Iran Yaitunishia Kifua Marekani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Iran Yaitunishia Kifua Marekani

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbonea, Sep 29, 2009.

 1. Mbonea

  Mbonea JF-Expert Member

  #1
  Sep 29, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 640
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33


  Kombora la masafa marefu la Iran, Shahab-3 Tuesday, September 29, 2009 6:20 AM
  Zikiwa ni siku chache kabla ya Iran kukutana mataifa sita makubwa duniani kujadili mitambo yake Nyuklia, Iran imefanya majaribio ya makombora yake ya masafa marefu ambayo yana uwezo wa kufika hadi Israel na nchi za umoja wa Ulaya. Wakati zikiwa zimebakia siku chache kabla ya mataifa makubwa sita duniani kukutana na Iran jijini Geneva, Uswizi kujadili mitambo ya nyuklia ya Iran, Iran imefanya majaribio ya makombora yake ya masafa marefu yanayoitwa Shahab-3 na Sajjil.

  Makombora hayo yana uwezo wa kwenda kilomita 2000 na hivyo kuzifanya nchi za Israel, Uturuki, Syria na sehemu za kusini mwa Ugiriki kuwa miongoni mwa maeneo ambayo makombora hayo yanaweza kushambulia.

  Makombora hayo pia yana uwezo wa kuvishambulia vituo vya kijeshi vya Marekani vlivyopo kwenye nchi za ghuba.

  Mwishoni mwa wiki iliyopita Iran ilifanya majaribio ya makombora yake ya masafa mafupi na ilitamba kwamba majaribio hayo yalimalizika kwa kuonyesha mafanikio makubwa.

  Kesho kutwa, alhamisi wajumbe wa nchi tano wanachama wa kudumu katika Baraza la Usalama yaani Marekani, Ufaransa, Urusi, Uingereza, China pamoja na Ujerumani watakutana na Iran mjini Geneva, Uswizi kujadili mitambo ya silaha za nyuklia ambayo Iran inatuhumiwa kuijenga kwa siri.

  Hata hivyo Iran ilisema kwamba katika mkutano huo inataka kuzungumzia masuala ya kimataifa zaidi na sio mradi wake wa nyuklia na kuongeza kwamba mradi huo wa nyuklia ni wa kuzalisha nishati kwa matumizi ya amani.

  Mataifa ya magharibi yametishia kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Iran iwapo haitaonyesha ushirikiano.

  Miongoni mwa vikwazo ambavyo vimetajwa ni kuzuia biashara ya mafuta ya Iran na kuziwekea vikwazo benki zake.
  Source: NIFAHAMISHE.COM
   
Loading...