Iringa hakuna mafuta ya taa kwa wiki tatu sasa!!

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,300
33,917
Kwa muda wa wiki tatu sasa wakazi wa Manispaa ya Iringa hawana Mafuta ya taa na hakuna taarifa yoyote toka wa viongozi wa Serikali wala wamiliki wa vituo vya Mafuta ni nini kinaendelea. Bei ya Umeme iko juu na mafuta hayapatikani serikali inategemea wananchi wataacha kukata miti ili kutengenezea Mkaa?
 
Viongozi wote wa nchi wako dodoma. Kesho wanakutana na katibu mkuu ccm kufundwa namna ya kuua upinzani. Kaeni chonjo. Mbeya tunasubiri tuone
 
Swali la kujiuliza ni kwa nini EWURA ambao ndiyo Sole Regulators wa masuala ya nishati hawakujua mapema kama Mafuta ya taa yanakwisha hadi wanasubiri yememalizika kabisa ndiyo wanakuja na hoja ya ku-down Grade mafuta ya ndege ili yatumike kama mafuta ya taa? Hivi hawajui kama ni asilimia 99 ya watanzania wanategemea mafuta ya Taa kama nishati yao kwa matumizi ya kila siku majumbani mwao?
 
Kwa muda wa wiki
tatu sasa wakazi wa Manispaa ya Iringa hawana Mafuta ya taa na hakuna
taarifa yoyote toka wa viongozi wa Serikali wala wamiliki wa vituo vya
Mafuta ni nini kinaendelea. Bei ya Umeme iko juu na mafuta hayapatikani
serikali inategemea wananchi wataacha kukata miti ili kutengenezea
Mkaa?

Hata Dar yameadimika.
 
Hii ndo Tanzania na Viongozi wanaojali maslai yao zaidi na kusahau mahitaji ya Wanainchi wao ambao waliwapa dhamana ya kuhakikisha mahitaji yao muhimu yanapatikana kwa wakati na urahisi.
 
Navumilia tu! Nawaomba wauza mkaa wasipandishe bei. Jana nilikia wanao mpango wa kuuza mafuta ya ndege, je imefikia wap? Je kwa sisi wa mikoani tutaambulia kitu kweli? Ukiwaza sana mambo ya nchi unaweza kuwa chizi....
 
Kwa muda wa wiki tatu sasa wakazi wa Manispaa ya Iringa hawana Mafuta ya taa na hakuna taarifa yoyote toka wa viongozi wa Serikali wala wamiliki wa vituo vya Mafuta ni nini kinaendelea. Bei ya Umeme iko juu na mafuta hayapatikani serikali inategemea wananchi wataacha kukata miti ili kutengenezea Mkaa?
Hujakosea kabisa mr.allen,kerosene imekuwa adimu sana hapa iringa,but nashangaa pale mafinga yanapatikana kiurahisi kwa bei kati ya 2150~2200/lita.
 
Mafuta ya taa yakikosekana maana yake no chakachua kwenye petroli. Afadhali!
 
tuliambiwa tutatumia mafuta ya ndege kwani ndo rahisi
cah kujiuliza kama ndivo mbona usafiri wa ndege ni ghali kuliko dala dala
 
Back
Top Bottom