Iran yakubali kusalimu amri, kuufuata ushauri wa Donald Trump rais wa Marekani

kenny mtanashati

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2021
Posts
322
Reaction score
902
Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka Iran irudi haraka kwenye meza ya mazungumzo na kusaini makubaliano ya kusitisha mpango wa nyuklia kabla haijapoteza kila kitu. Rais Trump ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Truth social Taarifa hiyo nmekuekea hapo chini kwenye comments

Trump amesema anafahamu mipango yote ya kimkakati ya mashambulizi ya Israel na inayofuata ni mikubwa na ya kikatili zaidi hivyo Iran isithubutu kuingia kwenye mtego wa kujaribu kupigana na Israel kwakua itapoteza kila kitu ikiwemo utawala wa Ayatollah

Rais Trump amesema Israel ina uwezo mkubwa kimedani na silaha za hatari ikiwemo za ubora wa juu mno zinazozalishwa Marekani na mbaya zaidi inajua kuzitumia kwa usahihi mkubwa

Trump anasema aliipa Iran siku 60 kusaini makubaliano ila ikazembea nafasi hiyo hatimaye usiku wa kuamkia leo ambapo ilikuwa ni siku ya 61 Israel ikachukua hatua kali. Trump anasema aliionya Iran kwamba inaweza kukumbana na hatua ambazo haijawahi kushuhudia, kuambiwa au kusikia ila ikawa haiamini ikadhani ni vitisho vitupu tu

Rais Trump amesema jambo lenye tija kwa sasa kwa Iran ni kuchangamkia fursa ya mazungumzo kukwepa mkono zaidi wa Israel, fursa ambayo ameiita kama nafasi ya pili "Second Chance" na kuitaka Iran kuitumia haraka kabla mambo hayajaharibika kabisa

Wakati huo huo rais wa Iran Masoud Pezeshkian amelaani mashambulizi ya Israel na kuapa kwamba lazima Iran ilipize kisasi chenye uzito unaostahili

Je Iran itajibu ili kupata awamu ya pili ya mashambulizi ya Israel?.

FB_IMG_1749829769426.jpg
 
Iiiihhh hiiii, Trump is breathing fire silently..!!
 
Dawa ya US ni kwenda nae kibabe ,kama Bwana kiduku alivyo fanya hadi saivi ana Nukes
 
kenge wewe hujui,yale ni maslahi ya Korea kusini
Binafsi mtu aki jibu kwa tusi sehemu Isio itaji tusi bali hoja moja kwa moja mtu uyo kwangu ni mjinga na mpumbavu , ivyo sina budi kuku certify kwamba we ni mjinga na mpumbavu .over
 
Rais wa Marekani Donald Trump ameitaka Iran irudi haraka kwenye meza ya mazungumzo na kusaini makubaliano ya kusitisha mpango wa nyuklia kabla haijapoteza kila kitu. Rais Trump ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Truth social Taarifa hiyo nmekuekea hapo chini kwenye comments

Trump amesema anafahamu mipango yote ya kimkakati ya mashambulizi ya Israel na inayofuata ni mikubwa na ya kikatili zaidi hivyo Iran isithubutu kuingia kwenye mtego wa kujaribu kupigana na Israel kwakua itapoteza kila kitu ikiwemo utawala wa Ayatollah

Rais Trump amesema Israel ina uwezo mkubwa kimedani na silaha za hatari ikiwemo za ubora wa juu mno zinazozalishwa Marekani na mbaya zaidi inajua kuzitumia kwa usahihi mkubwa

Trump anasema aliipa Iran siku 60 kusaini makubaliano ila ikazembea nafasi hiyo hatimaye usiku wa kuamkia leo ambapo ilikuwa ni siku ya 61 Israel ikachukua hatua kali. Trump anasema aliionya Iran kwamba inaweza kukumbana na hatua ambazo haijawahi kushuhudia, kuambiwa au kusikia ila ikawa haiamini ikadhani ni vitisho vitupu tu

Rais Trump amesema jambo lenye tija kwa sasa kwa Iran ni kuchangamkia fursa ya mazungumzo kukwepa mkono zaidi wa Israel, fursa ambayo ameiita kama nafasi ya pili "Second Chance" na kuitaka Iran kuitumia haraka kabla mambo hayajaharibika kabisa

Wakati huo huo rais wa Iran Masoud Pezeshkian amelaani mashambulizi ya Israel na kuapa kwamba lazima Iran ilipize kisasi chenye uzito unaostahili

Je Iran itajibu ili kupata awamu ya pili ya mashambulizi ya Israel?.

View attachment 3367116
Hivi trump ana afisa habari ofisi kwake!? Maana anavyoongea mara nyingi yupo mbele ya muda.
 
Dawa ya US ni kwenda nae kibabe ,kama Bwana kiduku alivyo fanya hadi saivi ana Nukes
Sasa uzuri wa kiduku anaenda Nate kibabe huku anafanya mipango bila kupigana na nchi yoyote ile. Shida ya Iran anafanya ubabe huku anafadhili vikundi vya kupigana na israel. Hama's hizbullah wayouth. Ndiyo shida ilipo
 
Back
Top Bottom