GodfreyTajiri
JF-Expert Member
- Sep 26, 2010
- 1,006
- 712
Uwezo wa Mungu ni mkubwa, unaweza pata msaada kutoka sehemu usiyotegemea kabisa ukatatua tatizo. Kumbe huyo aliyetoa msaada ameongozwa na Mungu aje akusaidie.Mfano uko hospitalini unatakiwa ufanyiwe oparesheni ya jicho na kuna kiasi fulani cha fedha kinahitajika, unaeleza tatizo lako usaidiwe; matokeo yake wanakuambia Mungu atakusaidia utapona. Sasa ataponaje bila kupata matibabu?
Binadamu wanachangamoto kweli, unamweleza shida zako ukifikiri atakusaidia ata kwa mchango kidogo; matokeo yake wanakushauri Mungu atakusaidia.
Sasa mtu ana njaa, hitaji lake kwa sasa ni chakula; sasa hapo Mungu atamsaidiaje, badala ya wewe kumuwezesha kula? Urafiki ni kutatua kero iliyopo, na si kuhamisha majukumu kwa muumba.
Hii kuhamisha majukumu ni dalili ya uchoyo.
Aliyeshiba ndio hupata nguvu ya kuomba, hujala siku 2 hiyo nguvu ya kuomba utaipata wapi?Uwezo wa Mungu ni mkubwa, unaweza pata msaada kutoka sehemu usiyotegemea kabisa ukatatua tatizo. Kumbe huyo aliyetoa msaada ameongozwa na Mungu aje akusaidie.
Nakubaliana na wewe 👆, kwa hiyo usimueleze mtu matatizo yako ambaye hawezi kukusaidiamaana yy hana uwezo wa kukusaidia
Watu tunajuana hali zetu za kiuchumi, kuna mwngne unaona tu hana uwezo wa kukusaidia hata ukimuomba......lkn hii haimaanish usmuombe maana huez jua anaweza kukusaidia hata kmawazo tu.Nakubaliana na wewe 👆, kwa hiyo usimueleze mtu matatizo yako ambaye hawezi kukusaidia
Si bora nijisemee mimi mwenyewe kuwa atanisaidiaKwa hiyo hauamini kwamba Mungu atakusaidia? Kukufariji hivyo ni msaada tosha! Jifunze kuwa na shukrani
Haukuweza kujisemea sasa ndiyo maana amesaidia kukumbushia.Hata kama ungeweza kujisemea sio vibaya akakumbushia maana ni jambo jema.Jifunze kuwa na shukraniSi bora nijisemee mimi mwenyewe kuwa atanisaidia
Shukrani kwa kupata maneno matupu haisaidii mkuuHaukuweza kujisemea sasa ndiyo maana amesaidia kukumbushia.Hata kama ungeweza kujisemea sio vibaya akakumbushia maana ni jambo jema.Jifunze kuwa na shukrani
Kukukumbusha kwamba Mungu atakusaidia ni maneno matupu?Shukrani kwa kupata maneno matupu haisaidii mkuu
Ndio maana hata kwenye nyumba za ibada tunatoa hela na hawapokei maneno matupuKukukumbusha kwamba Mungu atakusaidia ni maneno matupu?