Iran yavumbua Ballistic Missile yenye composite built-engine

Amewashindwa washika manati kwa Iran ataweza? Waswahili mnatabu sana
FB_IMG_15813725589306962.jpg

Tafuta kingine cha kuzungumza
 
Kila mtu anaelewa mpango/mipango ni nini rafiki.
Mpango wa Israel wayahudi wa Judea na wapalestina waarabu unaitwa mpango was karne.

Mpango was Iran kuifuta Israel ulipaswa use umeshatekelezwa zamani sana ndio maana nauliza wamekwama wapi?
Kwan mpango wa muamala wa karne wa ISRAEL Unakwamia wapi ?!

Mbna huu huuongelei ?![emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iran imezindua kombora jipya linalojulikana kama 'Raad 500' ambalo linatumia injini aina ya kompositi inayojulikana kama 'Zahir' sambamba na kuzindua kizazi kipya cha makombora ya kijeshi na makombora ya kubeba satalaiti. Uzinduzi huo umehudhuriwa na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hussein Salami.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sepah News, katika hafla hiyo pia kumezinduliwa kizazi kipya cha injini aina ya kompositi ya anga za mbali inayojulikana kama 'Salman' ambayo itatumika katika makombora ya kijeshi na makombora ya kubeba satalaiti.

Mafanikio hayo yataiwezesha Iran kutengeneza makombora ya kubeba satalaiti yenye uzito wa chini na pia makombora ya nchi kavu kwa nchi kavu na nchi kavu kwa anga. Hali kadhalika teknolojia mpya iliyotumika inawezesha makombora hayo ya Iran kukwepa ngao za makombora zinazotumiwa na adui.

Kamanda Mkuu wa IRGC Meja Jenerali Salami (kushoto) akihutubu katika halfa ya kuzindua makombora mapya

Mafanikio ya Iran katika sekta ya ulinzi na kujihami yanaendelea kutoa indhari kwa madola ya kigeni yanayofanya chochoko dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kadiri Iran inavyopiga hatua kubwa katika sekta hiyo ndivyo maadui wake wanavyozidi kufeli na kudhoofika. Iran imefanikiwa katika sekta ya kijeshi pamoja na kuwa imewekewa vikwazo ambavyo havijawahi kushuhudiwa dhidi ya nchi yoyote ile.

TIM AMERIKA MJIPANGE

View attachment 1352947

Sent using Jamii Forums mobile app
A nation with 4000 years of civilisation being forced to make major arms of destruction instead of developing the welfare of its people.
 
Arms Mhim sana katika ulimwengu wasasa nahata wazamani nahata ujao pia
A nation with 4000 years of civilisation being forced to make major arms of destruction instead of developing the welfare of its people.
Maendeleo yawati ama raia ama taifa la iran kwaujumla wake yanazingatiwa sana na viongozi wa IRAN Ila wapuuzi wamataifa yakigeni ndio wanaleta uchawi kwakuwasulubu raia kwavikwazo vyakila leo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iran imezindua kombora jipya linalojulikana kama 'Raad 500' ambalo linatumia injini aina ya kompositi inayojulikana kama 'Zahir' sambamba na kuzindua kizazi kipya cha makombora ya kijeshi na makombora ya kubeba satalaiti. Uzinduzi huo umehudhuriwa na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hussein Salami.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sepah News, katika hafla hiyo pia kumezinduliwa kizazi kipya cha injini aina ya kompositi ya anga za mbali inayojulikana kama 'Salman' ambayo itatumika katika makombora ya kijeshi na makombora ya kubeba satalaiti.

Mafanikio hayo yataiwezesha Iran kutengeneza makombora ya kubeba satalaiti yenye uzito wa chini na pia makombora ya nchi kavu kwa nchi kavu na nchi kavu kwa anga. Hali kadhalika teknolojia mpya iliyotumika inawezesha makombora hayo ya Iran kukwepa ngao za makombora zinazotumiwa na adui.

Kamanda Mkuu wa IRGC Meja Jenerali Salami (kushoto) akihutubu katika halfa ya kuzindua makombora mapya

Mafanikio ya Iran katika sekta ya ulinzi na kujihami yanaendelea kutoa indhari kwa madola ya kigeni yanayofanya chochoko dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kadiri Iran inavyopiga hatua kubwa katika sekta hiyo ndivyo maadui wake wanavyozidi kufeli na kudhoofika. Iran imefanikiwa katika sekta ya kijeshi pamoja na kuwa imewekewa vikwazo ambavyo havijawahi kushuhudiwa dhidi ya nchi yoyote ile.

TIM AMERIKA MJIPANGE

View attachment 1352947

Sent using Jamii Forums mobile app
naona picha ya marehemu kwa mbali akiangalia copy
 
Back
Top Bottom