Is Mufuruki suffering the colonial legacy or nobility syndrome?

Mufuruki yuko sahihi. Tusilazimishe mambo. tutumie fursa kufanya kazi na wengine toka nje ili tupate ujuzi zaidi. Ni kweli vyuo vyetu vimejikita zaidi katika vyeti na kufaulu mitihani. hakuna training ya managers ya kiwango cha juu.
And that problem is even reflected in the level of discussion we are having here. Arguments zimejaa personal attacks. Utajua hata critical thinking hatuna. Yaani mtu hawezi kujenga hoja bila kumuattack mtu. Ni kweli aliosema Mufuruki yaudhi , lakini yana ukweli kwa hiyo yapaswa tujitafakari na kujitathmini
 

Na mbaya zaidi serikali ya awamu hii ndiyo kabisaa inapiga vita Critical thinking, na kuchochea unafiki wa kuimba sifa kwa watu. Mengi yanayofanyika ambayo ni kinyume kabisa na logic na mantiki, yanaimarisha sana unafiki na kutofikiri.

Kwa mfano, Marekani waliwekeza sana kuwashawishi vijana kusoma sayansi ili kukabiliana na tishio la Urusi, pale mrusi alivyorusha Sputnik angani. Matokeo yake tunayajua. Sisi tunawekeza kuwavuta wabunge wa upinzani wahame vyama vyao, tena tunawaambia wafanye haraka kabla hawajakuwa-blocked na sheria ambayo inakataza kurudia uchaguzi inapokaribia uchaguzi mkuu. baada ya hapo tunajiingiza kwenye chaguzi zenye kupoteza fedha, muda na rasilimali nyingi tu za taifa letu, ikiwa ni pamoja na kuwajingisha "maprofesa" wetu na "madaktari" wetu wahubiri huu ujinga na kuutetea kwamba "Demokrasia ina gharama".

Hapa napo tutavuna tu ujinga zaidi, wala hatukwepi
 
Mimi sioni tatizo mkenya kufanya kazi Tanzania, kama amefaulu vigezo vyote. ambalo serikali yetu ingeweza kufanya ni kuwa na programu ya kuwezesha watanzania waliosoma ndani na hata nje, kushika madaraka kwa wingi zaidi katika makampuni ya ndani na hata nje, on a competitive basis. tukianza kuwazoeza kuwapendelea, wala hawatakuwa good managers. tofautisha kulinda soko la ndani la bidhaa, na "kulinda soko la ndani la managers"
 
sasa ulitaka atetee ujinga? serikali hii haipendi wafanyabiashara, inawachukia kweli kweli wala siyo siri
 
Issue ni kuwa si kweli kuwa hakuna mtanzania mwenye uwezo kama au zaidi ya huyo mdada, kwahio isiwe sababu ya kuwatukana watanzania na kuwahadaa kuwa hakuna mwenye uwezo
 
Suala la Sylivia inawezekana ni msuguano wa diplomasia ya uchumi kati ya mataifa yetu mawili. Sylivia ungekuwa hatoki Kenya pengine angekuwa na nafasi zaidi. Ushauri wangu kwa kina Mufuruki ni kwamba kama watafute MTU competent kutoka mahali kwingine na si Kenya tu. Na hata ikiwezekana mtanzania kwenye Diaspora. Wapo watanzania Diaspora wanaweza kufit hiyo portfolio kama ndani inashindikana kupat mtu sahihi. Na pia hili ni somo kwa wakuu mbali mbali wa vitengo ndani ya makampuni ya simu, kwamba imeshindwa kuonyesha leadership skills mpaka wanatafutwa watu nje ya kampuni.
 
sasa ulitaka atetee ujinga? serikali hii haipendi wafanyabiashara, inawachukia kweli kweli wala siyo siri
Ni kweli mkuu,mfanyabiashara mkwepa kodi,mleta bidhaa fake nchini,hapendwi na serikali hii,tena wanachukiwa kweli,
 
Roho ya kukosa.Tatizo la Wabongo kuwa na chuki dhidi ya walio nacho kuwazidi.Angekuwa mzungu au mwarabu husikii kashfa akiwa tajiri zaidi ya kumpamba kwa misifa kedekede.Acheni Roho korosho
Kwani waliopata utajiri kwa biashara ya utumwa hawakuwa wezi? Roho ya kukosa ni mbaya sana! Hata benki angalia wafanyakazi wanavyokuangalia ukiwa mswahili mwenye mafanikio katika biashara. Wanakuangalia kama mwizi na hasa ukiongea nao kiswahili. Ukitaka ufanikiwe kama mambo ya mkopo na kadhalika wewe wapigie ung'en'ge tu. Loan application yako inapita tu. Ukisema nao kiswahili wanataka kugrab hiyo biashara yako wafanye wao. Hawajui kuna mambo mengi kwenye biashara ni si wazo peke yake!
 
Mfiaukweli,
Unajua wengine hawajui uchungu wa kuwekeza hela yako kwenye biashara. Ukiwekeza pesa yako unataka uhakikishe pesa yako haipotei na biashara inakua haraka inavyowezekana. Kwa hiyo unachagua leadership team itakayohakikisha hilo. Serikali yetu hilo inalijua ndiyo maana kule TIC, ukiwa na TIC Certificate of Incentives unapewa kitu kinachoitwa "automatic permits for employing an initial quota of 5 foreign nationals on the project holding Certificates of Incentives". Lakini wakati mwingine watekelezaji wa sheria ya uwekezaji wanalisahau hili au ni mkomoeni tu!
 
Mimi ndiyo maana namkumbuka sana Rais Mkapa pamoja na mapungufu ambayo yaliyojitokeza wakati wa utawala wake. Ni yeye aliyefanya kazi kubwa ya kuanzisha zoezi la kuvutia wawekezaji wakubwa na wadogo na hasa wa kigeni wakati huo kila kona ya nchi yetu inanuka ujamaa "uliotelekezwa". Kama ni kumuenzi katika hilo tumuenzi akiwa bado yuko hai.
 

Bado kuna watu wanawaza huo huo ujamaa uliotelekezwa.
 
Ni kweli mkuu,mfanyabiashara mkwepa kodi,mleta bidhaa fake nchini,hapendwi na serikali hii,tena wanachukiwa kweli,
Naam, umesema kweli. Kwa serikali hii, WAFANYABIASHARA WOTE NI WAKWEPA KODI, WALETA BIDHAA FEKI, WEZI. Hiyo ndiyo imani kubwa kabisa ndani ya serikali ya JPM. kwa hiyo hata anapokutana na wafanyabiashara, anafanya hivyo basi tu, lakini matendo yake yote yanaegemea FALSAFA hiyo
 
ahhahaaaa wanetutia hasara kwenye DART wanataka na wengine wale hasara
 
Acha kuuliza maswali 'magumu' hivi bro.
 
Mimi naamini wapo watanzania wengi wenye uwezo mkubwa kwenye nafasi kama hizo. Sasa najiuliza, kwani nafasi hizo zinapatikana kwa kuomba kazi kama zilivyotangazwa na kupitia kwenye mchujo au zinapatikana kwa kutokuomba hizo kazi an kubaki kulalamika tu na kusubiri kupata appointment za kisiasa?

Kuna bwana mmoja aliomba kazi pale Tanzania Petroleum Bulk Procurement Agency kupitia Sekretarieti ya ajira. Alikuwa na qualifications za ukweli na experience ya muda mrefu kuhusu maswala ya "downstream petroleum sector". Yeye hakuitwa hata kwenye interview. Sasa cha ajabu ukibahatika kumjua mtu aliyepewa nafasi ile utachoka na kubaki mdomo wazi. Tabia hii ikiendelezwa kwenye ajira kwa ajili ya ku-support uchumi wa viwanda tutakuwa tunamuangusha mkulu kabisaaaaa. Ameshindwa hata kubadili muonekano wa tovuti yao iweze kuakisi ukweli wa wanalolifanya kweli??!!
 
Mufuruki yuko sahihi. Tusilazimishe mambo. tutumie fursa kufanya kazi na wengine toka nje ili tupate ujuzi zaidi. Ni kweli vyuo vyetu vimejikita zaidi katika vyeti na kufaulu mitihani. hakuna training ya managers ya kiwango cha juu.
Vyuo vya Tanzania ni bure kabisa, mturuki yuko sawa
 
pumba tupu, ukweli humuutaki kabisa
 
Wakati ninafanya MBA pale UDSM kati ya watu walionifundisha Research Methodology ni Professor Okoso Amaa. Nilimuuliza swali ambalo hakuwa na majibu yake. Nilimuuliza hivi "Kwa nini UDSM Business School hawafundishi report writing kama mojawapo ya core subject ili kuendana na expected deliverables kwenye Research Methodology?" Alijibu kwamba yeye yuko Part-time na hana jibu kwa nini haifundishwi. Huyu ndiye aliyeanzisha Faculty of Commerce and Management - wakati ule (Kwa sasa UDSM Business School). Ndiyo maana wanafunzi wengi wa UDSM wanapata shida sana ku-compile Busines Plan reports and Feasibility Study reports. Kwa sasa sijui hali ikoje pale? Lakini tunaweza kubadilika. Muda wote wa maisha yangu nimefanya kazi nyingi kwenye private sector. Nimejifunza mambo mengi sana huko kuliko niliyojifunza vyuoni. Ninatamani sana kuwafundisha vijana mambo haya lakini sina fursa kwa sababu sina GPA ya kuweza kufundisha vyuo vya elimu ya juu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…