Sinoni
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 6,187
- 10,659
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuma shehena zingine mbili za misaada ya kibinadamu katika mji wa Aleppo (Halab) uliokombolewa hivi karibuni kutoka mikononi mwa magaidi wakufurishaji.
Mkuu wa Hilali Nyekundu ya Iran (IRCS) Amir Muhsin Ziaee amesema shirika hilo limetuma tani 70 za misaada ya dharura Aleppo katika kipindi cha wiki moja iliyopita. Amesema shehena hiyo inajumuisha vyakula, mahema na dawa.
Hali kadhalika amesema ICRS ilituma vikopo 150,000 vya chakula mjini Aleppo mapema mwezi Disemba na kabla ya hapo pia shehena ya tani 80 elfu ilitumwa katika mji huo. Iran imekuwa ikituma misaada ya kibinaadamu mara kwa mara nchini Syria kadiri inavyowezekana.
Jeshi la Syria lilitangaza Disemba 22 kuwa limefanikiwa kuukomboa kikamilifu mji wa Aleppo ambao umekuwa ukikaliwa kwa mabavu na magaidi tokea mwaka 2012.
Ushindi huo ulipatikana pamoja na kuwa magaidi mjini Aleppo walikuwa wakipokea misaada kutoka Marekani, Uturuki na baadhi ya nchi za Kiarabu katika Ghuba ya Uajemi.