Iran yavumbua Ballistic Missile yenye composite built-engine

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,601
Iran imezindua kombora jipya linalojulikana kama 'Raad 500' ambalo linatumia injini aina ya kompositi inayojulikana kama 'Zahir' sambamba na kuzindua kizazi kipya cha makombora ya kijeshi na makombora ya kubeba satalaiti. Uzinduzi huo umehudhuriwa na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hussein Salami.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sepah News, katika hafla hiyo pia kumezinduliwa kizazi kipya cha injini aina ya kompositi ya anga za mbali inayojulikana kama 'Salman' ambayo itatumika katika makombora ya kijeshi na makombora ya kubeba satalaiti.

Mafanikio hayo yataiwezesha Iran kutengeneza makombora ya kubeba satalaiti yenye uzito wa chini na pia makombora ya nchi kavu kwa nchi kavu na nchi kavu kwa anga. Hali kadhalika teknolojia mpya iliyotumika inawezesha makombora hayo ya Iran kukwepa ngao za makombora zinazotumiwa na adui.

Kamanda Mkuu wa IRGC Meja Jenerali Salami (kushoto) akihutubu katika halfa ya kuzindua makombora mapya

Mafanikio ya Iran katika sekta ya ulinzi na kujihami yanaendelea kutoa indhari kwa madola ya kigeni yanayofanya chochoko dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kadiri Iran inavyopiga hatua kubwa katika sekta hiyo ndivyo maadui wake wanavyozidi kufeli na kudhoofika. Iran imefanikiwa katika sekta ya kijeshi pamoja na kuwa imewekewa vikwazo ambavyo havijawahi kushuhudiwa dhidi ya nchi yoyote ile.

TIM AMERIKA MJIPANGE

4bv6ec84f4a9411lfli_800C450.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Nadharia ya uhuni.
Nadharia ya uhuni ilopiga kambi za jeshi la US pale IRAQ [emoji23][emoji16][emoji23][emoji23]

MKUU Nakukumbusha Kesho Ni Bahman 41(Mapinduzi Yakiislam Yanatimiza Mwaka Wake Wa 41) Nakumbuka Kuna Uzi Wako Uliutoa Ukasema Kama Mwaka Jana 2019M Ulikua Haumalizi Jamhuri Yakiislam Ya AJEMI Ina Anguka [emoji16][emoji16][emoji16] Ule Uzi Kila Nikiutafta Naona Siuoni Sijui Ulikwisha Ufutaa[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bwana Utam,
Vita ndivyo ilivyo, hata hamas huvurumusha makatyusha Israel kujiburudisha. Tunaangalia matokeo nani mshindi.
 
Maendeleo ya kutengeneza machuma ya kuua watu?
Hayo unayo yaita machuma ndio yanaipa kiburi marekani kufanya anayo duniani hayo unayo yaita machuma ndio yanayo kulinda ndani ya nchi yako.
Hata hivyo Iran haijapiga hatua kwenye silaa tu hata miundo mbinu yake imepiga hatua kubwa mno jambo ambalo sisi litatuchukua miaka mingi kufikia hayo maendeleo.
 
Iran imezindua kombora jipya linalojulikana kama 'Raad 500' ambalo linatumia injini aina ya kompositi inayojulikana kama 'Zahir' sambamba na kuzindua kizazi kipya cha makombora ya kijeshi na makombora ya kubeba satalaiti. Uzinduzi huo umehudhuriwa na Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) Meja Jenerali Hussein Salami.

Kwa mujibu wa tovuti ya Sepah News, katika hafla hiyo pia kumezinduliwa kizazi kipya cha injini aina ya kompositi ya anga za mbali inayojulikana kama 'Salman' ambayo itatumika katika makombora ya kijeshi na makombora ya kubeba satalaiti.

Mafanikio hayo yataiwezesha Iran kutengeneza makombora ya kubeba satalaiti yenye uzito wa chini na pia makombora ya nchi kavu kwa nchi kavu na nchi kavu kwa anga. Hali kadhalika teknolojia mpya iliyotumika inawezesha makombora hayo ya Iran kukwepa ngao za makombora zinazotumiwa na adui.

Kamanda Mkuu wa IRGC Meja Jenerali Salami (kushoto) akihutubu katika halfa ya kuzindua makombora mapya

Mafanikio ya Iran katika sekta ya ulinzi na kujihami yanaendelea kutoa indhari kwa madola ya kigeni yanayofanya chochoko dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kadiri Iran inavyopiga hatua kubwa katika sekta hiyo ndivyo maadui wake wanavyozidi kufeli na kudhoofika. Iran imefanikiwa katika sekta ya kijeshi pamoja na kuwa imewekewa vikwazo ambavyo havijawahi kushuhudiwa dhidi ya nchi yoyote ile.

TIM AMERIKA MJIPANGE

View attachment 1352947

Sent using Jamii Forums mobile app
Wairan noma sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Nadharia ya uhuni ilopiga kambi za jeshi la US pale IRAQ [emoji23][emoji16][emoji23][emoji23]

MKUU Nakukumbusha Kesho Ni Bahman 41(Mapinduzi Yakiislam Yanatimiza Mwaka Wake Wa 41) Nakumbuka Kuna Uzi Wako Uliutoa Ukasema Kama Mwaka Jana 2019M Ulikua Haumalizi Jamhuri Yakiislam Ya AJEMI Ina Anguka [emoji16][emoji16][emoji16] Ule Uzi Kila Nikiutafta Naona Siuoni Sijui Ulikwisha Ufutaa[emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
Acha maneno
ShowImage.jpeg

Israel anti ballistic missile

2c833f8e-6584-484f-96f7-2df670747129.jpg

Hii ballistic missile yao ziko nne hapo in one
 
Back
Top Bottom