Is Police a running Dog?

sirjohn

JF-Expert Member
Aug 6, 2014
767
677
Kwanza kabisa niwape pole Askri wote katika nchi hii hasa wale wa Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa na ngumu wanayofanya..naposema kazi kubwa na ngumu wanayofanya nikiwa na maana Polisi wanafanya kazi katika mazingira magumu kwa maana ya uhaba wa vitendea kazi na maisha yao kwa ujumla.. hili wote tunalijua..Rais analijua na Nchemba analijua..huhitaji kufanya utafiti au kufanya ziara kuzijua shida za Polisi.


Tunajua wananunua hata uniform zao ambazo ilitakiwa wapewe bure, tunajua wana mishahara midogo, tunajua wanaishi kwenye magofu, tunajua wanalala nyumba ya chumba kimoja lakini humo kuna mama na watoto wa zaidi ya miaka 18, tunajua Polisi wakipanda vyeo huwa mishahara yao inapungua/inashuka badala ya kuongezeka, tunajua wanapanda vyeo kwa mwendo wa kinyonga! tuanjua hata wakati mwingine wakipanda vyeo huwa ni vyeo vya mabegani tu maana haviongezi unafuu katika maisha yao bali ni ongezeko la shida, taabu na majuku.

Kuna rafiki zangu wawili mmoja aliingia JWTZ na mwingine aliingia TPF na wote ni graduate na waliingia katika majeshi haya mwaka mmoja lakini wa JWTZ ni kapten kwa sasa (nyota tatu sasa ) na yule wa TPF ni A/Inspector (Mkaguzi msaidizi wa Polisi/nyota moja)..wote haya tunajua, kwa hiyo tunapo wapa pole Polisi wetu kwa kazi ngumu na kubwa wanayoifanya tunajua tunachokisema.

Kama mtakumbuka kabla ya uchaguzi mkuu 2015 Serikali iliongeza posho ya Askari wote nchini hadi kufika tsh 300,000 kwa mwezi lakini posho ile kwa Jeshi la Polisi waliipata baada ya miezi 3-4 huku wenzao wa JWTZ wakiwa wameishaipata..chanzo cha haya majeshi kuonekana hili ni bora kuliko jingine ni nyie viongozi, treatmet zenu kwao siyo sawa! hii ni kwa Magereza nk!..mnawagawa wapiganaji wetu.....

Tunaelewa walipewa posho hiyo siku chache kabla ya uchaguzi mkuu, tunajua why walipewa posho ile kwa wakati ule, na nyie mnaelewa, mimi naelewa na kila mtu anaelewa ukweli na bahati nzuri na hata rais wetu naye anaelewa ukweli wa hili jambo, hili liko wazi na hata mapolisi wanalijua hivyo. Sababu ilikuwa ni hali ya uchaguzi ilionekana kuwa ngumu kwa watawala!..yote haya tunajua..lakini kwa kuwa Polisi ni running dog huwa hawasemi wamefundishwa kukaa kimya bado walikaa kimya..


Tunaelewa na tunakumbuka na audio na vidio tunazo kipindi cha kampeni mh. Rais aliwaomba Polisi wasimamie uchaguzi vyema ili ashinde na kuwa Rais na maslahi yao atayalinda..! tunajua Polisi walifanya nini hadi uchaguzi ukapita salama, tunajua walikataa hata tusikae mita 100 baada ya kupiga kura, tunajua kuna watu wamepata mateso na shida kubwa sana kipindi cha uchaguzi kwa kupitia Jeshi letu la Polisi..hayo yote tunajua na tunaamini Jeshi la Polisi walikuwa na nia nzuri kutupitisha salama hasa kipindi cha uchaguzi na walifanikiwa! punda afe mzigo ufike....Tunasubri Mh. Rais alinde na kuboresha maslahi ya Polisi na Askari wote kwa ujumla..

Kama unataka ujue Polisi is a running dog kamuulize Kova..Kova baada ya kustaafu aliomba kurudi pale chuo cha Polisi Moshi kuwa mwalimu! ile kauli ilishangaza sana..kama kamishna mstaafu wa Polisi hata mwezi uraiani hana toka astaafu anaomba kurudi kufundisha je hawa wanaostaafu bila cheo wanakuwa na hali gani! jibu ni moja Polisi kuna tatizo lao binafsi na pia kuna tatizo wa kimfumo...Hivi nani hakumbuki mikwala ya kamanda Kova ya kuhakikisha nchi inakuwa salama hasa kipindi kile cha uchaguzi! simtetei kamanda Kova ila naona hali aliyo nayo ni ngumu mno baada ya kustaafu..kwa kuwa alikuwa ni running dog basi akumbukwe..aende hata huko Somalia akatuwakilishe katika ngazi ya ubalozi..


Tunajua na tulisikia Rais akiwaahidi Askari wote nchini kuwa ile pesa ya DUTY FREE sasa itaingia kwenye acc. za Askari wote moja kwa moja lakini sasa ni miezi zaidi ya mitano nasikia hawajaipata hii pesa.. anywa tusubri wakati utafika..pia tunajua kuna Askari wa Jeshi la Polisi waliotoka depo sasa ni karibia au zaidi miezi saba hawajaripwa posho wala mishahara.


Hawa hawa Polisi wenye njaa, maisha magumu, ambao hawajapewa mishahara na posho miezi zaidi ya saba ndiyo tunawapa silaha za moto wakalinde bank, wakatulinde sisi na mali zetu, wakasimamie usalama barabarani, wakajinunulie uniform alafu baadae tuwambie wanakula rushwa! hivi nani anaweza akafanya kazi kwa mazingira kama haya! hawa kazi yao ni tofuati na ya Shigongo ya #kunwaajimwanagu#..tunaposema haya hatufanyi kwa nia ya uchochezi ila tunajua Polisi wetu walivyo na shida toka anaingia Jeshini hadi anastafu, tunandugu zetu huko ni mapolisi na bahati nzuri first lady baba yake alikuwa Polisi, ameshi Ostybei, haya anayajua...na anajua why nasema Police is a running dog! baada ya mawindo Polisi huwekwa pembeni na
kutupiwa minofu isiyofaa..


Polisi anadharaulika na kila mtu, kuanzia viongozi, mpaka sisi wanajamii! Polisi kwetu ni kama CONDOM! inauma sana lamini lazma tuseme na msema kweli ni.mpenzi wa Mungu..hawa watu tuwape haki yao japo tunatambua sungura huyu ni mdogo.. tunasahau bila Polisi hii nchi ingekuwa na hali mbaya sana ya kiusalama, hali mbaya sana wakati wa chaguzi, hali mbaya wakati wa usiku na mchana wakati wa masika na kiangazi!.lakini kwa kuwa Polisi wetu wamefunzwa kuvumilia basi hujipa moyo na kosonga mbele huku wakichapa kazi, Polisi toka anaingia depo hadi anastafu ni shida tu! tafuta wenye ndg au wastafu wa Polisi wakusimlie..

Juzi kule Nzega nilimuona kamanda wa Jeshi la Polisi anawatoa Askari wake barabarani akiwemo DTO na RTO kwa kosa la gari kupata ajali na kuuwa raia..well and good maamzi lazma.yachukuliwe! lakini yale maamzi ni sahihi na yanasaidia kutatua tatizo? Najaribu kuwaza wakati mwingine mchawi wa Jeshi la Polisi ni Polisi wenyewe na ndiyo wanamalizana na mara nyingi wanafanya kazi kwa lengo la kuwafurahisha watu furani hasa watawala..Polisi msipojitambua ninyi wenyewe hakuna atakayewatambu mtaishia kusubri Rais wa upande wetu hadi dunia hii iishe..!


Ni kwele mazingira ya kazi zao ni tofauti na majeshi mengine lakini bado naamini ndani ya Jeshi la Polisi kuna tatizo kubwa! niliwahi kumuona RPC wa Ilala uchaguzi wa Meya anaingilia kwa kuvutana mashati na wanasiasasa..huku pembeni yake kukiwa na Askari wake wa ngazi ya chini..nilishangaa sana! RPC unakabana mashati na wanasiasa pembeni yake kukiwa na vijana wake wakakamavu na wenye misuri wa FFU! kwa kweli nilikudharau sana wewe RPC na na zile nyota zako nilizidharau! nadhani viongozi wao ndiyo wanashida zaidi na siyo Askari wa Chini..Jana tena nimeona huko mbeya mkuu wa trafiki anawatoa barabarani Askari wa usalama barabarani kwa makosa ya ajabu sana! hawa Askari wa chini mnawaonea sana na hamuwasaidii badalaye yake mnawaongezea msongo wa mawazo, ndiyo maana kila siku wanajiua kwa kujipiga risasi...Askari wa chini siku hizi uraiani hawana amani na huko makazini kwao ndiyo hana amani kabisaa.!

Kama mh. Mwigulu Nchemba unatasoma post hii nakuomba uwasidie hawa Askari wa chini, pia jaribu kuangalia na kupitia maamzi aliyoyachukua kamanda wa traffiki pale Nzega na Mbeya na kwingine kote, mimi naamini wale Askari wameonewa ila wananyamaza kwa kuwa hawana pakusemea! sisi tunawaonea Askari kwa matusi na mambo mengine na bado wao wenyewe ndani kwa ndani wanaoneana! Nina imani na wewe mh. Waziri, jaribu kuwasaidia hawa Askari wetu japo nimeandika mambo mengine ambayo hutayafurahia ila nakuomba basi yachukue yaliyokufurahisha..

Bahati mbaya waliyonayo hawa Askari hasa wa Jeshi la Polisi ni pale sisi tunaposikia habari za Askari kufukuzwa, kuwawa akiwa kazini au vinginevyo! baadhi yetu huwa ni kicheko, kufurahi na kushangilia, nderemo na vifijo! poleni sana Polisi kwa jamii, raia na watawala kuwafanya yatima... Polisi tunawapenda pale tunapohitaji huduma yao..wanasiasa wanapenda Askari kipindi cha uchaguzi na huwapatia ahadi za kila namna, sisi raia tunawathamini Askari pale tunapoona mwizi, jambazi, kibaka au pale tunapotaka msaada wao kwa namna nyingine.. hali ikiwa shwari Police is a running dog.

Kabla sijamaliza nimeona wiki iliyopita Mkuu wa Mkoa akimtuhumu kamanda Siro kuwa inawezekana amekula rushwa ya Sisha! mjadala wa swala hili umekuwa mkubwa sana..mbali na hilo la rushwa nimeona RC Makonda akiwaita maRPC katika mikutano yake na kuwataka watoe maelezo ya mambo kadhaa juu ya ulinzi na usalama! sijaona shida katika hili ila tatizo ni namna ya RC Makonda anavyowaita na kuwamlisha au kuwataka wajibi maswali anavyotaka yeye na bahati mbaya huwaita kwa dharau kama watoto wake kwa kuwa Polisi wamefundishwa utii na uvumilivu basi hufanya anachotaka RC Makonda! hivi mambo ya usalama, unamtaka RPC akuelezee kwenye vikao vyako na wananchi? hii nchi tunaipekeka wapi..kuna watu wanasema angekuwa brigedia au Offisa yoyote wa JWTZ angetii na kufanya kile RC Makonda anachowafanyia akina.Sirro? jibu ni ndiyo na kwa mjibu wa katiba yetu RC ni mteule wa Rais hivyo kwa ngazi ya Mkoa RPC hata SIRRO yuko chini yake! tatizo ni namna, wakati na mahali pa kufanyia haya mambo.. ..kuna haki ya kumpa heshima RC! na ni kwa mjibu wa katiba na siyo ubabe!..Tatizo RC amesahau kuwa hawa Ma RPC wana mafunzo na miiko yao ya kazi, wana jua utendaji wao wa kila siku, wanajua kuambizana na kupeana maelekezo ya namna mbali mbali ila siyo kwa style ile anayotumia Makonda..

RC ni mwenyekiti wa ulinzi na usalama Mkoa anashindwa nini kubanana na Ma RPC hawa kwenye vikao vyao vya ndani vya ulinzi na usalama ila ameamua kuwadhalilisha mbele ya jamii na kwenye mikutano ambayo inaonekana ni ya kisiasa hawa makamanda na kwa bahati mbaya wamekaa kimya (IGP na Nchemba mko wapi Makonda anawadhalilisha wapiganaji wako..).


Mh.Rais nina imani kubwa sana na wew, jitahidi sana kulitengeneza hili Jeshi la Polisi na kama ikiwezekana lifumue lote kuanzia mavazi yao wanayovaa maana nayo yamezoeleka sana na sasa raia wanayaona ya kawaida na wakati mwingine wakiyaona hawajisikii amani wala furaha..wafanye Polisi chombo kipya na msaada kwa raia, wafanye hawa Polisi watishe kwa majambazi na wasiotaka kufuata sheria, wafanye hawa Polisi wajisikie wao ni walinzi wa mali zetu, wafanye hawa Polisi wapende kazi zao, wape pesa ..!
[HASHTAG]#Wanalinda[/HASHTAG] bank# wanalinda mali zetu# wanatulinda sisi#wanafuata hatari sisi tunaikimbia#wanabeba bunduki sisi tunabeba ela# wanalala vituoni/au kwenye zile suti zao wakiumwa na mbu sisi tunalala ndani ya nyumba zetu nzuri#..Mh. Rais hebu watendee muujiza hawa Askari usisubiri mwaka huu uishe bila kuwatendea muujiza..
 
Back
Top Bottom