Kimsingi Jumuiya ya Commonwealth wanakuwa na watu wao wa kuangalia mwendendo wa upigaji kura kwa kila nchi mwanachama. Kwa hiyo basi, iwapo kulikuwa na kasoro za kiuchaguzi katika upigaji kura nchini Kenya basi jamaa wale waliokuwa wametumwa na commonwealth lazima waandike kitu cha namna hiyo katika taarifa zao kwa wale waliowatuma. Iwapo wataandika taarifa chafu, basi Kibaki ana la kujibu kwa uongozi wa Jumuiya.
Na iwapo Kibaki atatangaza ali ya hatari kwa nchi yake, kutokana na vurugu zinazoendelea, basi maamuzi ya commonwealth ni kumchukulia hatua za kinidhamu kama vile walivyofanya kwa Mussharaf wa Pakistan. Hio ndio hali halisi.
Ila binafsi nasikitika sana kuona ndugu zangu na jirani zangu wa Kenya wamefikia hatua ya namna hii, watu kuuwawa, nyumba kuchomwa moto na uporaji uliokithiri.
Mungu awaepushe wasiingie katika vita ya wenyewe kwa wenyewe! Nisingependa hili litokee, kwani kurudi katika amani waliyokuwa wameizoea itakuwa ngumu sana kama wataingia vitani.
Lakini pia ikumbukwe kwamba ni Wakenya hawahawa waliomuondoa Muingereza kwa vita ya Maumau, kwa hiyo huenda hawajasahau mbinu zao, ndio uoga wangu hasa ulipo iwapo wataamua ku dela na Kibaki kwa namna hii!