Iran plans to launch satellite to GEO: IRGC chief

Iran plans to launch satellite to GEO: IRGC chief

KABAVAKO

JF-Expert Member
Joined
Apr 5, 2011
Posts
229
Reaction score
32
amiri20121111154328420.jpg
A schematic view of GEO

The commander of the Islamic Revolution Guards Corps (IRGC) says Iran will soon launch a satellite into the Geostationary Earth Orbit (GEO), a circular orbit more than 35,000 kilometers above the planet’s equator.

Major General Mohammad Ali Jafari said on Sunday that the satellite would be carried on a missile which had been developed by the senior IRGC commander, Hassan Tehrani Moqaddam, before his martyrdom a year ago.

The Iranian general added that numerous young scientists have joined the IRGC Self-Sufficiency Organization since Tehrani Moqaddam’s martyrdom to push ahead with his projects.

Jafari stated that Iran is one of the few states capable of launching satellites into GEO, adding: “With this missile and on this level, I don’t think that except for two or three countries and Iran, any other country would be capable of sending satellites into GEO.”

He emphasized that scientific progress in Iran will continue in all sectors.

“Western governments and the United States are likely to feel threatened by Iran’s scientific progress. That’s natural, but we will do our job.”

Iran launched its first indigenous satellite, Omid (Hope), in 2009. The country also sent its first biocapsule of living creatures into space in February 2010, using the indigenous Kavoshgar-3 (Explorer-3) carrier.

Moreover, in June 2011, Iran put the 15.3-kilogram Rasad (Observation) orbiter in space. Rasad's mission was to take images of the Earth and transmit them along with telemetry information to the ground stations.

Iran also launched Navid-e Elm-o Sanat (Harbinger of Science and Industry), another indigenous satellite, into orbit on February 3, 2012.

The country is one of the 24 founding members of the UN Committee on the Peaceful Uses of Outer Space, which was set up in 1959.

Tehran also plans to launch the country's first manned mission to space by 2019.
 
Halafu kuna wale wanaodai eti Uislamu ndio unaochelewesha mataifa ya Kiarabu. Kwa kweli elimu haina dini wala kabila au jinsia. Inategemea zaidi msukumo wa taifa, utashi wa mtu na kuwepo na nyenzo....basi.
Tena Iran ingekwenda mbele kwa haraka zaidi lau si vikwazo vya zaidi ya miaka thelathini. Mara kadhaa Iran imeshindwa kununua hata chuma (chuma maalum kwa vifaa hivi) ikabidi ingojee mpaka iweze yenyewe kuchimba na kutengeneza vyuma hivyo. Marekani ilizuia kuuziwa Iran fiber optics *(zinazotumiwa katika mawasiliano kama mobile phones) miaka miwili iliyopita. Miezi sita iliyopita Iran ilifikia uwezo wa kutengeneza yenyewe. Pia Marekani ilipanga kuwazuia wanaoiuzia mafuta yaliyosafishwa Iran wasimamishe. Wakati huo Iran ilikuwa ina import 40% ya mafuta yaliyosafishwa. Hivi sasa licha ya kuwa hai-import, ina export benzine, petroli, na derivatives nyingine!
Vikwazo hivi vya sasa, vikali zaidi kuwekewa nchi yeyote ile duniani, kwa madai ambayo hayajathibitishwa eti Iran ina nia ya kutengeneza silaha za nuklia- hivi sasa Iran iko katika mchakato wa kuona kuwa haiuzi mafuta ghafi kabisa. Badala yake iko mbioni ya kuweza kugeuza mafuta yote inayoyachimba kuwa bidhaa za mafuta- ikifanikiwa itakuwa nchi ya kwanza duniani net oil producer kufanya hivyo (Hata Urusi haijaweza kufikia).
Kwa wanaofahamu mambo, Iran ni nchi ya kuvuliwa kofia. Kwa kweli inapigania haki kwa niaba yetu sote. Imagine kama siku moja TZ itataka kuwa na programme ya nguvu za nuklia kwa kuzalisha umeme halafu iambiwe hapana na the arrogant forces, Tanzania ingekuwa na ubavu wa kupinga? Lakini kwa vile Iran hivi sasa inalipinga hilo, basi ni dhahiri future hakutakuwa na nchi yeyote itakayoweza kuikataza nyingine kwa kupanua ujuzi wake katika masuala ya nishati ya nuklia.
Hawa Wazungu wataka kuhodhi elimu itakayotumika siku za usoni wawe wao tu ndio wenye elimu hiyo ili waje watutoze fedha nyingi kama hivi sasa wafanyavyo katika bidhaa zao. Wanajua kuwa mafuta siku moja yatakwisha na huenda nishati ya nuklia ikawa ndiyo pekee itakayotumiwa katika vitu vingi vya mustakbali-ndege, meli,etc sasa wataka kuhodhi future za watoto na wajukuu wetu.
Lakini watu wengi hawafahamu haya. Wanajiingiza katika kundi la kuilaani Iran wakikubali hoja za Wazungu kuwa sababu pekee ya kuwa na program ya nishati ya nuklia ni kuuunda bomu la nuklia la kumpigia Mwisraeli- Mungu wa Wazungu.
 
Iran kosa inalofanya ni kuruhusu IAEA kukagua vinu vyake vya nuclear japo sio vyote, mfano Palchin na Fordo ambavyo ni underground ktk milima na bado vikawekewa superstructure cement maalum ili kuvumilia incase imevamiwa kivita hadi US wamekubali kua zile bunkebuster walizonazo haziwezi penetrate ile cement ya iran...Iran inapaswa kuisisitiza IAEA kwenda kukaguwa shuguri zote zinazofanywa na ISrael ktk kinu chake cha DEMONA apo itakua inatenda haki....Kuhusu progress IRAN inatisha imagine North korea na QUBA zilivyo hoi kwa sasa thats why ktk hii dunia ambayo inafumba macho upande fulani you must be aggresive...US,UK na UEwametambua kua vikwazo dhidi ya IRAN imewafanya sio wakome na waache ila ndo imewapa chachu ya maendeleo kwani wameweza kutengeneza fighter jets,warships,submarine,missiles,medicine,cars etc na sasa satellite imefikia mpaka Germany wanatengenezewa super tankers na Iran apo ujue wapo mbali...
 
.................."Western governments and the United States are likely to feel threatened by Iran's scientific progress. That's natural, but we will do our job." .............................................

nimefurahiswa na kauli hiyo.
 
Lakini week chache zlizo pita wananchi wa Iran walikuwa wanalia kuwa khali ya uchumi siyo nzuri, na pia kushuka kwa thamani ya pesa yao dhidi ya USA dollar,so bidhaa na uduma zimepanda bei gafla zaidi ya 50%
Pili kabla ya USA election, Aljazeera walionyesha maonyesho ya ndege, manwari na meli za kijeshi za marekani katika gulf ya Oman ambayo hayajawai kuonekana, na shughuli hiyo wakialikwa wahandashi wa habari wa vyombo mbali mbali vya kimataifa na ambao waliambiwa wafikishe ujumbe (nadhani walengwa walikuwa, china, Russia, na Iran).
So nadhani hapa watu wanaonyeshana nani zaidi
 
Even mimi na feel threatened. Yaani hawa jamaa watakuwa wanatunasa kama filamu wakiwa angani nasisi hatuwaoni? Wakiamua kujitoa muhanga na missile sinazo ongozwa na hiyo GEO kitu wote tunaisha. Naomba wayahudi watusaidie kutungua hiyo mitambo ya wa iran.
 
Haya ni matusi. Si jambo la kawaida mtu kujitoa mhanga. Wanaojitoa mhanga kwa kuua watu wasio na hatia ni watu waliochanganyikiwa na hawana uhusiano kwa vyovyote na Uislamu. Dini hii ni ya amani kamili na wala usiwe na shaka nayo. Kuna watu wameingiza siasa chafu katika Uislamu na miongoni mwao ni Marekani yenyewe iliyomuandaa Osama bin Laden na Alqaida yake ili kupambana na ukomunist.
 
Mkuu kwanini unautetea Uislamu wakati mimi sijautaja mahali popote? Au unamaanisha Waislamu tu ndio ruksa kujitoa mhanga. Nilikuwa sijui
 
Mkuu kwanini unautetea Uislamu wakati mimi sijautaja mahali popote? Au unamaanisha Waislamu tu ndio ruksa kujitoa mhanga. Nilikuwa sijui
Akutukanaye hakuchagulii tusi. Hapo unarudia matusi ya kwamba waislamu ni tatizo kwa kujitoa mhanga. Lakini unafahamu ukweli kuwa wajitoao mhanga wameajiliwa na mashirika ya kijasusi ya nchi za magharibi kwa maslahi ya nchi hizo. Mkuu wa ugaidi duniani ni Marekani akifuatiwa na Israel na Uingereza lakini umefumbia macho maovu yao.
 
Even mimi na feel threatened. Yaani hawa jamaa watakuwa wanatunasa kama filamu wakiwa angani nasisi hatuwaoni? Wakiamua kujitoa muhanga na missile sinazo ongozwa na hiyo GEO kitu wote tunaisha. Naomba wayahudi watusaidie kutungua hiyo mitambo ya wa iran.
Je hao walonazo ( ukitoa wairan) hawawezi kutushambulia ? Kumbuka marekani weshawahi kupiga nyuklia Japan , Uingereza ilishatuma meli yenye nyuklia kuipiga Argentina katika vita vya ISLAS MALVINAS / FALKLAND ISLANDS ( hawakuwahi kuipiga kwani kabla meli hiyo kufika walishapata ushindi ). Nionavyo ni kuwa hizi silaha zipigwe marufuku dunia nzima.
 
Lakini week chache zlizo pita wananchi wa Iran walikuwa wanalia kuwa khali ya uchumi siyo nzuri, na pia kushuka kwa thamani ya pesa yao dhidi ya USA dollar,so bidhaa na uduma zimepanda bei gafla zaidi ya 50%
Pili kabla ya USA election, Aljazeera walionyesha maonyesho ya ndege, manwari na meli za kijeshi za marekani katika gulf ya Oman ambayo hayajawai kuonekana, na shughuli hiyo wakialikwa wahandashi wa habari wa vyombo mbali mbali vya kimataifa na ambao waliambiwa wafikishe ujumbe (nadhani walengwa walikuwa, china, Russia, na Iran).
So nadhani hapa watu wanaonyeshana nani zaidi

Hapo kwenye Red mkuu unatudanganya, hivi unawafahamu WARUSI? URUSI ndo Taifa Pekee lenye Makombora Ya hatari kabisa mkuu, USA unafahamu hilo, Ka google uone Siraha za URUSI

R-36; NATO reporting name: SS-18 Satan
 
Je hao walonazo ( ukitoa wairan) hawawezi kutushambulia ? Kumbuka marekani weshawahi kupiga nyuklia Japan , Uingereza ilishatuma meli yenye nyuklia kuipiga Argentina katika vita vya ISLAS MALVINAS / FALKLAND ISLANDS ( hawakuwahi kuipiga kwani kabla meli hiyo kufika walishapata ushindi ). Nionavyo ni kuwa hizi silaha zipigwe marufuku dunia nzima.

Nakubali zipigwe marufuku kuliko wa iran wawe nazo. Wale hawaelewiki wakiamka vibaya, kwishney.
 
Akutukanaye hakuchagulii tusi. Hapo unarudia matusi ya kwamba waislamu ni tatizo kwa kujitoa mhanga. Lakini unafahamu ukweli kuwa wajitoao mhanga wameajiliwa na mashirika ya kijasusi ya nchi za magharibi kwa maslahi ya nchi hizo. Mkuu wa ugaidi duniani ni Marekani akifuatiwa na Israel na Uingereza lakini umefumbia macho maovu yao.

Mkuu naomba uwache kabisa kutaja dini kwenye mada ambazo hazihusu dini. Watu wamekuwa sensitive siku hizi, sio kama zamani. Nahisi ulimwengu unatafuta sababu za kuisha
 
Wairan wanaiga mataifa makubwa , kama hofu ya fujo na vita vibaya , vipo tokea ilipoundwa UN kwa mtindo wa upendeleo , mataifa 5 kuwa na kura ya turufu , je huoni kuwa huu ni upendeleo usio na maana ? mimi nikifanya kwa kuwa ni taifa dogo nitawekewa vikwazo au hata kuvamiwa , wao wakifanya nani atawahukumu ? hakuna usawa na tunadanganyana kuwa sote ni sawa.wameshika mpini ! tufikirie ....
 
Back
Top Bottom