Iran yailaumu Israel kwa shambulio la ndege isiyo na rubani yaonya, kulipiza kisasi

EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
21,713
35,525

Iran yailaumu Israel kwa shambulio la ndege isiyo na rubani yaonya, kulipiza kisasi​

.

Iran imeilaumu Israel kwa shambulio la ndege isiyo na rubani kwenye eneo la kijeshi katikati mwa mji wa Isfahan siku ya Jumamosi.

Balozi wake katika Umoja wa Mataifa alisema matokeo hayo yalionyesha kuwa Israel "ilihusika na jaribio hilo la uchokozi".

Iran, alisema, inahifadhi haki "ya kujibu kwa uthabiti vitisho vyovyote au vitendo viovu" vya Israel.

Israel haijathibitisha au kukanusha kuwa ilihusika na shambulio hilo, ambalo Iran ilisema lilisababisha uharibifu mdogo, ingawa hii haijathibitishwa.

Nchi hizo mbili ni maadui wakubwa na katika miaka ya hivi karibuni zimekuwa zikishiriki katika kile kilichoelezwa kuwa ni "vita kivuli" vya mashambulizi yasiyodaiwa dhidi ya mali, miundombinu na raia wa kila mmoja wao.

Israel inajulikana zaidi kufanya mashambulizi kwa kile inachosema kuwa ni uhamisho wa silaha za Iran kwa wanamgambo nchini Lebanon na pia inaaminika kuhujumu maeneo ya nyuklia ya Iran na kuwaua wanasayansi wa nyuklia wa Iran.

Iran, ambayo inakataa haki ya Israel kuwepo, imeshutumiwa na Israel kwa kupanga kushambulia raia wa Israel na Wayahudi. Kila upande pia unaaminika kushambulia meli ya mwingine.

Katika barua kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, balozi wa Iran Amir Saeid Iravani aliishutumu Israel kwa "jaribio... la kuanzisha shambulio la kigaidi dhidi ya uwanja wa warsha" wa wizara ya ulinzi ya Iran. Hakubainisha ni ushahidi gani Iran inao kwa hili.

Bw Iravani alisema Iran ina haki ya kujibu "popote na wakati wowote inapoonekana inafaa".

Madhumuni ya eneo lililoshambuliwa haijulikani, ingawa ripoti zinaonyesha kuwa inaweza kuhusishwa na utengenezaji wa makombora
 
hawezi hata siku moja. israel sio kama marekani. ukipiga israel lazima na yeye akupige na sio kukupiga tu, ni kukupiga hadi paume na usirudie tena.
Saivi anapigana kuuziwa F15XE huo mzigo ni advanced kuliko F16 Falcon unadiziwa na F35 ni stealthy features tu.

Inabeba mabomu mazito zaidi anawaza kufanya kila alifanya Iraq na Syria nuclear facilities
 
Tutegemee uhasama kushamiri zaidi.
atakachofanya iran pekee ni kuwapa silaha hamas au hezbolah wazirushe israel, na israel atajibu kwa kubomoa magorofa ya Gaza na Lebanon, na kuua watu. mwisho wa siku iran ataanza tena kutoa pesa kujenga gaza na lebanon. siku zote iran ametamka wazi kwamba wanayemwogopa ni israel wala sio marekani. usicheze na taifa la Mungu.
 
Israeezi hata siku moja. israel sio kama marekani. ukipiga israel lazima na yeye akupige na sio kukupiga tu, ni kukupiga hadi paume na usirudie tena.
Israel Hana uwezo huo kwa Iran,asingekua anabweka tu kila siku na kupiga kwa kuvizia, Iran alimuahidi USA kulipa kuuawa kwa general wake,na akalipa,huyo Israel mtegemea mabwana atapigwa kupitia Hamas na Islamic jihad
 
atakachofanya iran pekee ni kuwapa silaha hamas au hezbolah wazirushe israel, na israel atajibu kwa kubomoa magorofa ya Gaza na Lebanon, na kuua watu. mwisho wa siku iran ataanza tena kutoa pesa kujenga gaza na lebanon. siku zote iran ametamka wazi kwamba wanayemwogopa ni israel wala sio marekani. usicheze na taifa la Mungu.
Acha ufara taifa la mungu linaua ndugu zao wapalestina
 
Back
Top Bottom