Is It True?

Ni kweli halloo!Hiyo ya mwisho a woman is afraid of a cockroach inanikumbusha kisa kimoja mwaka 2006.Nilipokea ugeni wa wamama watatu toka denmark waliokuja kutembelea vituo vya watoto yatima.Nilikuwa nimewafanyia booking ya malazi kwenye hoteli moja.Kila mmoja alipata chumba chake na jioni ya siku waliowasili nchini nikawapeleka kwenye hoteli kuwaonesha vyumba vyao.Baada ya kuwapeleka wawili kwenye vyumba vyao nikabaki na mmoja wa mwisho ambaye pia nilimpeleka kwenye chumba chake. Huyu alikuwa mzungumzaji sana..... maswali meeengi juu ya tanzania.Nikafungua chumba tukaingia kisha tukasimama ili nimalize kujibu alichoniuliza.Mara huyo mama akamwona mende akikatisha sakafuni kuelekea mvunguni mwa kitanda.Mama alitahayari na kupiga kelele huku akikimbia kukaa nyuma yangu "My God Mr Shieka, what's that!"Aliuliza kwa sauti ya kigugumizi.Nilimpooza kwa kumwambia ni mdudu wa kawaida tu asiye na madhara.Akaniambia hatoweza kulala kwenye chumba kile alihitaji kingine.Ilibidi nimkubalie tukafanya mpango wa chumba kingine.Hawa wenzetu ni kweli ni waoga sana wa wadudu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…