ISACK AMTWANGA MCHINA

Mwasongola

Senior Member
Joined
Aug 8, 2018
Posts
149
Reaction score
109
MTANZANIA ATAMBA KATIKA KICK BOXING NCHINI CHINA, AMTWANGA MCHINA KWA KNOCK OUT

Mwanafunzi Mtanzania anayesoma nchini China Isaack Ibrahim Emmanuel juzi ameibuka kidedea katika mchezo wa kick boxing baada ya kumpiga kwa KO Mchina Zi xiǎo yún yǔ katika Mjini Jillin.


Isaack, ambaye anasomea uhandisi wa Madawa (Pharmaceuticals engineering) katika Chuo Kikuu cha Liaoning jijini Shenyang, ameushangaza umati mkubwa wa Wachina baada ya kucheza kwa ustadi na hatimaye kumgaragaza Zi ambaye hajawahi kupigwa hata mara moja.


Mpambano huo wa Kg 60 umempa umaarufu mkubwa Isaack kiasi kwamba hata waandaaji wa mapambano wameanza kupigana vikumbo kumtaka acheze mapambano zaidi. Akiwa na uwezo wa kutumia kwa kasi ya ajabu miguu na mikono yote, wataalamu wa mchezo huo wamemtabiria makubwa kijana huyu wa kutoka Mwanza.

Akiongea na michuzi tv kwa njia ya mtandao, Isaack amesema yuko fiti kupambana na yeyote na popote huku akiendea na Masomo bila wasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
HIVI ALIPATA KIBALI CHA KUCHEZA PAMBANO KUTOKA BONGO?

MAANA BAADAYE UTASIKIA KUPITIA RAIS WA NDONDI, Oooh huyu kijana ....!, Ooooh tutampa bend....., AU Atakuwa chini ya md....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…