kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 277
MHASIBU mkuu wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Ben Mpete amekuwa mwanachama wa CCM wa saba kutangaza nia ya kuwania ubunge wa jimbo la Iringa Mjini ambalo kwa sasa linashikiliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Monica Mbega.
Mbali na Mbega kutangaza kutetea kiti chake hicho, wana CCM wengine waliotangaza nia ya kumpokonya kiti cha ubunge ni pamoja na Edwin Sambala, Frederick Mwakalebela, Thomac Kimata, Jesca Msambalavangu na Zuberi Mwachula.
Mpete amesema umefika wakati wa kupokezana kijiti kutoka kwa mbunge wa sasa. Mbega amekuwa mbunge kwa awamu tatu tofauti moja akiwa Mbunge wa viti maalumu.
Tunakubaliana kwamba kazi aliyoifanya katika kusukuma gurudumu la maendeleo la jimbo la Iringa ni kubwa lakini muda wake wa kupumzika na mimi nimpokee kazi hiyo ya uwakilishi umewadia, alisema.
Kama alivyo Mbega, Mpete mwenye shahada ya juu ya uhasibu aliyoipata Novemba mwaka jana alisema atatumia utashi wake kisiasa, vipaji, akili na elimu aliyonayo kusaidiana na wakazi wa jimbo la Iringa Mjini kuharakisha maendeleo.
Alisema ajenda yake kubwa endapo atachaguliwa itakuwa ni kuufanya mji wa Iringa kuwa mji wa kitalii, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fursa ya elimu bora inakuwa kwa wakazi wote wa mjini hapa.
Tutaanzisha mfuko maalumu wa kusaidia wajane na yatima, na mfuko kwa ajili ya vijana wenye umri wa kati ya miaka 20 na 30, na pia tutahakikisha vijana wetu wanapata elimu ya ujasiriamali ili kuwawezesha kujua vyanzo vya mitaji, jinsi ya kuwekeza na kufanya biashara na mbinu za kujiajiri, alisema.