilivyotegemewa kwa sababu wa uroho na ulafi wa CHADEMA (kwa hili naamini Mtatiro hawezi wasamehe CHADEMA). Baada ya uchaguzi huo, UKAWA imekuwa al marhumu!

Kwa lugha nyepesi wapinzani ni waroho na hawawezi kuungana kwa tija; hayo ya Jusa ni maneno matupu! Hakuna ambaye atakubali kupoteza Chama chake ili kuunda umoja. Kwa mujibu wa sheria mkitaka kuwa na umoja wa vyama wenye nguvu za kisheria inabidi muue vyama vyenu ili kuunda chama kipya; Mbowe atakubali kuua CHADEMA?
 
Safi sana viongozi wetu.
Kikubwa watambue sisi wananchi bado tuko nao tunaunga mkono juhudi za raisi ila tukiwa hukuhuku.
Upinzani upo mioyoni mwa wananchi sio kwa wale viongozi uchwara walafi wa pesa ma madaraka wasaliti wakubwa.
Watafanikiwa kiwanunua wabunge ila hawatofanikiwa kutununua wananchi mpaka kufikia kubadilisha itikadi zetu.
 
Salary Slip sioni umoja wowote ndani ya wapinzani. Siamini kama Wapinzani wamewahi kujifunza na kuwa na umoja kwa nia thabiti. Wapinzani hawajaanza leo kuungana, walianza zamani hizo. Kumbuka wakati wa vuguvugu la vyama vingi wanaharakati wa bara walikuwa na NCCR na kule Zanzibar wakawa na KAMAHURU. Baadaye hao wakaungana na CCW cha Mzee Mapalala, lakini kwa uroho wa Maalim, Mapalala akaenguliwa toka chamani!

Sijui kama ulikuwepo na unafahamu nini kilitokea. Wapinzani wakaja wakaungana tena kwenye umoja fulani hivi nao haukufanya kazi. Wapinzani wakasema waachiane majimbo nayo ikawa shida wakati huo. Wakati wa bunge la Katiba tukaona wapinzani wakijumuika pamoja na UKAWA na wakaenda nayo hadi uchaguzi wa 2015; hii nayo haikufanya kazi kama ilivyotegemewa kwa sababu wa uroho na ulafi wa CHADEMA (kwa hili naamini Mtatiro hawezi wasamehe CHADEMA). Baada ya uchaguzi huo, UKAWA imekuwa al marhumu!

Kwa lugha nyepesi wapinzani ni waroho na hawawezi kuungana kwa tija; hayo ya Jusa ni maneno matupu! Hakuna ambaye atakubali kupoteza Chama chake ili kuunda umoja. Kwa mujibu wa sheria mkitaka kuwa na umoja wa vyama wenye nguvu za kisheria inabidi muue vyama vyenu ili kuunda chama kipya; Mbowe atakubali kuua CHADEMA?
Ndo wameamua hivyo mkuu,subiri matokeo
 
Hizi ni ndoto za mashabiki ila viongozi wa upinzani hawawezi kukubali kupoteza mamlaka hata madogo waliyonayo, kumwambia Mbowe na genge lake la kina John Mrema waje kukubali kugawana ruzuku na CUF na ACT ndani ya chama kimoja ni ndoto ya mchana.
We ndo unaota kuwa haiwezekani , subiri matokeo.
 
Hizi ni ndoto za mashabiki ila viongozi wa upinzani hawawezi kukubali kupoteza mamlaka hata madogo waliyonayo, kumwambia Mbowe na genge lake la kina John Mrema waje kukubali kugawana ruzuku na CUF na ACT ndani ya chama kimoja ni ndoto ya mchana.
Ni mapambano ndugu, likishindikana hili litazaliwa jengine tu... muhimu mapambano yanaendelea na hamuwezi kutukatisha tamaa. Kwa hapa tulipofikia msitegemee kama watanzania watasarenda. Alutacontinua!
 
mi naomba tu hivyo vyama super power vinavyojaziwa hio cream vielewe tu kuwa hii nchi haendeshwi kwa misingi ya kisheria,kwa hio hizo strategy zao lazima zije kuwa na nguvu za kulazimisha utawala wa sheria na tume huru ya uchaguzi,bila ya hivyo basi hata tukaunganisha na vyama super power vya kenya na uganda hakuna kitachokuwa hapa.
watu wazima lazima wawe na uelewa wa kuona hali halisi na kuitathmini hali ilivyo,isiwe mambo ya kutuharibu akili kwa mashindano ya kisiasa yasiyozaa matunda,miaka 30 sasa tuanpigishana kelele na watawala hata huo mfumo halisi wa vyama vingi haujapatikana hapa.
 
Salary Slip sioni umoja wowote ndani ya wapinzani. Siamini kama Wapinzani wamewahi kujifunza na kuwa na umoja kwa nia thabiti. Wapinzani hawajaanza leo kuungana, walianza zamani hizo. Kumbuka wakati wa vuguvugu la vyama vingi wanaharakati wa bara walikuwa na NCCR na kule Zanzibar wakawa na KAMAHURU. Baadaye hao wakaungana na CCW cha Mzee Mapalala, lakini kwa uroho wa Maalim, Mapalala akaenguliwa toka chamani!

Sijui kama ulikuwepo na unafahamu nini kilitokea. Wapinzani wakaja wakaungana tena kwenye umoja fulani hivi nao haukufanya kazi. Wapinzani wakasema waachiane majimbo nayo ikawa shida wakati huo. Wakati wa bunge la Katiba tukaona wapinzani wakijumuika pamoja na UKAWA na wakaenda nayo hadi uchaguzi wa 2015; hii nayo haikufanya kazi kama ilivyotegemewa kwa sababu wa uroho na ulafi wa CHADEMA (kwa hili naamini Mtatiro hawezi wasamehe CHADEMA). Baada ya uchaguzi huo, UKAWA imekuwa al marhumu!

Kwa lugha nyepesi wapinzani ni waroho na hawawezi kuungana kwa tija; hayo ya Jusa ni maneno matupu! Hakuna ambaye atakubali kupoteza Chama chake ili kuunda umoja. Kwa mujibu wa sheria mkitaka kuwa na umoja wa vyama wenye nguvu za kisheria inabidi muue vyama vyenu ili kuunda chama kipya; Mbowe atakubali kuua CHADEMA?
Jiti la Mbowe naona linakuuma bado
 
Hizi ni ndoto za mashabiki ila viongozi wa upinzani hawawezi kukubali kupoteza mamlaka hata madogo waliyonayo, kumwambia Mbowe na genge lake la kina John Mrema waje kukubali kugawana ruzuku na CUF na ACT ndani ya chama kimoja ni ndoto ya mchana.
Mbowe ameshughulikia wengi. .inaonekana jamaa mtamu sana hamwishi kumtaja huku mkibana pua
 
Back
Top Bottom