Isemavyo katiba na sheria kuhusu uchaguzi Zanzibar

kwamwewe

JF-Expert Member
Jul 15, 2010
1,801
541

Msikilize mwanasheria bingwa na aliyebobea ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, akielezea uvunjwaji wa Katiba uliofanywa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salim Jecha, kwamba uchaguzi wa Zanzibar wa tarehe 25 Oktoba, 2015 bado ni HALALI na pia kufafanua kwamba tamko BATILI la Jecha kuchapishwa kwenye Gazeti Rasmi la Serikali hakulipi uhalali wala kupunguza UBATILI wa tamko hilo.




 
Last edited by a moderator:
Mbona inajulikana wazi na kila mtu kwa sasa kuwa hlo tamko la Jecha hakulitoa kwa kufuata Ibara yoyote ya Katiba ya Zanzibar wala kifungu chochote cha sheria ya Zanzibar Electoral Commission Act, bali ilikuwa ni 'amri' aliyopewa kuitekeleza na viongozi wahafidhina ndani ya CCM.
Hata hivyo kwa kuwa viongozi hao waandamizi wamejivika kuwa above law hapa nchini, ndiyo maana pamoja na kulitumbukiza Taifa letu katika sintofahamu kubwa kutokana na agizo lao hilo kutekelezwa na Jecha, lakini hatutashuhudia kukiona chombo chochote cha dola kikiwatia mbaroni watu hao na kuwafungulia mashitaka, kwa kuwa watu hao wanaiona nchi hii kama mali yao binafsi na wanaamini Mwenyezi Mungu amewapa wao hati miliki ya kuitawala nchi hii hadi mwisho wa dunia!
 
Kwa wale viongozi wa CCM wanaoliunga mkono kwa asilimia 100 tamko hilo la Jecha la kufuta uchaguzi wa Zanzibar, tunawaomba basi wajitokeze humu jamvini na watwambie ni Ibara ipi ndani ya Katiba ya Zanzibar na vifungu vipi vya sheria ndani ya Zanzibar Electoral Commission vinavyompa mamlaka Jecha kufanya yale aliyoyafanya hapo tarehe 28/10/2015.
Naweza kukifananisha kitendo alichofanya Jecha kuwa hakina tofauti hata kidogo na kitendo alichofanya Kivuitu mwaka 2007 kule Kenya ambacho kiliisababishia nchi hiyo iingie kwenye machafuko makubwa ambayo yalisababisha vifo vya maelfu ya wakenya.
 
humphray Polepole licha ya kutokujua sheria yeye ndio mnazi namba moja kitetea upumb.abu wa jecha
 
Last edited by a moderator:
12240122_968008546600811_4822772123703526618_n.jpg
 
Hivi ni kwanini haijafunguliwa kesi yoyote kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar?
 
Hivi ni kwanini haijafunguliwa kesi yoyote kuhusiana na uchaguzi wa Zanzibar?


UTAIFUNGUA KWENYE MAHAKAMA IPI ??? TANZANIA HAKUNA MAHAKAMA HURU


MAJAJI NDIO HAO AKINA LUBUVA CCM



Unapeleka kesi ya tumbiri kwa nyani ???

ZAnzibar , Mahakimu ndio hao akina Mbwezeleni , mafia wakubwa wa CCM
 
Shoo Gap ,

msikilize Dada Fatma Karume anasema nini


 
Last edited by a moderator:
UTAIFUNGUA KWENYE MAHAKAMA IPI ??? TANZANIA HAKUNA MAHAKAMA HURU


MAJAJI NDIO HAO AKINA LUBUVA CCM



Unapeleka kesi ya tumbiri kwa nyani ???

ZAnzibar , Mahakimu ndio hao akina Mbwezeleni , mafia wakubwa wa CCM

Kwa hiyo mkuu, hakuna chombo hata kimoja kinachoaminiwa na Wapinzani? Tume ya Uchaguzi, Polisi, Mahakama n.k. HII NI HATARI. Haki sawa kwa wote inapatikanaje sasa?
 
Back
Top Bottom