Is she responsible?????

Prince Nadheem

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2012
Posts
1,270
Reaction score
1,111
Habari za jumapili wanajamvi?? kwa upande wangu mie iko pouwa namshukuru muumba kwa hilo. kubwa nalowasilisha siku ya leo ni kuwa hapa mitaa ya home kuna jirani yangu mmoja ana mke na mtoto 1. Sasa imetokea tu kwamba huyo mke wa jamaa yangu kamzoea sana mke wangu kiasi ambacho hata kama anaenda dukani huwa anamuacha mwanae kwa mke wangu.
Hiyo sio ishu saaaana ila sasa amekuwa na tabia ya kuja kushinda kwangu saana hasa kupiga stori na my wife za hapa na pale na mie mara nyingi akija huwa nawaacha wao wawili. kinachoanzanikera sasa hivi anakuja na mwanae hana nepi wala chupi ya mkojo halafu anamuweka kwenye sofa zangu,basi naam zinakojolewa kama mie ndio nina kichanga kumbe sie hata kichanga hatuna. ukimwambia mbona mtoto havalishwi nepi utasikia "tumemuacha hivyo ili apumue ila tukiwa tunaenda kwa watu tunamvalisha." sasa hapo mie ndio huwa najiuliza kama sie ni ngedere au? mtoto mwenyewe anakuwa ni mchafu muda wote kiasi ambacho hata mtu kumshika waona tabu unabaki kucheza nae upo miles away!
Kali ya leo ni kuwa jana nimerudi kutoka safari ya kikazi na niliingia kama saa tano usiku so nilikuwa na uchovu wa hatari. nimelala hadi saa nne unusu hivi ila ile kuamka tu namsikia yupo sitting room kwangu na mke wangu kama kawa. sasa hadi muda huu yupo kwangu ni saa nane kasoro sasa mie nipo room sijatoka nae bado yupo tu hata dalili siioni ya kutoka.
Sasa najiuliza maswali kuwa leo ni jumapili na mumewe yupo home,je chai alimuandalia/wamekunywa saa ngapi?? shughuli zingine za ndani kamaliza saa ngapi?? nani anampa company mumewe huko ndani?? Je na maandalizi ya lunch yanaendaje? Is she a reponsible woman?? je wakiwa na watoto zaidi ya huyo mmoja atakuw aje?? she's really absurd.:confused2::confused2::confused2::confused2:



:confused2:
 
si mmwambie live. kama vipi mpangieni muda wa kuja hapo..(naona anakuja kuangalia kideo). jirani atakunyimaje raha kwako. halafu naona mkeo ndo anamfuga.
 
Mpeni live au wife atafute njia ya kumkwepa, mbali na kuleta mwanae mchafu huyo anadalili ya kuleta umbea, yasubiri yanakuja.
 
mke wako angemwambia huyo mama kistaarabu.wamama wengine sio wastaarabu,ukienda kwa mwenzio,mume wake akija tu inatakiwa uondoke uwape nafasi mume na mke.lakini wengine hata mume akiwepo na yeye yupo,haipendezi.hayo maongezi, maongezi gani ya kila siku?
 
hapo kuna la zaidi .... ila mkuu inaonekana wewe ni muoga sana kama walivyowatanzania wengi ,,,, yaani unashindwa kumwambia ukweli?
 
Kwa nini wife wako anakuwa na mazoea ya kupitiliza kihiivyo na huyo jirani?? Dawa ni kuongea na mkeo aanze kumuepuka...ipo siku utakuta amejilaza chumbani kitandani kwako .....
 


tena mtu mwenyewe ametoka safari.... mbona ningemchukua my wife chumbani nikamgegede kwa raha zangu.
 
Kwa nini wife wako anakuwa na mazoea ya kupitiliza kihiivyo na huyo jirani?? Dawa ni kuongea na mkeo aanze kumuepuka...ipo siku utakuta amejilaza chumbani kitandani kwako .....


hapo ndiyo jamaa atajua hiyo ni zaidi ya story tu...

nb; mkuu hiyo signature yako imenifurahisha...... kwa hisani ya Mtambuzi
 
Last edited by a moderator:
Kuna ka mpango wife wako anacho na huyo mama dats why zinaiva sana ako kaishu kanahusika na kutunziana siri so anza na mkeo kumuuliza u special wa huyo shosti wake kung'ang'ania kwako hivyo.
 
mkuu nakushangaa sana....yaani hiyo mikojo mnaichekea tu? Si mmwambie?

Pili mkeo nae ana tatizo....badala ya kuitumia wikiend na mumewe anaitumia na shosti?

Khaaaa mi ningembalasa
 
mkuu nakushangaa sana....yaani hiyo mikojo mnaichekea tu? Si mmwambie?

Pili mkeo nae ana tatizo....badala ya kuitumia wikiend na mumewe anaitumia na shosti?

Khaaaa mi ningembalasa

Nikiwa nasoma story ya huyu kaka nilidhani anaulizia kama mkewe ni responsible au vipi, kumbe anaulizia mke wa mwenzie!
Kaka, mtu wa kwanza ambaye siyo responsible ni mkeo. Kama huyo ni rafiki yake hawezi kumchekea tu wakati mtoto anaharibu nyumba yake, huko ni kutokuwa responsible.
Pia huyo mkeo sijui ana shida gani. Yaani mume katoka safari, leo mapumziko, hamna mtoto, mume bado kalala yeye yupo nje na shosti...... Wanaongea nini ambacho ni muhimu kuliko kulala na husband? Huko nje anafanya nini cha maana? Jiulize kwanza haya
 
mkuu nakushangaa sana....yaani hiyo mikojo mnaichekea tu? Si mmwambie?

Pili mkeo nae ana tatizo....badala ya kuitumia wikiend na mumewe anaitumia na shosti?

Khaaaa mi ningembalasa

sasa mkuu mie naamka ndio nakuta hali kama hiyo kuwa mtu ndio kaja hiyo asubuhi kabla hata mie sijaamka,kuhusu suala la mkojo nilmwambia wife kuwa ampokee mtot then awe amweke chini ((kwenye kapeti); Ila very soon nampiga ban kabisa kwani urafiki wangu na mumewe ndio iloanza so kama vp tubakie wenyewe au ufe kabisa hata wetu.
 

Dah!! mkuu FP kwa huo mtazamo wako waweza kuwa sahihi kwa kiasi fulani sa katika uzi wangu sikugusia kila aspect ya maisha yetu; kivipi basi? sie mara nyingi tumezoea around saa mbili na nusu tunakuwa macho hasa kwa wakti wa weekend ila sasa kwa leo mie uchovu ndio ulionivusha na wife nae aliamka kufanya kazi zingine za ndani na ndio hapo huyo bi dad alipokuja. kiujumla mie mke wangu hapendi sana kulala baada ya saa mbili asubuhi na pia hapendi kulala kwa kuchelewa hadi saa sita za usiku bila ya 7bu maalumu
 
ur wife must be resonsible for that matter, mwanamke gani aenda kwenye nyumba za watu asubuhi yote hiyo je usafi kafanya saa ngapi? mipangilio imemshinda sasa anataka kumharibia mkeo ili awe kama yeye, mwambie mkeo awe makini na huyo dada.
 
jamani nyumba zingine njaaa. mi naona huyu mama kwake misosi haba so anakuja kuvizia kwako. ila kukatiza inabidi uongee na mkeo kuwa mara ww urudipo home basi hata kama alikuwa anaongea nae basi yeye aje chumbani mkae huko mpaka huyo mdada achoke. ataondoka na tagundua kuwa sasa hana nafasi.
 
Ndio uswahili, ukisema utaonekana mbaya.
Mwambie mkeo ndio inabidi awe na marafiki lakini sio urafiki wa dizain hii.

Mueleweshe kuwa yeye ni mke wa mtu, haishi peke yake, kwaiyo aweke mipaka ya urafiki akufikirie na wewe.
Weka mashart unayotaka wewe na mke inabidi afuate, kila siku. Jaribu kuwa mkali
 
Wewe ni Baba mwenye mji/nyumba mwambie mkeo avunje urafiki na huyo mama asije akamwambukiza umbea na uzurulaji mkuu, kama hawezi chukua jukumu mwenyewe familia inayoharibika ni yako.
 
kwa kweli wakuu nimeongea na my wife this evening na kumwambia kuwa lazima ajue mipaka ya urafiki interms of muda na rasilimali zingine na pia nitaapply hiyo ya kuwa kama nikirudi kutoka job namwita room and we stay in there together as long as possible
 
Inaonyesha mkeo anam entertain huyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…