Iran's Revolutionary Guards Launch 1st military satellite into Orbit Successfully

BINARY NO

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2011
Posts
2,155
Reaction score
2,171
Baada ya failure za kupeleka satellites kadhaa hatimae Iran Leo hii imefanikiwa kurusha satellite ya kijeshi yenye matumizi ya kijeshi angani....Tutegemee US,Israel na NATO kulaumu maana apo awali walikua wakihituhumu Iran kua satellite zake uenda zikawa na matumizi ya kijeshi

---

Iran.jpg

An Iranian military satellite, mounted on a domestically-built rocket, was sent into space by the air arm of the Islamic Revolutionary Guard Corps (IRGC) on Wednesday. The device is said to be the first of its kind in the country.

Called Qassed, the two-stage rocket blasted off on Wednesday from an undisclosed location in “the central desert,” with the Noor 1 satellite on board. It remains to be seen whether the launch has been completely successful, although state media said the satellite reached an altitude of 425km.

The Islamic Revolutionary Guard Corps oversaw the launch, which was timed to mark the elite group’s anniversary, according to Mehr news agency. The IRGC’s Aerospace Forces have an array of long-range missiles and satellite launch vehicles developed by Iran’s rocket industry.

It seems to be the second space-bound launch since February of this year. At that time, Iran reported that it had successfully put a communications satellite – called Zafar 1 – into orbit. However, the Defense Ministry later revealed that the device’s speed had been too low to actually reach orbit.

Source: Iran’s Revolutionary Guards launch ‘1st military satellite’ into orbit – state media
 
Jeshi la IRGC larusha satalaiti ya kwanza ya kijeshi ya Iran katika anga za mbali

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limerusha kwa mafanikio satalaiti ya kwanza ya kijeshi ya Iran katika anga za mbali.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sepah News, Jeshi la IRGC limetumia kombora la kubeba sataliti la Qased kurusha katika anga za mbali sataliti hiyo inayojulikana kama Nour-1. Oparesheni ya kurusha satalaiti hiyo imetekelezwa katika eneo la jangwani la Dasht-e-Kavir kati mwa Iran. Kwa mujibu wa taarifa satalaiti hiyo imerushwa katika anga za mbali katika umbali wa zaidi ya kilomita 425 kutoka sayari ya dunia. Kombora hilo la kurushia satalaiti lina sehemu ya aya ya 13 ya Sura ya 43 ya Qu'rani Tukufu inayosema:..."Ametakasika aliye mfanya huyu atutumikie, na tusingeliweza kufanya haya wenyewe."

Sataliti hiyo imereushwa katika anga za mbali na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu wakati jeshi hilo linaadhmisha mwaka wa 41 tokea kuasisiwa kwake mnamo Aprili 22 mwaka 1979.

Kurushwa satalaiti hiyo ya kijeshi katika anga za mbali ni tukio la kihistoria kwa sekta ya anga za mbali nchini Iran.

Iran ilirusha katika anga za mbali satalaiti yake ya kwanza kabisa inayojulikana kwa jina la Omid (yaani Tumaini) mwaka 2009. Iran pia imetangaza kuwa, katika kipindi cha miaka michache ijayo itatuma mwanaadamu katika anga za mbali. Tayari mazoezi yameshafanyika kuhusiana na lengo hilo kwa kutumwa nyani hai katika anga za mbali ambaye alirejea ardhini akiwa salama.

Mafanikio haya ya Iran katika sekta ya anga za mbali yamepatikana licha ya kuwepo vikwazo vya kila upande vya nchi za Magharibi dhidi ya Jamhuri ya Kislamu.

4bv88971a0f8bc1n15x_800C450.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
View attachment 1426369

Sent using Jamii Forums mobile app
Hili bandiko hujalitendea haki MKUU ilitakiwa lijitegemee

Sent using My COVID-19
 
Back
Top Bottom