njiwa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2009
- 13,259
- 7,106
Duuh! Wee Zawadi mbona unatia aibu na ung'eng'e wako usioeleweka?
Lakini si umeelewa..?!! sio mtihani huu..
Duuh! Wee Zawadi mbona unatia aibu na ung'eng'e wako usioeleweka?
Lakini si umeelewa..?!! sio mtihani huu..
Ilikuwa jambo la maana kuongea juu ya gadafi maanake mwanzilishi wa mada hii alimtaja kama mojawapo ya watu wanaoelewa maana yake waafrika kuungana. Ingawa nakubaliana naye kuwa kuna umuhimu wa kuungana kama sisi waafrika, inafaa tujihadhari wa viongozi ambao lengo lao sio kuendeleza Afrika, bali ni kujitafutia hadhi na mamlaka makuu. Mimi naonelea kutumia gadafi kama mfano wa viongozi ambao wanafaa kuigwa ilikuwa ni makosa, maanake tunajua sasa Ghadafi siye mtu anayeaminika. Juzi alitembelea Bara Uropa na kuwaambia wamlipe kitita kikubwa maana anafanya kazi nzuri sana ya kuwazuia waafrika weusi kuhamia huko wakipitia Libya, na tena akatumia maneno mengine ninaona aibu kuyarudia kwa sababu yanakera sana.
Sioni ubaya wowote mtu kuwa mwislamu, lakini ungekubaliana na mimi vita vya kidini ndivo vimesababisha maafa mengi sana duniani hata kuliko magonjwa yote. Kwa nini mtu atake kusababisha vurumai za kidini Afrika akitazamia kulazimisha kila mtu awe wa dini hili au lingine? Kama umekuwa ukifuatilia matamshi yake ungejua naongea juu ya nini. Kama mtu yuataka kudadilisha dinilake, afanye hivyo kwa hiari yake, sio kwa kulazimishwa (na mtu kulazimishwa si lazima uwekelewe bunduki kwa kichwa, kuna njia tofauti za kulazimsha).
rudia kuisoma post yako uilinganishe na issue inayojadiliwa hapa.
Ndugu MkenyaMzalendo,
Hapa africa Dini yenye wafuasi wengi zaidi kuliko wote ni Islam pili Ukristo lakini wote wafuasi wa dini mbili hizi tukufu wanaishi pamoja kwa amani kabisa kwa mfano kama hapa Tanzania Aids na magonjwa mengine ndio yanayo tuuwa zaidi kuliko Dini (Ndugu yangu angalia propaganada za Media zisikudanganye hasa CNN, BBC na Aljazeera).
Kwani wewe umenielewa vipi kutoka kauli uliyo-quote? Mantiki ya kitoto na lugha mbovu aliyotumia mwandishi ingefaa somo la Civil Studies kindergarten ya madrasah.
Naam umenena ukweli (ingawa ningpenda upachike takwimu zinazoonyesha waislamu ni wengi kuliko wachristo barani Africa),
Lakini nadhani haukunifahamu kabisa. Ukifanya utafiti haswa wa historia ya hizi dini mbili katika bara uropa na pia Asia, utakuta ya kuwa takwimu za watu waliouawa kwa sababu ya kidini imezidi idadi ya mauaji mengine yote
Ndugu Coach Parcells,
Hakuna makosa katika maneno alio andika ndugu Zawadi.
Ndugu Igunga,
Utamaduni wa uduni unawakweza. Crap is crap.
![]()
Kwani wewe umenielewa vipi kutoka kauli uliyo-quote? Mantiki ya kitoto na lugha mbovu aliyotumia mwandishi ingefaa somo la Civil Studies kindergarten ya madrasah.
My friend let me tell u something; I have studied Spanish, Arabic and French for six months only. ...
I blog everywhere in 6 different languages and I master none of them. That is my hobby and i enjoy it.
Ilikuwa jambo la maana kuongea juu ya gadafi maanake mwanzilishi wa mada hii alimtaja kama mojawapo ya watu wanaoelewa maana yake waafrika kuungana. Ingawa nakubaliana naye kuwa kuna umuhimu wa kuungana kama sisi waafrika, inafaa tujihadhari wa viongozi ambao lengo lao sio kuendeleza Afrika, bali ni kujitafutia hadhi na mamlaka makuu. Mimi naonelea kutumia gadafi kama mfano wa viongozi ambao wanafaa kuigwa ilikuwa ni makosa, maanake tunajua sasa Ghadafi siye mtu anayeaminika. Juzi alitembelea Bara Uropa na kuwaambia wamlipe kitita kikubwa maana anafanya kazi nzuri sana ya kuwazuia waafrika weusi kuhamia huko wakipitia Libya, na tena akatumia maneno mengine ninaona aibu kuyarudia kwa sababu yanakera sana.
Sioni ubaya wowote mtu kuwa mwislamu, lakini ungekubaliana na mimi vita vya kidini ndivo vimesababisha maafa mengi sana duniani hata kuliko magonjwa yote. Kwa nini mtu atake kusababisha vurumai za kidini Afrika akitazamia kulazimisha kila mtu awe wa dini hili au lingine? Kama umekuwa ukifuatilia matamshi yake ungejua naongea juu ya nini. Kama mtu yuataka kudadilisha dinilake, afanye hivyo kwa hiari yake, sio kwa kulazimishwa (na mtu kulazimishwa si lazima uwekelewe bunduki kwa kichwa, kuna njia tofauti za kulazimsha).
Katika hilo nakubaliana na wewe kuwa tunapoongelea muungano wa waafrika tunatakiwa kuwa makini, maana kuna viongozi wanaongelea muungano baada ya mambo yao kukwama. Mfano Gaddafi sio kiongozi wa kutuambia masuala ya muungano wa Afrika wakati huko nyuma alikuwa anaongoza kwa kuwadharau watu weusi na kuwa kuhamasisha zaidi muungano wa waarabu. Ni huyo aliyekuwa hataki kuziita nchi za maghreb kama ni Afrika. Ni katika kipindi chake waafrika weusi walinyanyaswa na kufukuzwa kutoka Libya katika miaka ya 1980. Halafu huyo ndiyo kiongozi aliyediriki kusema ukristo sio dini ya kiafrika ila uislamu akasahau kwamba hata uislamu sio dini ya kiafrika.
Baada ya kukuta waarabu wenzake hawaeleweki ndio anakuja kwa nguvu kupiga kelele za muungano wa afrika. Naungana na MkenyaMzalendo kuwa AU haina msaada wa maana kwa waafrika ndio maana watu kama Al Bashir, Mugabe na hata Kibaki wamefaidika sana na uwepo wa AU lakini raia wa kawaida huko Somalia wanaumia sana huku nchi zikiogopa kusaidia Somalia. Lakini lilipokuja suala la maslahi ya kibeberu pale DRC nchi za zimbabwe, Namibia, Angola, Rwanda, Uganda na nyinginezo zilipeleka wanajeshi wengi mno.
Kwa hiyo mi nashauri ili Muungano wa Afrika ufikiwe kila nchi iungane na jirani inaemuamini halafu pole pole tutakuja kuunganisha Africa nzima.