Leo nitajibu maswali mbali mbali ya Wapinga Mungu ambayo kila siku wanayatuma hapa. Nimetoa ruhusa kwa mtu yeyote yule kuyatumia popote pale atakapo.
Nitaanza kuweka maswali 5 na majibu yake, kila siku.
1. Swali: Kwa kuwa Mungu aliumba kila kitu, je aliumba giza, uovu, na mashimo ardhini? Kama aliumba uovu, haonyeshi kuwa mzuri mkamilifu. Kama sivyo, yeyote aliyeumba anaonyesha kuwa muumbaji pia.
Jibu: Mungu aliiumba vitu vyote. Giza si kitu, bali ni kutokuwepo au upungufu wa mwanga. Uovu si kitu, bali kutokuwepo au kupotoa mambo mema. Mashimo, giza, na maovu hayakuumbwa moja kwa moja na Mungu, lakini yametokea kama marudiorudio, au "matokeo ya maisha" ya mada, mwanga na mambo mema. Hivyohivyo, kivuli si kitu kinachojitegemea, kikiwa na mada, nishati, au roho. Hata hivyo, mimea inaweza kufa kwenye kivuli.
2. Swali: Kwa kuwa Mungu aliumba kila kitu kikiwa kizuri, kwa nini radi, milipuko ya magonjwa na majanga mengine hutokea?
Jibu: Kila kitu kilikuwa kizuri mwanzoni. Lakini Warumi 8:20-22 inaonyesha kuwa tokea wakati wa anguko, dunia "ilitiishwa chini ya ubatili" pia. Ulimwengu wote upo chini ya utawala wa mwovu(1 Yohana 5:19), na mkuu wa dunia hii ni Shetani kwa mujibu wa Yohana 12:31; 14:30.
3. Swali: Kwa nini Mungu aliwaumba Adam na Hawa, kwa kuwa Munug alijua kabla kwamba hawatamtii?
Jibu: Pamoja na Mungu kujua kuwa watafanya dhambi, anatuambia vitu kadhaa kutuonyesha kuwa kwa nini aliumba watu.
Kwa utukufu wake: Mungu aliumba watoto wake kwa utukfu wake. Isaya 43:7; 61:34.
Watu wa kuwapenda: Mungu anatupenda sana. Zaburi 145:9,17; 1 Yohana 3:1.
Kuwa watoto wake: 1 Yohana 3:1-2; Wagalatia 3:28, Warumi 8:15-17.
Kuishi ndani mwetu: 1 Yohana 4:12-16; Warumi 8:9-11.
Mungu hataki mtu yoyote apotee. Ezekiel 18:23, 32; 33:11; 2 Petro 3:9. Hata hivyo, Mungu hajuti kwa kuwaumba watu ambao walipopewa nafasi walichagua kwa hiari zao wenyewe kumkataa. Mungu aliishajua kabla kuwa watafanya dhambi, na bado hakupenda kuingilia uchaguzi wao au "kutokuwaumba."
Huenda moja ya sababu ya Mungu kuwaumba viumbe ambao watakuwa na sura yake inafanana na sababu ya wazazi kuwa na watoto. Ni kweli, watoto wana gharamua: nepi, chakula, na kweli wanasababisha maumivu ya kichwa tokana na kuugua, kuumia, na kutokutii lakini pamoja na hayo yote upendo unawafanya wastahili kuwepo.
4. Swali: Kwenye Mwa 2:16, kwa nini Mungu alimuumba Adam hali alijua kuwa ataanguka dhambini?
Jibu: Mungu anaweza kufanya kitu chochote kile, lakini mantiki ya kutokuwezekana si kitu. Mungu hawezi kumuumba kiumbe ambaye anachagua kumtii kama kiumbe huyo hawezi kuchangua kumtii Mungu. Kuweza kuchagua kumtii Mungu kunamaanisha kuwa na uwezo wa kuchagua kutokumtii Mungu.
5. Je Mungu aliumba maovu?
Jibu: Mwanzo yaweza oneekana ya kwamba ikiwa Mungu aliumba vitu vyote, kwa hivyo hata uovu uliumbwa na Mungu. Ingawaje uovu siyo "kitu" kama mwamba au umeme. Huwezi kuwa na ghala la uovu. Uovu hauwezi kujitegemea; ni kutokuwa na uzuri halisi. Kwa mfano, shimo ni kitu wazi, lakini linaweza kuwa kitu kingine. Tunaita ukesefu wa ugumu shimo, lakini haiwezi tenganishwa na ugumu. Kwa hivyo wakati Mungu aliumba, ni kweli kwamba vyote alivyo viumba vilikiwa vizuri. Kati ya kitu kizuri Mungu aliumba, vilikuwa viumbe vyenye uhuru wa kuchagua lililo jema. Ili tuwe na chaguo halisi, Mungu aliweza kuruhusu kuwepo na jambo kando ya jambo jema ili kuwepo na chaguo. Kwa hivyo Mungu aliruhusu hawa Malaika huru na Wanadamu kuchagua jema ama kukataa lililo jema (uovu). Wakati uhusiano upo kati ya vitu viwili vizuri, huwa tunasema kwamba huo ni uovu, lakini hiyo haiwezi kuwa "kitu" kilicho mlazimisha Mungu kukiumba.
Hata elezo zaidi litazaidia. Ikiwa mtu ameulizwa, "Je baridi huwepo?" pengine jibu litakuwa "ndio" ingawa hii huenda isiwe kweli. Baridi haiwepo, bali huja kunapokosekana joto. Vile vile, giza haliwepo; ni kutokuwa na mwangaza. Kwa hivyo uovu ni kutokuwa na wema, ama uzuri, uovu ni kukosekana na uwepo wa Mungu. Haikumlazimu Mungu kuumba uovu, lakini kuhurusu uovu kwa kukosa kwa wema.
Mungu hakuumba uovu, lakini uruhusu uovu uwepo. Kama Mungu hangeruhusu nafasi ya uovu, wote Mwanadamu na Malaika wengemtumikia Mungu kwa lazima, bali si kwa kuchagua. Mungu hakutaka "miigizo" kwa ufupi yenye ingefanya chenye aliwataka wafanye kwa sababu ya "ratiba" yao. Mungu aliruhusu jukumu la uovu ili tuwe na nia njema ya kweli na kuchagua ikiwa ama hatukutaka kumtumikia.
Kama binadamu walio na mwisho, hatuwezi kuelewa vilivyo Mungu asiye na mwisho (Warumi 11:33-34). Wakati mwingine twafikiri tunaelewa ni kwa nini Mungu anatenda jambo Fulani, kisha baadaye twagundua kwamba ilikuwa kwa dhumni tofauti mbali na lile tulilofikiri mbeleni. Mungu huvitazama vitu kwa hali ya utakatifu na mtazamo wa milele. Twavitazama vitu kutoka hali ya dhambi, kidunia au mtazamo wa muda. Ni kwa nini Mungu alimweka mwanadamu duniani akijua Adamu na Hawa watasini na kwa hivyo walete uovu, kifo, na matezo kwa mwanadamu? Ni kwa nini Hakuweza kutuumba wote na atuache tukae mbinguni kwenye tutakuwa wakamilifu na bila kuwa na matezo? Maswali haya hayawezi kujibiwa sehemu hii ya mbinguni. Chenye tunaweza kujua ni kwamba kama Mungu hutenda kazi takatifu na kamilifu na mwishowe itampa utukufu. Mungu aliruhusu jukumu la uovu ili atupe chaguo la kweli ikiambatana kama tunaweza kumwabudu. Mungu hakuumba uovu, lakini alihurusu. Kama hangeruhusu uovu tungemwabudu kwa idhini, si kwa chaguo la nia yetu.
Mungu awabariki na tuendelee kujifunza.